UFUFUO NA UZIMA
CATHEDRAL
IBADA YA JUMAPILI
22.03.2026
ASKOFU
DKT.JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: VYANZO VYA MATATIZO
![]() |
Kanuni ya kutatua tatizo ni kujua chanzo chake. Kila mtu anatatizo ama matatizo fulani kwenye maisha yake, na matatizo hayo yanatofautiana ukubwa. Matatizo mengi hulenga kuleta kifo, ama kifo cha biashara, ndoa, uhai wa mtu, au uchumi wa mtu. Kifo kinaweza kuwa mahali popote, mfano kinaweza kuwa kwenye chakula, kinaweza kuwa kwenye famalia au kinaweza kuwa sehemu yoyote. Zipo familia nyingine wakiwa wamefika levo ya kufanikiwa, wanakufa. Ni kwasababu kifo kipo ndani ya familia hiyo.
“Nikaona,
na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni
Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi,
waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi.” Ufunuo 6:8
Tatizo la Kifo: Je Kifo ni Tukio?
Kifo
sio tukio. Kifo ni mtu, yaani kifo ni roho ya mauti. Kinaweza kuwa sehemu fulani
ama kwa mtu fulani. Kifo sio tu kifo cha mtu kuondoka duniani, lakini pia kuna kifo
cha kuanza jambo lakini usilifanikishe. Kifo kinaweza kutumwa kwa mtu fulani na
mchawi, na akishatuma kifo hicho, ndo linatengezwa tukio la kukupata kama vile ajali
ama ugonjwa ambao unalenga kukuletea kifo.
“Na
mmoja wao akaenda nje kondeni ili kuchuma mboga, akaona mtango-mwitu,
akayachuma matango-mwitu, hata nguo yake ikawa imejaa, akaja akayapasua-pasua
sufuriani; kwa maana hawakuyajua. 40Basi wakawapakulia hao watu ili wale.
Ikawa, walipokuwa katika kula chakula, wakapiga kelele, wakasema, Mauti imo
sufuriani, Ee mtu wa Mungu. Wala hawakuweza kula.” 2 Wafalme 4:39-40
Kuna
vitu vinavyomtokea mtu, ila nyuma yake kuna mamlaka ya rohoni inayopelekea vitu
hivyo kutokea. Wanyama huwa wanauwezo wa kuona viumbe vya rohoni. Mfano, kwenye
biblia inaonesha punda aligoma kwenda mbele kwasababu aliona malaika ameshika
upanga akawa anagoma kwenda mbele. Hata kwenye maisha yetu ya kawaida, kuna
wakati mbwa wana bweka kwa hasira na hauoni mtu ni kwasababu wao wanakuwa wameona
wachawi.
“Na
yule punda akamwona malaika wa BWANA amesimama njiani, na upanga wake mkononi
mwake amekwisha kuufuta; punda akageuka upande ili kuiacha njia, akaingia
shambani. Balaamu akampiga punda ili kumrejeza njiani.” Hesabu 22:23
Katika
kila familia ama ukoo, inamchawi wake. Yaani anakuwepo mtu katika familia ambae
anafanya uchawi juu ya wenzake. Ukimjua mchawi wa familia unaweza ukampiga na kumshimba
kwa maombi. Ipo namna ya kuweza kumpiga, kwa kuomba kutumia jina la Yesu. Mtu
anapompokea Yesu Kristo, Mungu anaweka mamlaka ya kuwapiga wachawi na
kumwapisha mchawi aweze kurudisha kile alicho chukua kutoka kwako. Mamlaka hiyo
inahusisha sauti ya mamlaka.
“Nanyi
mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya
Mwana.” Yohana14:13
Sauti
ya mamlaka:
Ukiomba
kwa sauti ya mamlaka, unauwezo wa kumwamuru mchawi yoyote bila kujali cheo
chake na akakutii. Kama mwana wa Mungu, ukitumia sauti ya mamlaka unauwezo wa
kumpiga na kumuangamiza mchawi.
“Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na
nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.” Luka 10:19
Kuna
wakati, mtu matatizo ulionayo ni kwasababu ya mashetani ambao wanakua ndani ya
mtu huyo. Mtu pia anaweza akawa anateseka na ugonjwa kwa muda mrefu bila kupata
tiba, lakini chanzo cha ugonjwa huo ni mashetani. Lakini mtu aliyempokea Yesu
unaweza kuamuru mashetani watoke ndani ya mtu huyo, na mtu huyo akapona.
Kupitia
nyota yako,wachawi wanaweza kuona miaka ijayo utakuwa nani baadae. Hivyo kazi
yao wanaiba nyota ya mtu na kuitumia kwa ajili ya kazi zao.
Kinachomfanya
mchawi aweze kukuangamiza ni dhambi inayokaa ndani yako. Yaani dhambi ndiyo
inayompa shetani ama mchawi nafasi ya kukudhuru. Lakini kuna namna ya kuweza
kumzuia mchawi na mashetani, ni kwa njia ya kumkubali na kumpokea Yesu awe Bwana
na Mwokozi wa maisha yako. Yesu atakuondolea dhambi zako zote, na mashetani
hawana mamlaka ya kukushambulia kwa maana umeondolewa dhambi zako zote. Na una
mamlaka ya kumpiga na kumuangamiza.
Unatakiwa kuomba kwa kusema hivi;
“Baba wa mbinguni nimesikia sauti yako, leo nimetambua yakuwa mimi ni mwenye dhambi ninakuomba bwana Yesu unisamehee dhambi zangu zote ufute jina langu kwenye kitabu cha mauti Uandike jina langu kwenye kitabu cha uzima wa milele. Bwana Yesu leo ninayatoa maisha yangu kwako katika jina la Yesu amen”
BONYEZA HAPA KUANGALIA IBADA YA JUMAPILI


0 Comments