google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MALAIKA WAKUFANIKISHA NJIA YAKO

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 17.11.2024
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO: MALAIKA WAKUFANIKISHA NJIA YAKO

Ikonjia unaopaswa kuifuata pale unapo ongozwa na Mungu, Mungu ni roho ambaye anayo namna ya kumuongoza mtu ambaye ni wewe na Mungu ili akuongoze anatuma Malaika. Malaika hao wanaweza wakawa kwa namna ya rohoni na Maliaka pia wakawa kwa namna ya mwili. Kwa namna ya rohoni Malaika hawa wanasema na mtu kwa namna ya rohoni kwa kumuekea mtu kutaka au kuwa na shauku na inakubidi kufuata kile Malaika alicho kuonesha.

“Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye malaika wake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa miali ya moto.” Ebrania1:7

Inakubidi kufuata zile hatua ambazo Mungu anakuongoza na kuzifanya kwa maana zina faida na ndio njia sahihi Mungu alipokuongoza. Elimu haiwezi kukusadia kama hauto ongozwa na Mungu kwa kutumia Malaika zake. Lakini pale unaongozwa na Mungu haijalishi umesoma au hajasama. watu wengi wanashidwa kuwa imara kwasababu hawakuongozwa na Mungu.

Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama. Zaburi 32:8

Kuna viumbe rohoni wanatumwa na Mungu iliwawezekukupeleka mahali Mungu alipokuandalia viumbe hao ni Malaika, hao kazi yao kukulinda ukiwa unaenenda kwenye njia yako kwasababu shetani pia anawatumia viumbe wake ili kuweza kukuzuia kwenye ile njia ambayo Mungu amekusudia kuiendea ila kwa kupitia Malaika zake Mungu wanawazuia wale viumbe wakishetani ili wasiweze kukudhuru.

BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu,Nimwogope nani?Bwana ni ngome ya uzima wangu,Nimhofu nani?Watenda mabaya waliponikaribia,Wanile nyama yangu,Watesi wangu na adui zangu,Walijikwaa wakaanguka.3Jeshi lijapojipanga kupigana nami,Moyo wangu hautaogopa.Vita vijaponitokea,Hata hapo nitatumaini..Zaburi27:2

Mungu anamtumia mtu na shetani anamtumia mtu, ambapo Mungu anamtumia mtu ili aweze kukufanikisha kwenye njia aliokusudiwa na Mungu na shetani anamtumia mtu ili kuweza kuzuia kule Mungu alipo kukusudia na Mungu wanawazuia wale viumbe wakishetani ili wasiweze kukudhuru kwa kuomba.

“Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea” kutoka 23:20



Mungu anaweza kuwa na watu wake lakini watu hao wasiongozwe na Mungu, kwasababu mtu anaweza akawa na Mungu na bado akadanganywa.hii inamaanisha kwamba shetani anaweza akakudanganya kwa nama ya rohoni kwa sababu shetani anaiga ile mifumo kama ilivyo kwa Mungu kwa sababu pia shetani ni roho. Inakubidi kuomba ili kwa kupitia maombi utasababisha Malaika Mungu kuyaangusha kila uvuvio wa kishetani na kuyaenenda yale Mungu aliyo ya kusudia juu yako.

“Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.”2wakoritho11:3

Kuna mambo inakubidi kuongozwa na Mungu kwa kupita Malaika zake,inakubidi kumsemesha Malaika kwa njia ya maombi usipomsemesha hatajishugulishasha kwasababu ujamruhusu akuongoze, maombi ndio kitu kinacho mrusu akuongoze.

“Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.” Kutoka 23:20

Unapo jishugulisha na mambo ya Mungu na yeye atajishughulisha na wewe.ukiwa mtu wa rohoni kuna mambo yanakuwa kwako ni desturi kama vile kuomba, ukienda upande wa watu wanaopenda kishetani kuna mambo wanayafanya kama desturi na wanatimiza masharti.

“akasema, Ee BWANA, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.” Isaya 38:3

Mtu asipo omba kuna mambo huna kwasababu huja zungumza na Malaika kwa maombi inakusaidia kuwaruhusu Malaika waweze kukuongoza kwenye lile kusudi la Mungu. Mungu anakuwazia mema pale unapoomba unakuwa unafanya ya Mungu aliyo kuwazia mema.

“Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa. Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia. Matendo 16:25-27”

“MUNGU AMEKUWEKEA MALAIKA WA KUFANIKISHA NJIA YAKO” AMEN 

"BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA NZIMA YA JUMAPILI"

Post a Comment

0 Comments