google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWISHO WAKO ULISHA AMRIWA TANGU ZAMANI

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 27.10.2024
ASKOFU DKT JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: MWISHO WAKO ULISHA AMRIWA TANGU ZAMANI

Hatima yako ilishaamriwa na Mungu kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu kuwa  utakuwa nani. haijalishi watu watasema nini na kuna wakati mtu anaona kuwa ni bahati ila sio bahati ila kwasababu mwisho wako ulishaamriwa na Mungu. 

“kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi; nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.” Isaya 46:9-10

Mungu alikuwepo hakuwa na mwanzo wala mwisho yeye alikuwepo milele naye anatangaza mwisho wa mtu tangu mwanzoni na hakuna mtu anaye weza kujipangia mwisho wake. Mwisho ulishapangiwa na Mungu na mwisho huo ni mwema.

“Neno la BWANA lilinijia, kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.” Yeremia 1:4-5

Mungu pia anawatumia wanao kuchukia ili wakusogeza kule Mungu alipo kukusudia. Mungu anatangaza mwisho wa mtu tangu mwanzo kwa kutamka neno hilo mara kwa mara ili jambo hilo litimie kwasababu neno ndio kinacho umba kitu na pasiwepo na kitu cha kukizuia. Utu una maana kuliko dhehebu. mafanikio ya mtu hayaji kwasababu ya bidii yako ila inatoka kwa Mungu.

“Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.” Luka1:31

Pale Mungu anapotamka neno juu ya mtu neno lake lazima litimie. Mungu akitaka kubariki hakupi pesa ila anakupa neno ambalo neno hilo litabadilisha maisha yako na kuyaishi sawasawa na mwisho ambao Mungu aliishaamua kabla ya kuubwa kwa misingi ya ulimwengu.

“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.” Yohana 1:1-3

Pesa haibadilishi tabia ya mtu ila inadhihirisha tabia halisi ya mtu alionayo pale anapo pata pesa, pale mtu anapo pata pesa ndivyo marafiki wanaonekana lakini pale anapo kosa pesa ndivyo marafiki wanaondoka kwasababu ya mali yako na wala sio upendo wa kweli.

Wewe ni roho unaye kaa ndani ya mwili ambao ni mavumbi. wewe ulikuwa mbinguni na ukatumwa na Mungu na ukaingia kwenye mwili ambao ulikuwa tumboni mwa mama yako na kuzaliwa ukiwa ndani mwili. Mungu anajua mwisho wako kwasababu miisho ina fanana kwa hiyo Mungu anakukutanisha na watu wenye mwisho unaofanana. kama ilivyo kuwa kwa bwana Yesu alikutanishwa na wanafunzi kumi na wawili (12).

Kwakupitia hatima ya mtu mmoja inaweza kusababisha watu wakapanda kutokana na hatima ya mtu mmoja na mwingine akashuka. Tujifunze kuishi kwa amani na watu kwamaana kesho ndiyo Mungu anajua atakaye mtumia nani wa kukupeleka kwenye hatima yako. akili kubwa kuliko zote ni kuishi vizuri na watu.

Kutokukubaliwa na watu habadilishi hatima yako kwa maana mtu akipendwa sana haitoshi na kuchukiwa tu haitoshi. kiongozi yeyote inakubidi umuheshimu kukuchukia kwake haizuii hatima yako inakubidi uwe mnyenyekevu.

“Hakika yake huwadharau wenye dharau,Bali huwapa wanyenyekevu neema.Wenye hekima wataurithi utukufu,Bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha.” Mithali 3:34-35

Mungu akitaka jambo ni lazima litimie na hakuna mtu wakuizuia. Usijipe mawazo kunawatu lazima watakupenda na kuna watu ni lazima watakuchukia. vitu vinapungua thamani pale vinapo patikana kwa urahisi. Hakuna siri ya milele kwasababu kila siri ni lazima itaonakana. inakubidi utende wema juu ya kila mtu kwa maana kesho ya mtu Mungu anaweza kumtumia mtu ambaye haukumtegemea.

 Mtu akiwa na nguvu akazungukwa na watu dhaifu yeye nae atakuwa dhaifu na pia mtu dhaifu akizungukwa na watu wenye nguvu naye atakuwa na nguvu. Silaha mjinga huwa nikujipendekeza na lakini mwenye akili ni anataka kueleza ukweli ili tatizo hilo ili lipatiwe jawabu. Ni lazima ujizungushie watu wenye nguvu ili uwe imara/jabali.

Mambo maanne ili kupata watu wenye nguvu kwakuyaangalia mambo yafuatayo

1.    Kuambatana

2.    Muda

3.    Maarifa

4.     Matokeo.

“USHUJAA HAUANZI ILA ULIKUSHAKUWEPO KABLA YA KUUMBWA KWA MISINGI YA ULIMWENGU” AMEN.

 "BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA NZIMA YA JUMAPILI"


 

 

Post a Comment

0 Comments