UFUFUO NA UZIMA
CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI 30.11.2025
ASKOFU DKT GESHOM
MWAKILA
SOMO: KUKOMESHA MATUKIO YA
KISHETANI
Dunia imejaa matukio tofauti, na ndani ya matukio hayo yamegawanyika katika makundi mbambali. Kuna matukio ya furaha, matukio ya kupata, na matukio ya kukosa pamoja na matukio mengine mbalimbali.
Kwa kila jambo kuna majira yake,Na wakati kwa kila
kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa
kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa; Wakati wa kuua, na wakati wa
kupoza;Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga; Wakati wa kulia, na wakati
wa kucheka;Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza; Wakati wa kutupa mawe,
na wakati wa kukusanya mawe;Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;Wakati
wa kutafuta, na wakati wa kupoteza;Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa; Wakati
wa kurarua, na wakati wa kushona;Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;” Mhubiri
3:1-7
Nyakati
zimebeba matukio mbalimbali, kama vile wakati wa kupata ambao huambatana na matukio
ya kupata. Wakati wa mtu wa kupata unapofika, ni lazima matukio fulani ya
kupata yatokee ndani ya maisha ya mtu huyo. Kwenye maisha ya kila siku asili ya
mtu huwa ni katika ulimwengu wa roho. Hivyo hata wakati huwa unaanzia
kujulikana rohoni ndipo matukio fulani hutokea kwenye ulimwengu wa mwili.
“Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za
wokovu tele na hekima na maarifa; kumcha BWANA ni hazina yake ya akiba.” Isaya 33:6
Kwa
asili mtu ni roho ambaye yupo ndani ya nyumba ambayo inaitwa mwili. Watu wakitaka
kutengeneza matukio huwa wanashughulika na ulimwengu wa roho, na baada ya hapo matukio
yanaonekana kwenye ulimwengu wa mwili. Wachawi ili waweze kutengeneza matukio
juu ya mtu wanashugulika kwenye ulimwengu waroho ambao ni ufalme wa giza.
Ulimwengu
wa roho umegawanyika katika makundi mawili au falme mbili, kuna ulimwengu wa
roho wa nuru na ulimwengu wa roho wa giza. Ulimwengu wa nuru una nguvu kuliko
ulimwengu wa giza. Mtu ambaye yupo kwenye ulimengu wa roho wa nuru una uwezo wa
kuharibu ufalme wa giza. Kila matukio yanayo tengenezwa katika ufalme wa giza yanaweza
kuharibiwa na ulimwengu wa nuru. Ulimwengu wa nuru uaongozwa Mungu aliyembinguni
na ulimwengu wa roho wa giza unaongozwa na shetani.
Kuna
matukio ambayo yanaonekana kuwa ni ya kawaida ila yanakuwa yametengenezwa na
mtu. Kunakuwa na mtu ametamka maneno kwenye ulimwengu wa roho, na nyuma ya neno
hilo huwa kuna roho. Roho inasubiri neno ili kulipa uhai neno hilo. Kunakuwa na
viumbe vimesetiwa kusikiliza hilo neno ili kulitimiza katika upande wa Mungu ama
wa Shetani. Mtu akipakwa mafuta haijalishi muonekano wake, Mungu humtofautisha mtu
huyo na watu wengine.
Sio
kila matukio yanayotoka mbinguni huwa ni ya Mungu, kuna mengine yanatoka kwa Shetani.
Katika biblia inaonesha Shetani aliteketeza mali za Ayubu kwa moto kutoka
mbinguni, hii inaonesha kuna matukio ambayo yanatoka mbinguni ila Shetani ndio
aliyesababisha.
Kwenye
ulimwengu wa kiroho kuna mawakala wa aina mbili ambao ni mawakala wa mambo mema
na mawakala wa uharibifu. Mawakala wa mambo mema wanatoka kwa Mungu na mawakala
wa uharibifu huongozwa na Shetani. hivyo unatakiwa kuwafahamu mawakala wa
uharibifu kwa kufanya vita katika ulimwengu wa roho nao ni kwa kuomba.
"Kisha nikaona mnyama mwingine,
akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa
Mwana-Kondoo, akanena kama joka. Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule
wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie
mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.” Ufunuo13:11-12


0 Comments