UFUFUO NA UZIMA
CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 11.05.2025
ASKOFU GEORGE
BILINGI
SOMO: KUWAFUNGUA WALIOCHELEWESHWA
Mashetani huwa wana mwogopa mwana wa Mungu aliye juu. Mwana wa Mungu anauwezo kuamuru mashetani waondoke ndani ya mtu. Mwana wa Mungu anaweza kuamuru kile kilicho chukuliwa na mashetani kiweze kurudishwa. Ipo namna ambayo mwana wa Mungu anaweza kurudisha kila alichoibiwa kutoka kwa shetani. Namna hiyo ni kwa kufanya vita na mashetani kwenye ulimwengu wa roho kwa njia ya maombi.
“Kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe. Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia; akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu.” Marko 5:4-8
Kuna watu wanaishi maisha mazuri
na wanamiliki vitu ambavyo sio vya kwao. Watu hao wanaweza kutumia nyota na
kibali cha mtu mwingine kwa nguvu za kichawi wakati mtu huyo akiwa anaishi
maisha magumu. Kwenye dunia hii kuna watu wanaiba vitu vya mtu mwingine na
wengine wanarudisha vitu vilivyoibiwa.
“Lakini watu hawa ni watu
walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika
magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana
asemaye, Rudisha.” Isaya 42:22
Kuna mambo yanamfanya mtu
acheleweshwe kwenda pale Mungu alipokusudia aende, ingawa wakati wake wa kufanya
kusudi lake umefika. Kuna wakati mtu anashindwa kulitimiza kusudi la Mungu kwa
sababu mashetani yanafanya kazi ya kumzuia mtu huyo asilifanye kusudi hilo kwa
wakati uliopangwa na Mungu.
“Akainuka akaingia nyumbani; naye
akayamimina yale mafuta kichwani mwake, akamwambia, BWANA, Mungu wa Israeli,
asema hivi, Nimekutia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa BWANA, yaani, juu ya
Israeli. Nawe utawapiga nyumba ya Ahabu, bwana wako, ili nijilipize kisasi
cha damu ya watumishi wangu manabii, na damu ya watumishi wote wa BWANA,
mkononi mwa Yezebeli. Kwa maana nyumba yote ya Ahabu wataangamia; nami
nitamkatilia mbali kila mwanamume wa nyumba ya Ahabu, yeye aliyefungwa, na yeye
asiyefungwa, katika Israeli.” 2 Wafalme 19:6-8
Mungu humchagua mtu yeyote amtakaye
yeye. Haangalii kama ananguvu au ni dhaifu au ni tajiri au maskini kwa maana
Mungu hamtazami mtu kwa jinsi ya mwili bali anangalia kile alichokiweka ndani
yake Mtu huyo kabla kuja hapa duniani. Ili Mungu awezekuongea na mtu hutumia
neno lake ambalo kwa kupitia neno litamtia nguvu na kumpa ujasiri wa kufanya
jambo la kiMungu kwa wakati ulio sahihi.
“Na yeye aichunguzaye mioyo aijua
nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu. Nasi
twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao
katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale
aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana
wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale
aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia
haki; na wale” Warumi 8:27-30
Kuna mambo mtu anayafanya ila
ndani yake anaona kuwa hapa sio sehemu yake ila kwa Kadiri anavyoendelea kuwa
hapo ndipo anaendelea kuchelewa Kwenda kule Mungu alipokusudia aende. Kuna watu
wametumwa na kukuchelewesha kwasababu wanajua kuwa mtu akifanya jambo hilo la
kiMumgu litafanikiwa sawasawa na kusudi la Mungu.
“Wala msiifuatishe namna ya dunia
hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya
Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” Warumi 18:9
Nguvu kubwa ya shetani ni kuzuia
watu Mungu. mfano, simba akiwa amefungwa hana uwezo wa kumdhuru mtu ndivyo
ilivyo kama mtu wa Mungu pale anapozuiliwa na shetani lengo lao kubwa ni kumchelesha
mtu huyo na kumfanya asifanye kusudi la Mungu kwa wakati sahihi ambao Mungu amepanga
kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu.
“Miji ya Negebu imefungwa malango
yake, wala hapana mtu wa kuyafungua; Yuda amechukuliwa hali ya kufungwa;
amechukuliwa kabisa hali ya kufungwa.” Yeremia 13:19
1 Comments
This article, "KUWAFUNGUA WALIOCHELEWESHWA," offers a powerful and encouraging message about spiritual warfare and overcoming delays in one's life. It emphasizes the belief that believers have the power to challenge and reclaim what has been hindered by spiritual forces.
ReplyDeleteThe explanation that delays can prevent individuals from fulfilling God's purpose at the appointed time is a significant point, and the article provides a strong call to prayer and spiritual action. The use of biblical references helps to reinforce the message of divine empowerment and courage.
For those who resonate with spiritual teachings, this article provides a compelling perspective on perseverance and reclaiming one's destiny.