Monday, December 27, 2010

FAIDA 11 ZA KUMTUMIKIA MUNGU

Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima, jumapili ya leo 26 Disemba 2010 ambayo ndiyo jumapili ya mwisho ya Mwaka amefundisha neno la Mungu juu ya faida 11 za kumtumika Mungu. Kwa ufupi kabisa tumekuandika faida hizo. Tunakushauri upate nakala yako ya CD au DVD kwa kupiga simu namba +255 716 369190 au fika Kawe-Tanganyika Packers katika Viwanja vya Nyumba ya Ufufuo na Uzima katika kontena letu linalouza vitabu na utajipatia nakala yako. USIPITWE na Baraka hizi za kumtumikia Mungu chukua nakala yako Sasa.

Faida za Kumtumikia Mungu kwa ufupi:- Kutoka 23: 25-29

1. Atabariki Chakula Chako

2. Atabariki Maji yako

3. Atakuondolea ugonjwa katikati yako

4. Hapatakuwa na Mwenye Kuharibu Mimba

5. Ataondoa Utasa

6. Hesabu za siku zako ataitimiza

7. Atatuma Utiisho wake mbele yako

8. Atawafadhaisha wote wakufikirio

9. Adui zako watakuonyesha maungo yao

10. Atapeleka mavu mbele yako; watakao mfukuza Mhivi, na Mkaanani na Mhiti wote watoke mbele yako

11. Ukimtumikia Mungu, atakuheshimu- soma Yohana 12: 26