UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 15.12.2024
ASKOFU DR JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO:
INUKENI ENYI MALANGO YA MILELE MFALME WA UTUKUFU APATE KUINGIA
Paulo na sila walipokuwa gerezani walikuwa wanaomba na kumwimbia Mungu sifa na misingi ya gereza ikatikisika na milango ya gereza ikafunguka. Kwenye andiko hili lina tufundisha pale tunapo omba na kusifu kwa roho na kweli kuna milango ambayo iliyo fungwa kwenye Maisha. Kwa kuomba na kusifu kwa roho na kweli milango hiyo itafunguliwa kwenye Maisha yako. Kuna mambo shetani anataka kukuaminisha vitu na kuona baadhi ya mambo kuwa hayawezekani ili aweze kukukatisha tamaa, kwa kuomba unamzuia shetani asikujaribu pamoja na ushawishi wake.
“Lakini panapo usiku wa manane Paulo
na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa
wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata
misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya
wote vikalegezwa. Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa
milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa
wafungwa wamekimbia.” Matendo ya mitume 16:25-27
Kuna
mambo Yesu aliyafanya nayo yalikuwa ni miujiza ili kuweza kuweka Imani kwaajili
ya wakati wa mwisho, kama vile yesu kumuita Lazaro ambaye alikuwa amekufa naye Lazaro
akatoka kaburini. Hii inatufundisha kuwa Imani ndio msingi mkubwa na ina thamani
ambayo inaweza kufanya mambo ambayo kwa mtazamo wa kibinadamu haiweezekani ila unapokuwa
na imani inawezekana.
“Yesu
akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? Basi
wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru
kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini
kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki
kwamba ndiwe uliyenituma. Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu,
Lazaro, njoo huku nje. Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni
na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni,
mkamwache aende zake.” Yohana 11:40-44.
kuna
mambo Mungu ametupatia ili tuweze kuitumia ila kuna mambo mtu amefungwa kwasababu
ya mkuu wa anga kuwa funga watuwasione vile vitu ila pale unapo omba unamfunga
mkuu wa anga nawe unaanza kufunguliwa na kuona vile vitu ambavyo Mungu
amekupatia na kupata akili ya kuitumia.
“Mwenye
hekima huupandia mji wao wenye nguvu; Na kuziangusha nguvu za tumaini lao.” Mithali
21:20
Thamani ya Maisha ya mtu ni ya thamani kuliko kitu chochote ila kwasababu watu wamefunga fikla zao, Kwa kuomba inatusaidia kufungua akili ya kujua uthamani wake kwenye Taifa.
“Ni
nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole?Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye
mguno?Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu?Ni nani aliye na macho mekundu?Ni
wale wakaao sana kwenye mvinyo;Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.Usiitazame
mvinyo iwapo ni nyekundu;Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;Mwisho
wake huuma kama nyoka;Huchoma kama fira.Macho yako yataona mambo mageni;Na moyo
wako utatoa yaliyopotoka.” Mithali 23:29-33
0 Comments