Sunday, March 11, 2012

SOMO: Viti vya Enzi

Jumapili, Machi 11, 2012.

Na. Mch. Kingozi : Josephat Gwajima

Enzi ni utawala ambao mtu anakuwa nao.. mfano Mfalme akishika madaraka anaitwa mfalme ameingia kwenye enzi yake, pia Rais naye ni hivyo hivyo.. kwenye somo hili tutaangalia kwa undani zaidi kuhusu viti vya Enzi..

Kiti cha enzi cha Mungu….

Ufunuo 2:13 .. “….kiti cha enzi cha shetani…hapo akaapo shetani.” Maneno haya yaliandikwa katika karne ya kwanza , kipindi hiki wanafunzi wa Yesu walitawanyika kwa kuwa walikuwa wanauawa na Yohana alikuwa katika kisiwa cha patmo.. hapo Yesu alimtokea na kuumpa ufunuo juu ya makanisa mbalimbali.. ndipo kwenye kanisa mojawapo Yesu akamwambia hayo maneno kwa “ najua ukaapo ndipo kwenye kiti cha enzi cha shetani..”

Maana ya neno kiti cha enzi cha shetani..

Kiti cha enzi ni makao makuu ya utawala au utendaji kazi wa utawala ( center of operation) , tunaweza kuona pia katika ufunuo 16:10 “ kiti cha enzi cha mnyama” lakini ukirudi nyuma ufunuo 13:2 huyu mnyama alipewa uwezo na Yule joka.. “kutoka kwenye kiti cha enzi cha Yule joka” huyu joka kimsingi ni shetani yuleyule. Aliyetajwa kwenye ufunuo 12:7.. kumbe tunagundua kuwa shetani ana kiti cha enzi na hivi vinamaanisha makao makuu ya utendaji kazi wake..

Anaposema kiti cha enzi cha shetani hapa (mwanzo 2:12) ana maanisha ni mji kabisa ambao shetani kaamua kuufanya kuwa makao yake makuu ya utendaji kazi wake.. kumbe shetani anaweza kuweka kiti cha enzi ndania ya mji.. na mji ukakamatwa kwa kiti kile cha enzi..

Shetani anaweza kuweka kiti cha enzi ndani ya mtu.. kumbe shetani anaweza jenga mamlaka yake ndani ya mtu.. huyu anakuwa anatoa msaada wa kishetani. Ili wle wanaotaka kupata msaada wa kishetani wanamfuata na wanakutana na shetani moja kwa moja.. hii inatokea pale shetani anapo amua kuishi na kufanya utawala ndani ya mtu.. na ndio maana mapepo ukitaka kuyatoa yatajibu kwa kusema “mwacheni kiti wangu” hii ikionyesha kuwa Yule pepo amejenga utawala wake au kiti cha enzi ndani ya huyo mtu..

Uthibitisho wa viti vya enzi kwenye biblia..

Matendo ya mitume 16:16-34 tunamuona huyu kijakazi, ambaye shetani ameweka makao yake ndani yake, na kwa kiti hicho alikuwa anatenda kazi zake kwa watu.. ndio maana biblia inasema “aliwapatia faida nyingi sana bwana zake”.. unaweza kujiuliza kidogo kwanini watu wa mji wote waliwageukia wakina Paulo , na wakawaweka katika gereza maalum jiulize shida hapa ilikuwa kutoa pepo kwa huyu binti , kwanini wafanya biashara waliingilia? Utagundua kuwa shetani alikuwa ameweka kiti chake cha enzi ndani ya Yule binti, ambapo wafanya biashara walikuwa wanamfuata kwa ajili ya kuwaagua.. mfano kujua mambo yajayo..

Ni muhimu kujua , haijalishi una umri gani kumfanya shetani aweke kiti chake cha enzi.. na unaweza usijijue kuwa wewe ni kiti cha enzi maana huyu kijakazi alihisi ni sehemu yake ya maisha kumbe , ni shetani anatenda kazi ndani yake.. ni muhimu kupindua kiti cha enzi ndani ya watu kwa Jina la Yesu Kristo..

Kila mji unaouona una kiti cha enzi cha shetani.. na ndio maana ukiangalia miji mbalimbali hata hapa Tanzania kuna viti vyake vya enzi.. hawa ni watu wanaosimamia utawala wa kishetani.. na hawa ndio wanaojenga tawala za kishetani. Ukiangalia nchi nyingi za duniani utajiri unashuka kuzimu kwa shetani kupitia viti hivi vya enzi.. na nchi yaweza kushuka kiuchumi kwasababu ya viti hivi vya enzi..

Kwenye Marko 5: 1- luka 8:26 hapo tunaona habari nyingine ya kushangaza kidogo, kulikuwa na mji wa wagerasi huu mji ulikuwa wa kibiashara tunalijua hili pale tunapoona nguruwe na kwa wakati ule wayaudi walikuwa hawafugi nguruwe , hii inaonyesha mji huu ulikuwa ni wakibiashara.. na katika njia kuu ya kuelekea katika mji ule kulikuwa na watu wwili wenye pepo mathayo 8:28-… “…..wasiruhusu mtu apite…” utaona hiki ni kiti cha enzi kinachozuia biashara na ndio maana Yesu alipotaka kumtoa walimwambia wasimtoe kutoka kwenye ule mji.. kwasababu walikuwa kiti cha enzi cha mji wa wagerasi.. na hawa walikuwa wanakaa kuchuja wanaoruhusiwa kwenda ndani ya mji huo..

Hata ukoo waweza kuwa na kiti cha enzi cha shetani, kinacho simamia makusudi ya kishetani kufanyika ndani ta ukoo.. na ndio maana unaweza kuona kila ukoo una aina ya magonjwa na aina ya vifo..hiki kiti cha enzi kinawekwa na shetani ndani ya ukoo au familia ili kuutawala ukoo.. na ndio maana hata wale mashetani walimwomba Yesu asiwatoe kutoka kwenye ule mji..

Ili kuhama kutoka kwenye viti hivyo vya enzi, unatakiwa kuomba maombi ya kupindua viti vya enzi vya kishetani kwenye maisha yako.. kwamaana mtu anaweza akazaliwa chini ya kile kiti cha enzi na ikakufanya uwe na matatizo tangu tumboni.. na ndio maana baadhi ya familia zimewekwa chini ya laana na matatizo kwa sababu ya viti hivi vya enzi, yaani bibi aliachwa na babu, naye baba akamwacha mama na sasa wewe umekutana na matatizo ya kuachwaa ni muhimu kujua.. jaribu kuangalia nafasi ya maisha yako na familia yako... na ndio maana Mungu kakuchagua wewe kama kuhani wa familia ili upindue viti hivyo vya enzi.. ni muhimu kujua nafasi yako.. kataa kuishi chini ya kiti kile cha enzi..