UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 22.12.2024
ASKOFU DR JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO:
KESHO YAKO ILISHAAMRIWA NA MUNGU
Nyuma ya kila mwanadamu kuna mamlaka iliyomuweka. Ukimuona ng’ombe yupo juu ya tawi kwenye mti anakula majani, amewekwa. Yeremia alijulishwa kuwa kachaguliwa alipokuwa kijana sasa. Yeremia. Kila mtu kuna kazi kapewa ya kutimiza hapa duniani.
“Maneno ya Yeremia, mwana wa
Hilkia, mmoja wa makuhani waliokuwa katika Anathothi, katika nchi ya
Benyamini; ambaye neno la BWANA lilimjia katika siku za Yosia, mwana wa Amoni,
mfalme wa Yuda, katika mwaka wa kumi na tatu wa kumiliki kwake. Tena lilikuja
siku za Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, hata mwisho wa mwaka wa
kumi na mmoja wa Sedekia, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; hata wakati
ulipochukuliwa mateka Yerusalemu, katika mwezi wa tano. Neno la BWANA
lilinijia, kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla
hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. Ndipo
niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto. Lakini
BWANA akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu
nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru. Usiogope kwa
sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema BWANA.” Yeremia 1:1-8
Yeremia anaambiwa maneno haya akiwa mtoto, lakini
haiondoi kuwa alikuwepo tangu hajazaliwa. Yesu hakuanza kuwa Mungu alipozaliwa
la hasha, alikuwepo tangu hajazaliwa. Yesu alikuwa ni mwana kondoo aliyekwisha
chinjwa mbinguni, wito wake wa kufa baada alikuja nao kabla hajaziliwa. Hakuna
wakukuondolea wito uliopewa na Mungu.
“Nami niliaminilo ndilo hili, ya
kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo
Yesu.” Wafilipi 1:6
Mpango wa Mungu unaanzia juu kabisa, kabla
hujaziliwa ulishapangiwa utakuwa nani. Kabla mbingu na nchi hazijaumbwa hatima
yako ilipangwa kabla. Pamoja na magumu unayopitia, mpango wa Mungu juu yako uko
palepale.
Wewe unaonekana wa kawaida nje lakini mtu mwenye
uwezo wa rohoni anakuona kama mtu mwenye uwezo mkubwa sana. Kuzimu inakuona
vile ulivyo. Yeremia alikuwa mtoto lakini Mungu alimuona kama mtu mkubwa sana.
Badiliko la mtu huwa linamahala pakutokea (turning point – mahala ambapo Maisha
hugeukia). Yesu alikuwa wa kawaida mtoto wa seremala lakini alipofika
thelathini ndipo alipoanza kutekeleza kusudi lake. Kuanza kutumikia shauri la
mbinguni ni muda mchache.
Kwa maana kila kitu kilichozaliwa
na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu,
hiyo imani yetu. 1Yohana5:4
Wewe umeshuka kutoka mbinguni na hatima yako. You
are sharpened. Kazi iliyomleta Yesu duniani aliifanya kwa miaka mitatu tu, ila
kazi ambazo hakuitiwa kama useremala alifanya muda mrefu zaidi. Sara aliletwa
duniani kuleta uzao wa Mungu, ikafika ukomo wa kuzaa mpaka malaika alipokuja
kumjuza habari akacheka, hakuamini. Uwezo ulionao leo haumui utakuwa nani.
Ndipo Ibrahimu akaanguka kifudifudi
akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia, kwake atazaliwa mtoto?
Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa? Mwanzo 17:17
Kuna wakati mwingine Mungu anakufunga usijue wewe ni nani ili usije ukawaringia watu. Wewe ulipotoka mbinguni umepangiwa kuwa mtu fulani, hapo ulipo sio penyewe. Mungu anakupigisha hatua polepole mpaka ufike kwenye hatima yako.
"Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La." yohana 1:21
0 Comments