Thursday, December 16, 2010

MIUJIZA: Maiti yafufuka kupitia maombi ndani ya simu ya mkononi

Agnes Mrema kutoka kushoto mwenye nguo ya damu ya mzee akiwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima wakati akitoa ushuhuda kanisani ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima


Na Information Ministry

Miujiza mikubwa yatokea ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima baada ya mmoja wa Wachungaji wasaidizi (MP-Ministry Pastor) kupiga majeshi (maombi) kupitia simu ya mkononi na kumfufua Mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Agnes Mrema.

Mama huyo alijitokeza jumapili hii kutoa ushuhuda wa jinsi alivyokufa na hatimaye kufufuka kutoka kwa wafu. Mama huyo aliyekuwa na watoto wake wote wakati akitoa ushuhuda huo aliulezea umati mkubwa wa watu zaidi ya 30,000 juu ya namna alivyochukuliwa kwa nguvu na kutaka kuingizwa shimoni.

Katika ushuhuda wake mama huyo aliyekuwa akihojiwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima alikuwa na haya ya kusema “nilianza kuumwa kichwa na kuwashwa mwili mzima muda wa siku 21. Siku ya ijumaa tarehe kumi mwezi Disemba mwaka 2010 nikaona wanakuja watu wenye maumbo ya ajabu na wanatisha sana wakanifunga miguu na kumpeleka kijijini ambako shimo lilikuwa limeshaandaliwa kwa ajili yangu. Baada ya hapo nikaona kuna mtu ananisukuma nisiingie shimoni, ghafla nikafufuka”

Wakati hayo yote yakiendelea katika ulimwengu wa roho, mchungaji msaidi ngaza ya MP (Ministry Pastor) alikuwa akiiombea maiti ya mama huyo ambayo aliagiza iwekewe simu masikioni naye akaanza kuporomosha maombi ya nguvu ya kurudisha. Baada ya muda mfupi maiti hiyo iliinuka kwa nguvu na na pumzi ikamrejea akawa mzima.