UFUFUO NA UZIMA
CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI
23.03.2025
BISHOP BARAKA THOMAS
TEGGE
SOMO: ULIVYOZUNGUKA KWENYE MLIMA
HUU IMETOSHA.
![]() |
Wewe ni mtu wa mbinguni hata kama hauna hela au una dhambi bado utabaki kuwa mtu wa Mbinguni wewe ni roho kuna tofauti ya kuzaliwa na kushushwa anayezaliwa ni mwili anaye shuka ni roho ambaye ndio mtu na kiuingia ndani ya mwili. kuna wakati unatakiwa kumsifu Mungu hatakama unamatatizo kwa maana yeye ndio njia sahihi.
“Lakini panapo
usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za
kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.” Matendo 16:24
Mungu anaweza kuongea kuhusu
biashara yako na hatima yako kabla hata haujaiona. maneno ya Mungu ni lazima yatimie
kwa maana kila jambo matokeo yake yanaonekana kwenye ulimwengu wa roho na kuthihirika
kwenye ulimwengu wa mwili. Mungu anadesturi ya kumtengeneza mtu kabla hajaenda
kwenye lile kusudi aliompangia ili
waende sawasawa na kusudi la Mungu.
“BWANA, Mungu
wetu, alituambia huko Horebu, akasema, Mlivyokaa katika mlima huu
vyatosha; geukeni mshike safari yenu mwende nchi ya milima ya Waamori, na
mahali pote palipo karibu ya hapo, katika hiyo Araba, na nchi ya vilima-vilima,
na huko Shefela, na Negebu, na pwani-pwani, nchi ya Wakanaani, na Lebanoni,
mpaka mto huo mkubwa, mto wa Frati. Angalieni, nimewawekea nchi mbele
yenu, ingieni mkaimiliki nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, Ibrahimu, na Isaka,
na Yakobo, kwamba atawapa na uzao wao baada yao.” Kumbukumbu ya torati 1:6-8
Kuna wakati Mungu ana mambo ameweka juu yako na wakati umefika ila kwasababu ya tabia mtu anayo akipewa hiko kitu ni rahisi kupoteza Mungu anaruhusu muda usogezwe ili aweze kukutengeneza. kuna tabia ambazo sio nzuri mbele za Mungu anaruhusu mtu atengenezwe kwanza na kuwa imara baada ya hapo ndio utaweza kulifanya kusudi lake. una tabia ambazo sio nzuri mbele za Mungu anaruhusu mtu atengenezwe kwanza na kuwa imara baada ya hapo ndio utaweza kulifanya kusudi lake.
“BWANA, Mungu
wetu, alituambia huko Horebu, akasema, Mlivyokaa katika mlima huu vyatosha; geukeni
mshike safari yenu mwende nchi ya milima ya Waamori, na mahali pote palipo
karibu ya hapo, katika hiyo Araba, na nchi ya vilima-vilima, na huko Shefela,
na Negebu, na pwani-pwani, nchi ya Wakanaani, na Lebanoni, mpaka mto huo
mkubwa, mto wa Frati.” Kumbukumbu ya torati 1:6-7
Kuna mambo inakubidi uwe
na hekima inayotoka kwa Mungu kuna mambo muda wa Mungu umeshafika ila bado
haukuwa tayari kwasababu ya tabia inakufanya kukukwamisha. kwa namna unavyoishi
kuna sheria unapaswa kuifuata kutoka kwa Mungu ili uweze kufanya kusudi la hilo.
“Lakini mtu wa
kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa
ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.” Yakobo 1:5
Mambo ya Mungu yanamasharti
chochote anachokupa Mungu mfano mali, kibali, kipawa kina masharti.mfano
ukipewa pesa na mali nilazima kutoa fungu la kumi hayo masharti ni lazima
uyatimize ili ulivyo pewa uyatimize. Ndivyo kwenye ulimwengu wa giza napo ukitaka
vitu kuna masharti ni lazima kuya fuata ili uzije ukaipoteza. Masharti ni sawa
na sheria.
“Unisaidie nami
nitakuwa salama, Nami nitaziangalia amri zako daima.” Zaburi 119:117
Kikwazo kinacho mfanya mtu kushindwa kupata kile anacho kitaka kwasababu ya roho ya hofu ya kuchukua hatua. Namna ya kuishinda roho ya hofu ni kuwa na ujasiri wa kuamua jambo, ili uweze kuwa na ujasiri inakupasa kuomba, hofu pia ni sabababu ya kumfanya mtu kutokuamaua.
“Maana Mungu
hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.”2
Timotheo 1:7
Imani ina nguvu yakumfanya
mtu kutoka kuwa mtu dhaifu na kumfanya kuwa imara. kuna mambo mtu yanampata tena
ni magumu ila anawawekea Imani watu wengine kwa kuwa shauri ya kuwa inawezeka. kuna
watu kwenye jamii wanakuwa wanawatia watu hofu na kuwafanya kushidwa kuamua jambo
mfano kwenye ndoa watu hupenda kusema “ndoa si ya kuichezea na sio lelemama”. Hofu
inamfanya mtu asimiliki na kumfanya kumchelewesha kwenda kwenye kumiliki.
“Katika pendo
hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina
adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.”1 Yohana 4:11
Ulegevu wa kufanya vita
inakufanya usiumiliki, kuna mambo Mungu amekupa umiliki ila chanzo ni hofu na
kukufanya kuwa mvivuna kushindwa kufanya ahadi ya Mungu ni vizuri mtu kuwa
chini ya mamlaka ambapo inamfanya mtu kuongozwa na mtu aliyechaguliwa na Mungu kukuongoza
kwenda kwenye ile kusudi ulioitiwa.
“Kwa maana mimi
nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu;
nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya
hivi, hufanya.” Mathayo 8:9
0 Comments