UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 29.12.2024
ASKOFU DR JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: KUVUNJA MADHABAHU YA KISHETANI
Maadui wengi wa watu wa Mungu huwa wanatafutiwa sababu yoyote ili ya kutaka kumwangamizwa. kwenye biblia Yesu alikuwa anatafutiwa sababu na maadui zake ambao ni watu wa wayahudi lakini kila sababu wananayo itafuta na kushindwa kupata. Kwa watu wa Mungu kila jambo baya walilo panga juu yako lita wapata wenyewe.
“Basi Pilato alipoona ya kuwa hafai
lo lote, bali ghasia inazidi tu, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya
mkutano, akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki;
yaangalieni haya ninyi wenyewe.” Mathayo 27:24
Kweli unaweza kuizuia ila kweli itadhiirika kuwa
kweli hatakama kipindi kirefu au muda mrefu kupita ila ukweli ipo siku Utadhiihirika, pale adui anapotaka kukuzuia kuna wakati mwingine inakupeleka
kwenye mapenzi ya bwana na kuwa sehemu ya kukutengeneza ili kuitimiza kusudi la
Mungu.
“Mfalme akaamuru, nao wakawaleta
wale watu waliomshitaki Danieli, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na
watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao
vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu.” Danieli 6:24
Kifo akiji kama akijatumwa kifo sio kitu bali kifo
ni mtu, hata mashetani wakitaka kuongea na mtu anatumia kinywa cha mtu na pia
Mungu akitaka kuongea na mtu anatumia kinywa cha mtu, ukimtesa mtu wa Mungu
unamnoa na kumfanya kuwa imara. Ukitaka kumuharibu mtu wa Mungu mfanye mtu wa
Mungu akastarehe maana mtu akipata baadhi vitu anasahau kumtumikia Mungu.
“Je! Sulemani, mwana wa Daudi,
hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na
mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya
mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.” Nehemia
13:26
Ukitaka kupata vitu vya Mungu shugulika na tabia
yako, kupendana kushirikiana kukaa pamoja kwasababu sisi sote ni ndugu kwa
upande mwingine adui hutumia udhaifu huo au ujinga huo waweze kukandamiza na
kuwa silaha ya kukushinda. kama tukiamua kuondoa ujinga wetu ni kuuficha
udhaifu wako.
“Basi Daudi akatoka kwenda kila
mahali alikotumwa na Sauli, akatenda kwa akili; Sauli akamweka juu ya watu wa
vita; jambo hili likawa jema machoni pa watu wote, na machoni pa watumishi wa
Sauli pia.” 1samweli 18:5
Ukifanikiwa kumfanya kufikiri na kumfanya asikie na kumfunga fikla haina haja ya kumfunga jela,ndivyo waafirika tumeacha kutawaliwa kimabavu lakini tunatawaliwa na fikra,kwa kigezo hicho inapelekea kuvunja uwaaminifu wenyewe kwa wenyewe. kanuni za kipaumbele ili tuweze kuiongoza taifa letu tunatakiwa tuwe na maono ya mda mrefu
“Pasipo maono, watu huacha
kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.” Mithali 29:18
Mabadiliko hayaendi kwa makundi bali mabadiliko
yanaenda kwa mtu mmoja, kwasababu dhambi iliingia kwa sababu ya mtu mmoja ambaye
ni adamu na kukombolewa kwa wanadamu inatokana na mtu mmoja ambaye ni yesu. Kuwasaidia
watu inatokana na utashi wa mtu. Kitu kinacho mfanya mtu kushidwa kufanya mambo
yatakayo leta mabadiliko ni hofu au uwoga na watu wanajithamini wao wenyewe
pasipo kujali wengine
“Kwa sababu kama kwa kuasi kwake
mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa
kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.” Warumi 5:19
0 Comments