UFUFUO NA UZIMA CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 13.04.2025
ASKOFU BARAKA THOMAS TEGGE
SOMO: VIKAO VYA UHARIBIFU
![]() |
Maisha ya duniani ni akisi ya ulimwengu usioonekana ambao ni ulimwengu wa roho. Maisha ya mtu huanza katika ulimwengu wa roho na kuonekana kwenye ulimwengu wa mwili. Kuna mamlaka kwenye ulimwengu wa roho ambazo zinaamua muelekeo wa mtu kwenye ulimwengu wa mwili.
“Hapo mwanzo kulikuwako Neno,
naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo
alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye
hakikufanyika cho chote kilichofanyika.” Yohana 1:1-4
Watu wa Mungu hawafi kirahisi, maana
Mungu amewatuma kufanya kazi maalum Mtu ameletwa na Mungu kuja kuifanya kazi
yake hapa duniani, atakapomaliza kufanya kazi hiyo ndio muda wake wa kuwepo
duniani utakuwa umeisha. Hivyo sio rahisi wao kufa hadi watakapo likamilisha
kusudi la Mungu.
“Nimevipiga vita vilivyo vizuri,
mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;” 2Timotheo 4:7
Kabla ya kutokea kwa tukio lolote
zuri au baya, nyuma yake kuna vikao hufanyika katika ulimwengu wa roho. Wachawi
hufanya vikao vyao kwenye ulimwengu wa giza na baada ya hapo kuna wajumbe wa shetani hutumwa
kutekeleza maadhimio ya vikao vyao. Wajumbe hao huweza kuwawekea mawazo watu
ili wafanye mambo flani juu ya mtu na kumsababisha mtu kupatwa na matukio
mabaya. Matukio hayo ni kama vile kufilisika, ajali, magonjwa yasiyotibika, kuachwa
na mke au mume na matukio mengine mabaya.
“Mikaya akasema, Sikia basi neno
la BWANA; Nalimwona BWANA ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la
mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kuume na wa kushoto. BWANA
akasema, Ni nani atakayemdanganya Ahabu, ili akwee Ramoth-Gileadi akaanguke?
Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi. Akatoka pepo, akasimama mbele za
BWANA, akasema, Mimi nitamdanganya. BWANA akamwambia, Jinsi gani? Akasema,
Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. Akasema,
Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka ukafanye hivyo.”
1Wafalme 22:19-22
Kwenye ulimwengu wa roho yampasa mtu
wa Mungu kupigana vita kuvunja vikao na maagano ya ufalme wa giza ili kumiliki
katika ulimwengu wa mwili na kuzuia mambo mabaya yasimpate. Maombi ni namna ya
kupigana vita, ambapo unapoomba kwenye ulimwengu wa roho unaharibu vikao na
makubaliano ya ufalme wa giza.
“Kwa maana kushindana kwetu sisi
si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza
hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Waefeso 6:12
Ulimwengu wa roho ndio unaoongoza
ulimwengu wa mwili, hivyo jambo la rohoni linahitaji wa rohoni mwenzake. Hakuna
jambo lolote kwa jinsi ya mwili linaweza kuzuia jambo katika ulimwengu wa roho.
Kwakuwa mtu ni kiumbe cha rohoni, hivyo anaweza kubatilisha au kuruhusu jambo
la rohoni lisiweze kutokea ama litokee.
“Mauti na uzima huwa katika uwezo
wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.” Mithali 18:21
Asili ya nguvu kwa mtu wa Mungu
ni maombi. Maombi yanamsaidia mtu kuwa imara na kuweza kushinda upinzani kwenye
ufalme wa giza. Pia, maombi humfanya mtu aweze kumiliki kile alichopewa na Mungu
na kulitimiza kusudi lake duniani
“Nikamwelekezea Bwana Mungu uso
wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za
magunia na majivu.” Danieli 9:18
0 Comments