google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAANA YA PASAKA

UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 20.04.2025
ASKOFU DKT JOSEPHAT GWAJIMA 
SOMO: MAANA YA PASAKA 

Maana ya pasaka ni “passover” yaani pita juu. Pasaka pia inamaanisha kupata vitu ambavyo ulivipoteza mbele ya maadui zako na kuchukua chochote kutoka kwa maadui zako. Pasaka ilikuwepo hata kabla ya Yesu kuzaliwa, kuteswa, kufa na kufufuka. Kabla ya Yesu kuja, wana wa Israel walikuwa wakisherehekea pasaka kama sehemu ya kukumbuka Mungu alivyowatoa utumwani na kuwaweka huru. 

“Musa akawaambia hao watu, kumbukeni siku hii, mliyotoka nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa; kwa kuwa BWANA aliwatoa mahali hapa kwa nguvu za mkono wake; na usiliwe mkate uliochachwa.” Kutoka 13:3

Kabla ya jambo la Mungu kutokea, Mungu huwa anaandaa mazingira ya jambo hilo. Asili ya matukio yote katika mwili ni katika ulimwengu wa roho. Kabla Yesu hajazaliwa, kusulubiwa, kufa na kufufuka maandalizi ya matukio hayo yalikuwa yameshafanywa rohoni. 

“Kwa imani sisi tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu; vitu vinavyoonekana kutoka vitu visivyoonekana.” Waebrania 3:11  

Mungu alipowapiga wa Misri kwa pigo la kumi, aliwaagiza wana wa Israel kuchinja mwanakondoo na kupaka damu yake kwenye mihimo ya malango yao ili malaika wa kifo asije kuwadhuru atakapopita kuwaangamiza wa Misri. Kwa hakisi ya agano hilo, vivyo hivyo Yesu amefanyika mwanakondoo aliyechinjwa na kwa damu yake tunapata ondolea dhambi na kwa yeye nguvu ya mauti imeharibiwa. 

“Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 30Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.” Yohana 1:29-30

Kwenye mambo ambayo shetani hawezi kukuletea ni mauti. Kinacho muuwa mtu ni hofu au kuogopa ndio maana shetani silaha yake kubwa ni hofu. Hofu inaweza kufanya mtu ashindwe kuamua jambo ambalo linamanufaa kwenye maisha yake au kushindwa kufanya kusudi la Mungu kwasababu ya uwoga. Mungu ndio asili ya kila kitu, kwa hiyo usiogope wala usifadhaike maana Mungu yupo pamoja na wewe.

“Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia.” Isaya 41:10-11

Kwa namna ile ile Yesu alivyoondoka na mawingu kwenda mbinguni, ndivyo atakavyo kuja kuwachukua watu wake yaani wote waliompokea. Hivyo njia sahihi ni moja, kumkubali Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako na kuilinda imani yako. Ni muhimu kuutafuta kwanza ufalme wa Mungu kuliko vitu vingine, maana aliempata Yesu amepata vyote. Unatakiwa utafute kwanza ufalme wa Mungu na mengine yote utazidishiwa na Mungu.

“Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” Mathayo 6:3

Kinachompeleka mtu motoni na kuangamia sio wingi wa dhambi zake bali ni ugumu wa kukubali dhambi zake na kutubu. Tengeneza maisha yako upya na Mungu, ukakumbuke ni wapi ulipoanguka, ukatubu na kusimama kuendelea mbele. Hata unapopitia magumu, endelea kumshikilia Yesu maana yeye ndio njia ya kweli na uzima. Mtu hawezi kwenda kwa Mungu bila kupitia kwake.

“Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Yohana14:6


 

Post a Comment

0 Comments