UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 02.03.2025
ASKOFU DR JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO:
KESHO YAKO ILISHAAMULIWA MA MUNGU
Kesho
yako ilishaamuliwa na Mungu kabla haujazaliwa na ulivyo zaliwa kesho hiyo ipo
ndani yako. Mungu huwa anatangaza mwisho tangu mwanzo kama ilivyo kwa yeremia
alitabiriwa kuwa nabii wa mataifa tangu akiwa mdogo kwa maana kesho hiyo ipo ndani yake Yeremia. yeyote atakaye jaribu
kukuzuia anakuwahisha kwenye kesho yako iliyoamuliwa na Mungu.
“itangazaye
mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado;
nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.” Isaya 46:10
Kuna
wakati watu wanakufanyia ubaya ili upoteyeze ila Mungu anawatumia watu hao ili
kukupelekwa kwenye kesho yako uliowekewa na Mungu. inakupasa kufanya mema kwa watu kwa maana hujui
yupi atakaye kuvusha kuelekea kesho yako.
"Kwa maana mwenye kutisha ameangamizwa, naye mwenye dharau amekoma, nao wote watazamiao uovu wamekatiliwa mbali;" Isaya 29: 20
Ukitaka kuwa na mahusianao mazuri na Mungu pale unapoona umekosea kuwa mwepesi kuomba msamaha. kuna wakati Mungu anarusu mambo mabaya yakupate kwa lengo la kukutengeneza na kukufanya kuwa imara.
"uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi."Matendo 26:18
Majira huwa yanaonekana ila huwezi kujua muda gani majira hayo yatatokea, kipindi ambacho majira yanataka kutokea ndio shetani analeta magumu mengi ili kutaka kukuzuia ila hana uwezo wa kukuzuia kwa sababu mapenzi ya Mungu , hauwezi kuzuia kwasababu mapenzi ya Mungu ni lazima yatimie.
"Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo."Mwanzo 50: 60
Mungu anampango juu ya mtu na mpango huo hauwezi kubadilika hatakama kuna hila nyingi ndani ya mtu ila kusudi la Mungu litatimia. Mungu anatengeza ukombozi kwa namana usiyoiwaza.
"(kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye)," Warumi 9: 11
Ndugu ni hatari kuliko mtu wa mbali. Mtu unayewekeza sana kwake ndiyo mtu anaye kuwa ni adui yako mkubwa sana ila hao huwa hawakai sana. mtu huyo anajua udhaifu wako .
"Naye Yuda, yule aliyetaka kumsaliti, alipajua mahali pale; kwa sababu Yesu alikuwa akienda huko mara nyingi pamoja na wanafunzi wake."Yohana 18:2
Hakuna wema una mtendea mtu alafu Mungu asikupe thawabu yake wewe tenda wema kwasababu ni wajibu wako naye Mungu atashugulika na adui zako.ukitendewa wema au ukitenda mema usisubiri malipo kutoka kwa mtu na wala usione ni wajibu wake kukusaidia ila ni kwa neema ya Mungu. Kila alilipanga Mungu kwenye Maisha yako ni lazima yatimie.
"Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; "Warumi 13:3
Kusudi la Mungu litasimama hatakama watu wakikupinga kukudharau, kukucheka kutenga na kukusaliti na kutaka kukuangamiza ila mpango wa Mungu uko palepale. Hakuna kitu kitakacho zuia kusudi la Mungu kwa maana vyote vinatokana na Mungu, Kuna wakati kuna mambo yanatakiwa kuvunjika ili kusudi la Mungun alisimame juu yako.
"na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.Waefeso 1: 11
BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA YA JUMAPILI
0 Comments