UFUFUO
NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA
YA JUMAPILI 02.02.2024
ASKOFU
DR JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO:
MAOMBI
Kwa
kumuomba Mungu bila kukata tamaa ina mfanya mtu apate kile alichokiomba na
kukipata. Mungu anahitaji tumuombe bila kukoma maana kwa kadiri unavyoomba
ndivyo Mungu anavyo jibu maombi.
“Na
Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni
mvumilivu kwao? Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja
Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?” Luka 18:7-8
Mungu
anahitaji umsumbue kwa kumuomba, kwa maana Mungu anapenda pale tunapo
mnyenyekea kwa kumuomba pale unapo mwendea mara nyingi zaidi naye hupenda naye
anaona Fahari ya uumbaji wake waki nyenyekea mbele zake naye anakupatia kile unachokiomba.
“Kwa
sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea,
nayo yatakuwa yenu.” marko 11:24
Kuna
aina tofauti tofauti ya maombi;
1.Maombi
ya kinabii
Ni
aina ya maombi ambayo mtu anatamka neno nacho kinakuwa bila kuambiwa na Mungu
nacho kinakuwa kile ulicho kiomba.
Neno
la Mungu ni zaidi ya kila kitu kilichomo hapa duniani. Neno la bwana lina nguvu
kuliko kito chochote. kitu chochote ni ya muhimu ila wa muhimu zaidi ni aliye
ziumba vitu hivyo maana yeye ndiye mwenye nguvu kuliko kitu chochote na ana watoto
wake na amewapa nguvu nao wana haki.
“Macho
ya BWANA huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao.” Zaburi 34:15
Yale unayo yatafuta yapo kinyani mwako kwa kutamka neno ambalo Mungu amekupatia hayo ndiyo maombi ya kinabii. Kinywa chako ndiyo silaha ya kumshambulia adui huyo na kwa kutamka neno.
“Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.” Wafilipi 4:6
Kwenye mambo ya Mungu watu wengi usiwape maana hao wanaweza wakakupeleka kwenye mauti ila Mungu ndio mpe umpatie nafasi. Mungu akisema unafuata, kwa ufalme wa Mungu hakuna demokrasia.maombi ya kinabii yanaweza kutengeneza kitu nacho kikawa ambayo yapo sawa na mapenzi ya Mungu. Mtu wa Mungu akitamka neno juu hatakama adui atataka kubadili mbinu nyingine neno la mtu wa Mungu ni lazima itimie. Mungu anaweza kuhamsha mamlaka za dunia na kuwafanya wamshambulie yule adui
“lakini nitapeleka moto juu ya Moabu, nao utayateketeza majumba ya Keriothi; na Moabu atakufa pamoja na mshindo, na kelele, na sauti ya tarumbeta;” Amoni2:2
Unaweza ukamuona mtu kwa namna ya mwilini na kuongea naye lakini ndani yake ni Mungu anaposema na wewe na pia unaweza ukamwona mtu nje ila ndani ni shetani yupo ndani yake. mtu wa Mungu akikwambia jambo wewe fanya bila kuuliza maswali. bila nguvu za Mungu hauwezi kuzishinda nguvu za shetani, kuna mambo Mungu anarusu ili uweze kujifunza.
“Lakini watu wawili walisalia kambini, jina la mmoja aliitwa Eldadi, na jina la wa pili aliitwa Medadi; na roho ile ikawashukia; nao walikuwa miongoni mwao walioandikwa, lakini walikuwa hawakutoka kwenda hemani; nao wakatabiri kambini.” Hesabu 11:26
Ziko mamlaka za utekelezaji ambapo Malaika wana tekeleza kwa kile neno mtu wa Mungu anaposema neno, kwa kadiri unapo omba ndivyo inavyo kuwa. Mungu ametengeneza mtu naye fanana naye ambaye ndio wewe ambapo akisema mtu wa Mungu ndipo Mungu amesema.
“Baada
ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu;
na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.” Ufunuo 18:1
2. maombi yenye akili
Ni maombi ambayo unaondoa
kikwazo kwa kile ulichopewa na Mungu sasa baada kupewa unapaswa kushindana na
adui anayetaka kukuchelewesha, ni sawa mtu akupatia zawadi ya kiwanja na akakupatia
hati ya kiwanja na ila bado haja kukabidhi ila kuna mambo yanayo mfanya
asikupatie aidha kwasababu ya
0 Comments