Sunday, February 26, 2012

Ushuhuda wa kijana Eliya ambaye alikuwa akiishi na jini bila kujua..

Ibada ya Jumapili 26 Februari 2012

Shuhuda ya kijana Eliya ambaye alikuwa akiishi na jini bila kujua..
Eliya :-
Nilikuwa zanzibar kibiashara na nilikuwa nafanya biashara ya kuuza computer, ambazo nilikuwa nazifuata huko. Nikiwa katika mapumziko Zanzibar maeneo ya forodhani, na wa dada wawili wakaja wakaniambia tunahitaji kampani, kwakuwa nilikuwa bar. Wakniuliza una mtu, basi nikasema hapana, basi wakaja na tukaanza kunywa, baada ya muda tukiendelea kunywa. Wakaniuliza jina langu na shughuli zangu, nami nikawatajia.

Kesho yake asubuhi wakati nimetoka kutafuta riziki nyuma yangu, nikashangaa imesimama gari, na nikawaona wadada wale wale ambao niliwaona jana yake. Basi waliniomba niende nao nikawambia naenda kazini, wakanisihi ninywe nao supu. Basi baada ya hapo siku ile ikapita tena.

Siku moja nikiwa mwenge, gari aina ya vx lilipaki karibu nami ( namna alitaja ila tunaziifadhi) . Na pale akatoka yule yule binti aliyemuona Zanzibar na safari hii alikuwa mmoja. Nikamwambia naenda ofisini. Akaniambia tuingie kwenye gari na nikapanda. Na Yule binti akanipeleka hotelini, basi yule binti akaniambia Nina kitu cha kunieleza nikamshawishi aniambie. Basi akaniambia kuwa anaomba tuwe marafiki , basi nikamkubalia na nikaanza kumchukulia kama dada yangu. Basi tukaondoka na kuendelea kuwasiliana. basi baada ya siku chache nilienda zanzibar na Yule dada alinisaidia kutafuta mzigo na badala ya kukaa siku tano akakaa siku tatu........

.......ameruka baadhi ya matukio kwaajili ya muda kuwa mdogo.....

Nilikuwa msaada kwake kwa kipindi cha mwanzo, lakini baada ya muda, Mimi ndio nikaonekana ndiye ninaye hitaji msaada, kwa kuwa alikuwa na hela ambazo awali hakujidhihirisha.. Mwanzoni alikuwa Kama mtu asiye na hela.. Akawa ananipa hela siku baada ya siku. Basi nikafanikiwa kujenga nyumba mbili mlandizi, na baada ya hapo nilishangaa alikuwa anaendelea kunipa pesa, mwanzoni alinipa laki 7 lakini ilifikia kipindi ananipa hadi sh. Milioni 40.. Na bila kujua anatoa wapi kwakuwa hakuniambia anafanya kazi gani. Na hapo huyo msichana akanipa gari, alinipa vitu vingi. Na baada ya muda mazoea yakazidi basi nikamshirikisha kuwa kama inawezekana tuwe pamoja kama mtu na mchumba wake. Alikubali na kwa wakati huo nilikuwa sijui anapoishi na hapo nikamuuliza akaniambia baba na mama yake wako Nugwi Zanzibar. Basi tukakubaliana tuanze kwa kwenda kwa wazazi wangu ambao wapo singida,

Tukapanaga safari , tukiwa safarini kuelekea singida, Dodoma. Akapotea ndani ya gari tulilokuwa tumepanda. Maana yeye alikuwa amekaa siti ya dirishani hapo , nikawauliza abilia wengine nao walikuwa hawajui, . Na mara wakati tunajadili yule binti aliyekuwa akiitwa Hawa, akarudi . basi kukawa kimnya kila mtu alikuwa anaogopa. tuliposhuka kwa mapunziko mzee mmoja amabaye alikuwa abiria akaniambia nishuke.. Maana nitawaletea matatizo. Nikashuka naye baada ya kunisisitiza abiria kunisisitiza.

Tukiwa dodoma, nikatamani nimuone mguu wake, maana niliambiwa awali kuwa jini anakuwa na kwato. Kwa kuwa kwa wakati huo nilikuwa sijawahi kuona miguu yake, tokachukua chumba pale Kilimanjaro hotel Dodoma, akatoka kidogo, lakini nilimvizia akirudi nione miguu yake, cha ajabubbaada ya kurudi Yule binti akakataa kupumzika na alikataa kuvua viatu pia. Basi kwakuwa alikuwa na nguvu kunizidi basi nikapanga kumkimbia, kwa kuwa nilianza kuingiwa na hofu, nikamwambia kwa kumdanganya kuwa naenda kununua vocha. Lakini nilipotaka kukimbia kufika getini nikakutana naye anatokea ninakoelekea. Basi ikabidi nirudi ili nimuangalie miguu asubuhi wakati wa kuamka, Asubuhi nilipoamka yeye akaniwekea mkono kichwani hapo nikalala hadi akaoga akamaliza. Nakuja kuamka baada ya masaa bila kujua usingizi niliupatia wapi..

Basi kesho yake tukapanda gari lingine la kuelekea singida. Tukiwa njiani, manyoni polini, ghafla akaanza kupiga kelele akisema sitaki kwenda kwenu siwezi kwenda, na sitaki kwenda.. Basi gari likasimama manyoni singida na kwa kuwa sikuwa na jinsi ikabidi nishuke na tulipofika tu akatoweka tena. hapo nikasema sina jinsi zaidi ya kukimbia nikakimbia umbali kama wa kutoka Kawe hadi ubungo kufika tu nataka nipumzike nikamuona kutokea mbele, na akawa ananihoji unaenda wapi.. Nikamuomba msamaha nikataka kwenda polisi nikakutana naye anatoka polisi. Nikawa sina jinsi zaidi ya kumtii tu. basi tukarudi dodoma, na hapo akainua mikono yake ikamwagika kitu Kama maji, akanimwagia mguu akiniambia tutaona nani baba Kati yako na Mimi. Baada ya hapo .. Yeye aka toweka

Nikiwa Dodoma nikaamua kutafuta kanisa.. Kwakuwa alikuwa amechukua hela zote, Na nikapata kanisa nikamwelezea Mch. Na akaniombea na akaniambia nipumzike na ghafla yule binti akatokea hofisini nilipomuelezea Mch. , mchungaji akakimbia kutoka ofisi na Mimi nikakimbia kumfuata mchungaji basi Yule Mch. Akaniambia kamtafute pastor Max. Wa ufufuo na uzima ndiye atanisaidia kwa kudai Mimi nitamletea matatizo.

Basi walinipa nauli kidogo na nikaja dar. nilipofika dar. Nikaenda kwenye nyumba yangu mikocheni nikaenda lakini sikuikuta tena eneo amabalo ilikuwepo awali. Na nikaamua kuja kumtafuta Mch. Max. Basi nikaja kanisani na nikaombewa japo nilikuwa sina imani kabisa ndani.

Basi jioni yake nikatoka naelekea kutafuta chochote hapo kufika getini akanigusa na akanilazimisha turudi nyumbani.. Cha ajabu tulipokuwa na yeye ile nyumba nikaikuta Basi akaniambia anataka kwenda kwao Nugwi Zanzibar. Basi alipoondoka. Mimi nikaamua kuja kanisani kuonana na pastor max. Basi nikaamua kuondoka na nguo chache nikaja kanisani. Na hapo akaniombea na baada ya kuniombea akaniambia kuwa twende tukaione hiyo nyumba. Na tulipofika hatukukuta nyumba tena ambapo ndio palepale aliponipeleka awali na ndipo nilipokuwa asubuhi lakini si kuona nyumba tena. Tukakuta uwanja uko wazi.. Basi ndio nikaamua kumpokea Yesu. Amen

No comments:

Post a Comment