UFUFUO NA UZIMA
CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI
03.11.2024
ASKOFU BARAKA
THOMAS TEGGE
SOMO: BWANA YU PAMOJA NAWE MTU
SHUJAA
“Neno la BWANA lilinijia, kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.” Yeremia1:4
Vile mtu anavyojiona ni tofauti na watu wengine wanavyomuona. Mtu unavyojiona ina nguvu kuliko watu wengine wanavyomuona. Mungu anawezaa kumbadilisha yule mtu aliyekuwa muovu na kuwa mtu mwema. Mungu yupo pamoja na mtu hatakama anapitia changamoto.
Mtu wa rohoni
anavyojiona ni tofauti na mtu wa mwilini anavyomuona mtu. Ukifuata ule mtazamo
wa rohoni utaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu na kufanya hivyo haijalishi
unapitia nini utakuwa imara tu. Unapomuomba Mungu anakukirimia yale yakupasayo
kuyafanya ili kuweza kutimiza kusudi alilokupa kabla ya kuumbwa kwa misingi ya
ulimwengu.
Mungu haangali kama wanadamu wanavyoangalia. Ili kuweza kujua Mungu anavyokuona wewe anatumia
mtu ili kuweza kujua namna Mungu anavyokuona.
Wewe ni shujaa
una uwezo wa kufanya mambo makubwa bila wewe kujua una huo uwezo kama ilivyokuwa kwa Gidioni. Gidioni alijiona kuwa hawezi ila Mungu alimwambia aende kuwaokoa wanaisraeli.
“BWANA
akamtazama, akasema, Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa
Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma?” Waamuzi 6:14
Ukiwa ndani ya Mungu
unakuwa salama haijalishi kuna mambo gani unayapitia. Hauwezi kupatwa na
mabaya kwa maana Mungu yupo upande wako. Inakubidi usiogope kwa jambo
lolote unalolipitia kwa maana Bwana ndio tumaini lako. Kuna mambo makubwa na
mazuri mtu anayafanya kwa sababu Mungu yupo ndani yake. Inakubidi usiwe na hofu
kwa maana hofu pia ni roho ya shetani.
“usiogope, kwa
maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia
nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.”
Isaya 41:10
Mungu hawa haangalii
kama binadamu kwa sababu mwisho wa mtu ulishaamriwa na Mungu kabla ya kuumbwa
kwa misingi ya ulimwengu. Haijalishi mtu huyo ni wa aina gani kama ilivyo kwa
Gidioni ambapo baba yake alikuwa anaabudu miungu mingine, au Sauli ambaye ni Paulo
ambaye alikuwa anaua watumishi wa Mungu ila Mungu aliwatumia kufanya mambo
makubwa yaliyo mapenzi yake.
“WEWE NI SHUJAA
MUNGU YUPO PAMOJA NAWE” AMEN
0 Comments