google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWISHO USHAAMRIWA

 UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 20.10.2024
ASKOFU DKT JOSPHAT GWAJIMA
SOMO:MWISHO USHAAMRIWA.


Mwisho wako Mungu alishaamua tangu mwanzo hatakama unajionaje sasa, kuna wakati mgumu unapitia ila mwisho wako ulishamriwa  kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu Mungu alishaamua mwisho wako/hatima yako.

“kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi; nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.”Isaya 46:9-10

Hakuna mtu anayeweza kutengeneza mwisho wa mtu ila Mungu ndio anayoijua mwisho wa mtu kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu. unaweza ukapitia mambo magumu ila mwisho wako ulishaamuliwa unapitia mambo hayo ili yaweze kukutengeneza ili uweze kwenda kwenye hatima yako ambayo Mungu ameshaiamua kuna wakati watu watakutenga na kukukataa ila kuna wakati watahitaji msaada wako kwasababu mwisho wangu ulishaamliwa.

“Ndipo Yeftha akawakimbia hao nduguze, akakaa katika nchi ya Tobu; na watu mabaradhuli walikwenda na kutangamana na Yeftha, wakatoka kwenda pamoja naye.Ikawa baadaye, wana wa Amoni wakapigana na Israeli. Ikatukia, hapo wana wa Amoni walipopigana na Israeli, wazee wa Gileadi wakaenda kumtwaa huyo Yeftha katika ile nchi ya Tobu;” Waamuzi11:3-5

Watu wanawahukumu mtu kwanamna alivyo na kumtenga kwasababu hawajui mwisho wa mtu ndio maana baada ya mwisho wa mtu kudhihirika ndipo watu wanajuta na kutaka kumwomba msamaha mtu huyo kama ilivyo kuwa kwa Yefta. Mungu anaficha miujiza kwa yule anayechukiwa.

“Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi, Je! Ninyi hamkunichukia mimi na kunifukuza nitoke katika nyumba ya baba yangu? Basi kwani kunijilia hivi sasa wakati mlio katika taabu?” Waamuzi11:7 

Adui wa mafanikio ni mafanikio unayo yapata kwa muda mfupi na kumfanya ashindwe kumtafuta Mungu kwa bidii na baada ya hapo inapelekea mtu kucheleweshwa kwenye mafinikio na ili uweze kurudi kwenye asili yako na kuendelea kupambana ili kuweza kupata mafanikio yako kwa Kuomba kwa bidii ili kuweza kwenda kwenye mafanikio yako.

Muujiza unakuja kwa mambo mawili

     i.    1. Kuamini

    ii.   2. Kutamka neno

Kuna mambo mtu anayafanya pasipo yeye kutegemea kwasababu tayari mwisho wako ulishaamriwa. Kuna mambo mtu anapitia sio kwasababu unaomba sana ila ile hatima yako inakulinda. hatima ina thamani sana inakubidii uielekee  kwasababu usipoielekea utaijutia baadae. Kila mtu ana hatima yake na kunawakati hatima ya mtu ipo kwa mtu unaye mfuata na kumsikiliza anaweza akawa mtumishi wa Mungu kama ilivyo kwa Yoshua alimfuata Musa.

kuna kuinuliwa kwengine inabidi hadi pale mtu mmoja aweze kuinuliwa kama ili vyo kwa yesu kuinuliwa. Kunawakati lazima mtu aporomoka ili uweze kuchukua nafasi ambayo mtu ayeistahili kama ilivyo kwa Esta kuwa malikia baada ya mke wa mfalme alipokuwa anakiburi.

“Ndipo mfalme alipomnyoshea Esta fimbo yake ya dhahabu. Basi Esta akaondoka, akasimama mbele ya mfalme.” Esta 8:4

“MWISHO WAKO ULISHAAMRIWA NA MUNGU KABLA YA KUUMBWA KWA MISINGI YA ULIMWENGU”AMEN

 

Post a Comment

0 Comments