UFUFUO
NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA
YA JUMAPILI 08.12.2024
ASKOFU
DR JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: INUKENI ENYI MALANGO YA MILELE MFALME
WA UTUKUFU AWEZE KUINGIA
Tena
itakuwa siku hiyo, asema Bwana MUNGU, nitalifanya jua litue wakati wa adhuhuri,
nami nitaitia nchi giza wakati wa nuru ya mchana. Amosi 8:9
Kila
mamlaka inayo onekana katika ulimwengu wa mwili chanzo ni katika ulimwengu wa roho
inaweza ikawa ni kwa Mungu au kwa shetani. Sio bidii ndio inayo mfanikisha mtu
hata bidii pia inatoka kwa Mungu kupitia ulimwengu wa roho ambapo Mungu
anakutumia kama chombo chake.Mungu awatafuti wenye sifa bali humchagua yoyote
na kuumpatia sifa watu wote walioko duniani ni watu wa Mungu baada ya Muda
madhehebu ili wekwa na watu, ila wote wanatoka kwa Mungu.
Na
alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia,
akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu,
atakayefanya mapenzi yangu yote. Matendo 13:22
Kuna
baadhi ya watu usiwasukilize maana ukiwasikiliza unaingia kwenye mitego kama
hawa kuku bali kuongea na baba wa uongo ambaye ni shetani naye roho ya uongo
ikamwingia naye akashawishiwa na shetani. Shida ya mwanadamu kutokukiri kuwa
amekosa maana pale unapo kosea inakubidi uombe msamaha kwa maana Mungu anasamehe.
Lakini
nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu
fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. 2wakoritho 11:3
Pale
mtu anapo funga ndoa mwanamke amewekwa na Mungu kama msaidizi ambaye atamsaidia
mwanaumwe kulitimiza kusudi la Mungu ila inakubidi kuishi na mwananke kwa akili
na pia usisikie kila ushauri. mali iliyo ibiwa ina fanya kazi sawasawa kama
vile shetani aliiba miliki kutoka kwa adamu na hiyo milki ina eendelea kufanya
kazi sawasawa.
Kadhalika
ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo
kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu
kusizuiliwe. 1 Petro 3:7
Kuna nchi katika ulimwengu
wa roho ina mkuu wa anga lake ndio maana kuna mataifa wanafanya mambo maovu na
kuya sapoti kwa sababu kuna mkuu wa anga wake. Yule anayetawala anaitwa mwenye
nguvu wa anga.viumbe hao wanakaa angani ndipo akimwona mtu mwovu na anayefanya
mambo maovu na viumbe wanao kaa angani
na kuingia ndani ya mtu. Kuna namna ya
kumshinda mwenye nguvu
I. I.Uwe mwenye nguvu kuliko yeye
Ili
uwe mwenye nguvu inakubidi umkiri Yesu na baada ya kumkiri yesu inafanyika kuwa
mwana wa Mungu
II.
unamwendea
III.
Unamfunga
IV.
Kumkanyaga silaha anazo zitegemea
V.
kuwagawa mateka wake
Hawezi
mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake,
asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake. marko
2:27
0 Comments