Sunday, January 8, 2012

Ujumbe wa Leo:Tunza moto wa Madhabahu Usizimike

Mnenaji: Mch. Adriano (RP)
8/01/2012
Utangulizi
Usipoutunza moto wa madhabahu , NI hatari kubwa kwa kuwa waweza kuzimika, na kwakuwa unaweza kuzimika ni muhimu kuutunza moto wa madhabahu.
Madhabahu NI daraja la Kutoka ulimwengu wa roho kuingia ulimwengu wa mwili au kinyume chake, Ndani ya mtu madhabahu ni moyo wa mtu aliyeokoka.

Mambo ya walawi 6: 8-13
"moto wa madhabahu utawala juu ya madhabahu daima usidhimike," hili NI agizo la Mungu kwa Musa, alimwambia moto wa madhabahu uliowashwa NA kuhani usizimike , NA kwa namna hii Yesu alikuja kuleta moto duniani ( luka 12:49)
Kumbe moto ushatupwa duniani na kazi yake ni kuharibu kazi za shetani, magonjwa, tabu shida, mikosi n.k. Na huo moto uliowashwa na Bwana Yesu hauwezi kuzimwa.

Moto ni nini?
Moto wetu sisi kama watu tiliookoka ni Roho mtakatifu ambaye anakaa ndani yetu, Samson naye alipotaka kuangamiza mashamba ya wafilisti alitumia moto, akawafunga mbweha wawili wawili na moto na kuwawepeleka kwenye mashamba ya wafilisti , kazi ya Mungu duniani imeanza kama moto, huu moto yaani ni roho mtakatifu hutuongoza, ukiubeba moto huu utaingia kila mahali. Utafanya mambo makubwa.

Umuhimu wa moto
Tunaona wanafunzi wa Yesu baada ya Yesu kupaa, walibaki kuusubiri moto ( Roho mtakatifu). Matendo ya mitume 1:12-14! Hii inatuonyesha umuhimu wa moto, maana kabla ya kupokea moto petro alimkana Yesu, lakini baada ya kupata moto alimtangaza Yesu bila uoga! Kumbe moto huu unatupa ujasiri.

Pia katika ufunuo 8:5! Tunaona vitu kadhaa katika andiko hili.
1. Kukawa radi
2. sauti
3. Umeme
4. Tetemeko la nchi.

Hapo kabla tunaona malaika akachukua chetezo akakijaza moto wa madhabahu, hili neno " moto wa madhabahu" ni Roho mtakatifu ambaye baada ya malaika kuachilia wakati wake, kukatokea radi, sauti, umeme na tetemeko la nchi. Kumbe ukimbeba roho mtakatifu( moto wa madhabahu) unaweza kusababisha mambo hayo kwenye maisha yako.

Ni muhimu kujua ulipokuja duniani, Mungu alikuandaa kama chombo chake na hapo shetani alikuona wewe, na uweza na baraka ulizopewa kwahiyo shetani anakufuatilia ili kuchukua kile ulichopewa na ikibidi akitumie yeye!

Moto huu unatupa uwezo wa kumiliki duniani, na ndiyo maana biblia inasema kila tunapokanyaga tumepewa, hii tunaona kwa wana waisrael walipokuwa wanavuka mto yordani , Mungu aliwaambia makuhani waliokuwa wamebeba sanduku la agano, wakanyage maji ili wavuke, kumbe unaweza kupita kwenye wakati mgumu, huoni njia lakini kumbe shetani amefunga uweza wa umiliki wako, lakini ukibeba moto wa Roho mtakatifu ambao umeachiliwa duniani, hapo utavuka kwenye hatma yako. Na hizi ndizo kazi za roho mtakatifu.

Isaya 66:1 hizi zote ni kazi za Roho mtakatifu. Roho mtakatifu anaweza kufufua kuponya, kufungua kuwatangazia wafungwa uhuru wao. Mambo ya walawi 10:1-2 " nao ukawala nao wakafa mbele za Bwana " Mungu aliagiza moto wa madhabahuni usichanganywe na moto wa kigeni ambao Mungu hakuwaagiza. Hawa NI watoto wa haruni. Hii inatuonyesha kuwa moto wa Bwana hauitaji kusaidiwa, unasimama wenyewe, hauwezeshwi NA moto wa kigeni! Moto ndio unaomtofautisha mkristo mmoja hadi mwingine, NA moto huo ni uweza wa Mungu .

Uthibitisho wa kiimaandiko:
Matendo 1:5, mathayo 3:15. Atawabatiza kwa roho mtakatifu na kwa moto, mathayo 3:11. Kubatizwa na roho mtakatifu maana yake ni kuingia ndani ya roho mtakatifu. Hapo kitu chochote kabla ya kuingia au kutoka ndani yako lazima kipitie kwanza kwa Roho mtakatifu , ugonjwa hautapita kwako kabla ya kupita kwa roho mtakatifu, na mashetani hawatakuwa na nafasi kwenye mwili wako.
Unatakiwa kujua kuwa shetani anaweza kujaribu kuzuia njia yako, labda masomo, kuzaa , kupita n.k. Lakini jambo lakufanya hapa si kuhuzunika bali ni kupokea moto kutoka kwa Bwana ambao NI Roho mtakatifu, ukiwa na moto hakuna wa kukuzuia kabisa. " katika mambo yote sisi NI washindi NA zaidi ya kushinda, katika yeye aliyetupenda"