Sunday, February 24, 2013

USHUHUDA WA MAMA AMBAYE BINTI YAKE ANA DALILI ZOTE ZA MTOTO WA DAWA


Mama huyu alikiri kuwa mtoto wake ana dalili zote ambazo Shehe Omary alizitaja. "Dalili 10 za mtoto wa dawa kama zilivyo zipo kwa mtoto wangu" alisema mama huyo.

Mama huyo alishauriwa kumleta mwanaye kanisani Ufufuo na Uzima kwaajili ya maombi zaidi.

SHEHE OMARI AKIELEZEA JINSI ALIVYOKUA AKITENGENEZA WATOTO WA DAWA NA DALILI ZAKE.

Kwasababu ya mila nyingi za kiafrika, watu wengi sana wamejikuta wakikimbilia kwa waganga pale wanapogundua kukosa mtoto. Wakati ninasomea falaki nilijifunza namna 11 jinsi ya kumpatia mwanamke mtoto hata kama hana uwezo wa kuzaa. Wakati nikiwa mkuu wa chuo cha kichawi pale Temeke, tulikuwa tukifundisha watu kwa habari ya mimba za kijini.

Kwa wakati mteja alipokuwa ananijia kwaajili ya kuaguliwa, jini ambalo lilikuwa ndani yangu lilikuwa linapanda ndani yangu na kwenda na kumwendea mteja alafu husoma taarifa ya mteja. Baada ya muda hutoka kwa mteja na kurudi kuja kuniambia mimi tatizo la mgonjwa huyo. Baada ya hapo nilikuwa namtajia mteja tatizo lake na kumfanya aniamini kuwa nitatatua tatizo lake hapo kila nitachomwambia lazima atafanya.

Baada yakuupata (win) moyo wa mteja, nilikuwa namwagiza vitu mbalimbali vya kufanya na kuniletea kwaajili ya uaguzi. Baada ya siku kadhaa lazima mteja huyo (ambao wengi wao walikuwa wanawake) atarudi kwaajili ya uaguzi. Katika namna hii ya kwanza ya kutengeneza mtoto wa dawa; tulikuwa tunaingiza jini ndani mwanamke na jinni yule alikuwa na uwezo wa kwenda kuiba mtoto katika nyumba ya mtu wa karibu na kumwingiza katika tumbo la mwanamke yule. Matokeo ya aina hii ya mtoto wa dawa ni uwezekano wa wazazi wakitanzania kujikuta wamezaa mzungu au mtoto mwenye sura ya jirani yake.

Madhara ya aina hii, husababisha ile mimba ambayo imeibiwa kwa mtu wajirani kupotea. Na ndio maana unaweza kumwona mtu alikuwa mjauzito lakini baada ya muda mimba ile ikapotea. Na ikitokea yule jini ameshindwa kumpatia mtoto kutoka katika maeneo yale, huamua kujitengenezea nyama kutoka katika mwili wa mwanamke. Matokeo ya aina hii mwanamke anasumbuliwa sana na mimba; unaweza kuta ni muda mfupi tu wa ujauzito lakini mwanamke huyo anakuwa ameshasumbuliwa sana na magonjwa mbalimbali.

Hivyo mtoto kama huyo akizaliwa anakuwa mwili ni binadamu lakini katika roho ni jini asilimia mia moja.

Dalili za kumtambua mtoto wa dawa wa aina hii:-
1. Macho yake hayachezi mfano akigeuka huwa anageuka na shingo yote
2. shingo yake huwa inageuka polepole haigeuki kwa haraka.
3. Macho yake huwa yanameza picha/ ukiangalia kwenye kiini cha jicho lake hakionyeshi picha.
4. Safari zake za muhimu (anazozisisitizia) huelekea upande ambao haangaliani na jua,kama ni asubuhi basi ataelekea upande wa Magharibi
5. Ana sifa nyingi zilizojificha/ anaweza kuwa na elimu ya juu lakini haionekani,au hapendi kusema
6. Huwa anafanya jambo zuri lakini hazingatii wakati:- mfano inawezekana wamekuja wageni nyumbani alafu yeye ndio akaanza kufagia muda ule.
7. Yeye ni mtendaji mzuri sana lakini hapendi kukubaliana. Yaani kama ni mtoto unaweza ukamwachia kazi afanye yeye akakataa kwa muda ule lakini jioni ukija utamkuta amefanya vyote.
8. Kwenye mikusanyiko mingi hupenda kuwa wa mwisho kutoka.
9. Ukimwangalia kwenye kipaji cha uso; kama una nguvu za Mungu utamwona kama nyama yake inatetemeka/ inatikisika
10. Huwa hafi. Kwasababu huyu ni jini hivyo hutumika katika mwili kwa muda fulani lakini baada ya muda hupotea tu bila kuonekana.

Hizo ni dalili za mtoto wa dawa anayetengenezwa kwa namna hii:
Swali: kuna madhara gani kwa wanafamilia?
Wanafamilia wanaoishi naye watapata madhara, kwasababu jini/mtoto huyu anaweza kuwa maskani ya majini na mapepo wachafu katika familia. Nakumbuka alikuwepo mama mmoja Tanga tuli tulimtengenezea mtoto wa namna hii. Baada ya muda mama yule aliokoka lakini yule mtoto hakuwahi kulipuka mapepo na mara nyingi inaghalimu msaada wa Roho mtakatifu kumsaidia mtu wa namna hii.

Swali; Jini hili laweza kukua na kuwa  kiongozi au kuoa?
Kiukweli linaweza kabisa kuwa kiongozi, mbunge, waziri au hata rais. Pia linaweza kuoa pia na kuzaa watoto pia; mfano mwanaume wa kijini akioa mke wa kawaida watoto wake watakuwa na ujini sana. Lakini kama mwanamke ni jini na mwanaume ni binadamu watazaa watoto wanaowasumbua sumbua sana.
USHUHUDA WA MAMA AMBAYE BINTI YAKE ANA DALILI ZOTE ZA MTOTO WA DAWAMchungaji Kiongozi Josephat Gwajima; akimwongoza sala ya toba binti wa kiislamu ambaye karibu ndugu zake wote waliingizwa chini ya utawala wa shetani kwa njia ya kuogeshwa maji ya bahari.
ili kuokoa maisha yake Mchungaji akamuongoza sala ya Toba ili aingie katika utawala wa Yesu Kristo!!!

Sunday, February 17, 2013

MATUKIO YA JUMAPILI YA TAR. 17 Feb 2013 KATIKA PICHA

Tarehe 17.02.2013; Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima alifundisha kuhusu Zindiko la nchi (Laana ya Nchi), katika ibada hiyo kulikuwepo pia na aliyekuwa shehe wa kiislamu, aitwaye Omari Mnyeshani. Shehe Omari ambaye alikuwa mmoja wa watu waliozindika nchi alitoa ushuhuda jinsi walivyozindika na mambo waliyofanya katika kuizindika nchi ya Tanzania.

Hapa tunakuletea matukio katika picha ya ibada hiyo.
Watoto wa Showers wakimwimbia BWANA katika ibada ya leo

Platform Choir wakimsifu Mungu, mapema asubuhi ibadani leo

Baba Mchungaji Josephat Gwajima akiwasili ibadani

Platform Choir wakimsifu Mungu ibadi, Mungu hushuka kupitia sifa


Madhabahuni kabla ya Mchungaji kiongozi kuanza kufundisha

Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akifundisha madhabahuni

Sheik Omari akitoa ushuhuda wake alipokuwa akifanya uchawi

Baba Mchungaji akipita katikati ya watu kuwaombea waliokuwa hawewezi na wagonjwa

Mama akieleza juu ya mwanaye mwenye matatizo ambaye alizunguka maeneo mengi bila mafanikio yoyote

Mchungaji Kiongozi akimfungua, aliyekuwa amefungwa na mapepo na nguvu za giza

Mchungaji Kiongozi akipita katikati ya watu na kuwafungua wote waliokuwa hawawezi na waliokuwa katika tabu na mateso mbalimbali.

wakati huo alikuwa akiruhusu maswali kwa mtu mmoja mmoja, na kupitia maswali hayo wengi walifunguliwa.


Mtoto ambaye alikuwa anatokewa na bibi yake usiku na kumpeleka kula nyama na damu za watu, akifunguliwa katika ibada ya jumapili hii

dada ambaye katika familia ya watoto tisa yeye pekee ndiye alikuwa hajafanikiwa na shetani alikuwa amemfunga
alifunguliwa baada ya maombezi

Msichana ana aliyezaliwa huku akiwa analilia jina la bibi yake, walipompa jina akaacha kulia
jambo ambalo limemletea vifungo vingi katika maisha yake.
alifunguliwa baada ya maombezi

Maelfu wa watu waliojitokeza kumpokea Yesu kwa mara ya kwanza kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yao

Moto ulishuka wakati  baba akiwa anawaombea waliokuja kumpokea Yesu

Baba Mchungaji akiwaombea watu waliojitokeza kumpokea Yesu Kristo

Friday, February 8, 2013

UJUMBE: KUPAONDOA HAPO AKAAPO SHETANI


Na Mch. Frank Andrew (RP)                                                   8th Feb. 2013Ufunuo 2:13-14 “napajua  ukaapo…. Hapo akaapo shetani” Yesu anaongea na kanisa kuwambia kuwa hapo ukaapo ndipo akaapo shetani; anaendelea kwa kusema “nawe walishika sana jina langu,wala hukuikana imani” kuna watu wanaishi wanamjua Mungu lakini bado mahali wakaapo ndipo penye makao ya shetani. Baada ya somo hili utaweza kujua na kuangamiza na kupaondoa kila mahali pa maisha yako ambapo shetani anakaa.

Dalili za akaapo shetani (Ufunuo 2:13-15):
1. Kuna mafundisho ya Balaamu.
2. Kuna mafundisho ya ukwazo.
3. Mafundisho ya kulaani watu wa BWANA.
4. Vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.

Dalili ya nne inataja sanamu, utajiuliza kwanini Mungu anakataza sana kwa habari ya sanamu mara kwa mara katika Biblia?. Jibu ni kwamba nyuma ya kila sanamu kuna roho, tunaweza kujifunza kitu kupitia Danieli 3:13-23 hii ni habari ya Shedraka, Meshaki na Abednego, Mfalme alisimamisha sanamu ili watu wote waibudu. Lakini watu hao wa Mungu watatu hawakukubali kuitumikia wala kuibudu sanamu kwasababu walijua kuwa nyuma ya ile sanamu kuna roho ambayo si Mungu JEHOVA yaani (miungu inayotumikiwa). kumbe shetani alikuwa amekaa nyuma ya ile sanamu na ndiye aliyekuwa anataka kuabudiwa.

Kama mtu uliyeokoka ni muhimu ukapajua mahali ambapo shetani anakaa katika maisha yako. Ili shetani akae mahali ni lazima kuwe na kiti chake cha enzi, ama wewe mwenyewe umepaweka kwa kupenda au watu wengine wamekuwea. Na shetani amekuja na kutawala maisha na kazi yake ni kuchinja, kuharibu na kuiba (Yohana 10:10) na ndio maana pepo wachafu wengi huwa wanasema “kiti wangu kiti wangu” ni kwasababu shetani katika ulimwengu wa roho amekaa katika maisha ya mtu huyo.

Kiti cha kwanza cha shetani ni dhambi (hii ni kumtengenezea kiti shetani mwenyewe), kuna tabia ndani ya mtu ambazo zinaweka kiti cha enzi cha shetani kwenye maisha yako. Tabia ya kiburi, mfano wa Naamani kiti chake cha enzi kilikuwa kwenye kiburi (2Wafalme 5:1-12) kiburi kilitaka kumkosesha muujiza wake. Alipokuwa na ukoma akamwendea nabii Elisha, naye akamwambia akajichovye kwenye mto wa Yordani uliokuwa na matope, lakini mwanzoni Naamani akajibu kwa dharau kuwa ameacha “mito bora kuliko yote ya Israeli kule alikotoka”. Hiko ndicho kinaitwa kiburi kwa kiti hicho shetani ameendelea kukaa katika maisha ya watu wengi, ni muhimu kujua kuwa Mungu hutenda kazi kupitia mambo madogo na hata Musa alikutana na Mungu katika kichaka, hivyo kuna viti vingine vinaondoka kwa kuamua kujishusha na kusikiliza kile watumishi wa Mungu wanachokwambia aua neno la Mungu linachokwambia.

Kimsingi, kuuleta utakatifu ni kumchafulia shetani mji; Paulo alipomtoa pepo wa utambuzi ndani ya kijakazi, wakamwita “anayechafua mji”. Kuna dhambi inatendwa ndani ya mtu na dhambi inayotendwa nje ya mtu. Watu wengi hutubu dhambi za nje kwa urahisi bali wengi husahau kutubu dhambi za ndani (moyoni) ambazo ni mbaya kama vile kutokusamehe, uchungu na wivu. Hizi ni hatari kwasababu hazijawahi kutubiwa. Dhambi za namna hii zinaleta madoa madoa katika vazi la utakatifu na wakati huohuo, Biblia inasema hakuna chenye madoa wala mawaa kitakachoingia mbinguni. Ili kujisafisha ni muhimu kutubu dhambi hizi na kunena kwa lugha muda wa kutosha ili kumruhusu Roho mtakatifu aombe ndani yako.

Pia, kiti cha enzi kingine cha kujiwekea ni pale unapoamua kwenda kwa mganga wa kienyeji ili kupokea makombe, kupigwa chale au kutoa kafala. Mizimu na waganga huweka viti vya enzi kwenya maisha ya watu. Pia, katika sherehe za arobaini za misiba kunakuwa na ibada kamili kabisa ambazo zinaweza mpa shetani kiti cha enzi katika maisha yako. Kwa namna hii shetani anapata nafasi kabisa katika maisha ya watu wengi bila ya wao kujua yaani unampa shetani mamlaka kamili juu ya maisha yako.

Vipo viti vya Enzi vya kuwekewa; ama na wachawi au waganga. Hawa ni pepo wachafu wanaotumwa kwenye maisha yako ili watende kazi ya kufunga maisha yako na kuweka mateso aidha ndani yako au kwenye familia. Unakuta mtu anamatatizo ya ndoa, matatizo ya shule, woga, wizi au tabu mbalimbali kwasababu ya kiti cha enzi cha shetani kilichowekwa kwenye maisha yake.

Viti vya enzi vingine ni vya familia au ukoo, havi husimamia tabia zinazofanana. Pia mara nyingi ukoo ulio chini ya kiti cha enzi hicho, watu wake huwa wanakufa vifo vinavyofanana na matatizo yanayofanana. Katika ukoo wa namna hii unakuta wanaukoo wote ni maskini, hawaoi, hawaolewi, au wakiolewa waume wao wanakufa; hii yote ni kazi ya kiti cha enzi cha shetani katika ukoo. Ndio maana ni muhimu kuwa makini na sherehe za koo na kimila. Ili kukomboka ni lazima umuondoe aliyekaa kwenye kiti cha enzi hiko kwa kutumia Jina La Yesu.

Bomoa pale akaapo shetani katika jina la Yesu, viti vya enzi vyote kama hirizi, na dawa za kiganga sambaratisha katika Jina la Yesu kristo. Tumepewa mamlaka ya kuwashinda waganga, wachawi na wote wanaofunga maisha yetu. Mungu akuweke huru katika Jina la Yesu.

-Frank Andrew-
Resident Pastor

Monday, February 4, 2013

UJUMBE: MAOMBI YANAYOZAA MATUNDA


MCHUNGAJI: FRANK ANDREW (RP)                                                      Jumatatu 4th Feb, 2013

UTANGULIZI:
Mungu anatuhitaji tuombe, tunatakiwa tuombe sio tu kwasababu tunauhitaji bali kwasababu Mungu anahitaji tuombe. Tatizo la watu wengi wanashindwa kupokea majibu ya maombi wanayoomba na wengine wameshindwa hata kuomba.wengine wamejikuta wakikata tama bila kujua kuwa wao ndio wanakosea katika kupeleka haja zao kwa Mungu na katika kupokea. Hapa tutajifunza sababu na jinsi ya kuomba ili kupokea kutoka kwa BWANA.

SABABU NNE: KWANINI TUNAMUOMBA MUNGU:
1. Kujinyenyekesha mbele za Mungu.
2. Kuonyesha kuwa yeye ni Mungu wetu.
3. kuonyesha kuwa vyote viko mikononi mwake
4. Tunampa heshima kama baba mwenye familia ya watoto watakatifu.

MAOMBI YANAHUSISHA VITU VIKUBWA VITATU:
1. Mhusika AU muombaji mwenyewe:- huyu ndiye muombaji na mwanzilishi wa maombi.
2. Maombi yenyewe:- haya ni mahitaji au ujumbe ambao unapelekwa kwa unaye muomba.
3. Unayemuomba:- unayemuomba ni nani kwako na mna uhusiano gani naye.

Kwa kujua umuhimu wa kuomba, wanafunzi wa Yesu walimwomba Yesu; awafundishe jinsi kuomba na hapo Yesu aliwapa fomula ya kuitumia ili kuomba. Hii ndiyo inayoitwa sala ya BWANA, kimsingi hii ni kanuni ya kuomba aliyoifundisha Yesu na si maombi yenyewe kama wengi wanavyodhani, KANUNI hii ni sawa na kanuni yengine za kufanya jambo fulani. Mfano kuna kanuni za kupika au kanuni za kuimba.  Tatizo la watu wengi ni kwamba wanatumia hii kanuni kama ndio maombi yenyewe. Kwa mfano Yesu aliposema “Baba yetu uliye mbinguni…” alimaanisha kuwa unapokuwa unaanza kuomba ni lazima ujue unamuomba baba aliye mbinguni na si magomeni. Hii ni kanuni jinsi ya kuomba na haitaji moja kwa moja haja yako, bali ukiitumia kama kanuni inakuletea majibu:=

Yakobo 5: 15-16 “kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii”, Biblia inaposema kuomba kwake mwenye haki: anamaanisha kuwa yeye anayeanzisha maombi ni lazima awe ni mwenye haki yaani msafi. Kiukweli kuna wakati mwingine Mungu hutenda kwasababu ya neema yake lakini kimsingi ili maombi yako yafae inabidi uwe mwenye haki. Hivyo kabla ya kuingia kwenye maombi unatakiwa ujitakase kwanza ili Mungu akikutazama aone uko safi. Ni muhimu kutengeneza uhusiano mzuri na Mungu, tengeneza haki kwanza kabla ya kuingia kwenye maombi. Yaani kama hujaokoka uokoke kwanza, na kama umeokoka lakini hauko sawa na Mungu, unatakiwa utengeneze maisha yako kwanza. Katika mstari wa 15* Biblia inasema “ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi” ikiimaanisha kuwa kabla ya kuingia kwenye maombi unatakiwa ujisafishe na ujitakase kwanza.

Baada ya kujitakasa kinachofuata ni kupeleka ujumbe wenyewe kwa Mungu. Watu wengi kwasababu hukosea kuomba wamedhania kuwa Mungu huwa hajibu maombi; lakini Biblia inasema Mungu anajibu maombi. Biblia inasema, Zaburi 2:8 “uniombe nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako...” na katika Mathayo 7:7 “Ombeni nayi mtapewa…” kumbe unapoomba lazima Mungu akujibu kama ukiomba sawasawa na mapenzi yake. Ni muhimu kabla ya kupeleka hoja yako uamini kwanza kuwa Mungu yupo sawasawa na Waebrania 11:6 “...lazima aamini kuwa Mungu yupo”.  Haya maandiko tutatumia katika kuangalia jinsi ya kuomba na wapi watu wengi wanapokosea wakiwa katika kuomba…

KANUNI ZA KUPOKEA KUTOKA KWA MUNGU:
Watu wengi wanajua kuomba lakini kati yao wengi hawajajua namna ya kupokea. Kwasababu kuna namna ya kuomba na namna ya kupokea. Watu wengine wanajua kuomba lakini hawajui jinsi ya kupokea haja zao. Haifaidii kitu kujua kuomba na huku ukiwa hujui jinsi ya kupokea. Kuna mambo kadhaa ambayo unatakiwa uyatilie maanani unapokuwa unaomba kama ifuatavyo:-

1. Tengeneza uhusiano wako na Mungu:-
Maandiko yanasema “haja zenu na zijulikane mbele za Mungu” pamoja na kuwa Mungu anajua haja zetu lakini bado anahitaji sisi tumuombe. Hii ni sawa na kuomba kwa jirani wakati baba yako mzazi yupo; utajisikiaje mtoto wako anapokuwa na shida alafu akuombi wewe baba yake, alafu yeye anajitengenezea sanamu na kuiomba. Utakavyojisikia ni sawa kabisa na Mungu anavyojisikia kwetu ndio maana Mungu anasema kuwa anaona wivu (kutoka 20:4). Mungu anataka tumuombe yeye ili kujenga uhusiano na yeye. Ukiomba au kuiabudu sanamu unamfanya Mungu awe na wivu.

2. Unaongea nini ukiwa katika maombi yako:-
Maombi unayoongea kwenye maombi ni ya muhimu sana kwenye kupokea haja zako kutoka kwa BWANA. Ttuangalie kwa habari ya Hana; 1Samweli 1: 1 - 24; Elikana alikuwa na wake wawili Penina na Hana, kama lilivyojina lake Hana hakuwa na watoto kwasababu tumbo lake lilikuwa limefungwa. Hana hapo kwanza alikuwa anaenda na malalamiko na kulia. Watu wengi hupeleka malalamiko kwa BWANA, badala ya kupeleka hoja kwa Mungu. Hata siku moja Mungu atendi jambo bila kusudi, na ndio maana tumbo la Hana lilikuwa limefungwa kwa muda wote ule. Emu tuangalie mambo kadhaa yaliyokuwa yakimzuia Hana.

>Sababu ya kuomba:-
1Samweli 1:1-24 Hana alikuwa anamuomba Mungu ampe mtoto ili amkumeshe penina, na ndio sababu inayowafanya wengi washindwe kupokea kwa BWANA kwasababu hawana sababu ya Kibiblia inayowafanya Mungu awape mahitaji yao. Mfano mtu anamwomba Mungu mke ili amfulie nguo au amechoka kuishi mwenyewe. Hiyo si sababu; Mungu anahitaji hoja yenye nguvu ili upokee mwambie jukumu lako la kutimiza kwenye maisha yako na nafasi ya mke katika kumtumikia Mungu; hapo lazima akutendee.

>Peleka haja ya moyo wako:-
Mungu haitaji hali yako ikoje sasa bali anahitaji kujua unataka nini. Picha ya tatizo lako unatakiwa uwe nayo wewe lakini mbele za Mungu unatakiwa upeleka haja ya moyo wako na si malalamiko. Kwa wakati ule Hana alikuwa anapeleka hali yake ilivyo na penina na si uhitaji wake kwa BWANA. Unakuta mtu anamuomba Mungu gari ili awaonyeshe wengine, huyo hawezi pata kwasababu si sawa na mapenzi ya Mungu.

>Mwangalie Mungu na si jambo unalohitaji:
Ibarahimu alipompokea Isaka ilimradhimu Mungu kumjaribu ili ajue upendo wake upo kwa Isaka au kwa Mungu. Watu wengi wanamuomba Mungu jambo lakini wakilipokea ndilo linalofanyika mzigo mkubwa wa kutokumtumikia Mungu, mfano mtu anaomba mume akipokea tu; baada ya siku chache haji kanisani anasema eti anamuhudumia mumewe. Kwasababu hii hata Hana akupata mtoto mpaka alipobadilisha maombi na kumuomba Mungu mtoto, kwa kumuahidi BWANA kumtoa mtoto huyo awe mtumishi wake.

3. Imani na Bidii:
Watu wengi wanafikiri bidii ni kutumia nguvu tu katika maombi, bali bidii ni ule mzigo; ni muhimu unapokuwa unaomba uwe na mzigo wa kuombea. Ili uzae matunda katika maombi ni lazima uwe sawa na mama mjauzito aliye katika kuzaa; lazima uwe na uchungu yaani umaanishe. Vivyohivyo kupokea kutoka kwa BWANA Unatakiwa umaanishe na lazima uamini pia kuwa ni wakati wako wa kupokea kutoka kwa BWANA. Unapoomba unatakiwa moyo na akili yako iwe kwenye kile unachohitaji. Kuna watu wanabidili maombi kila kukicha kwa kuhisi kuwa Mungu awasikii lakini bidii ni kubaki kwenye jambo hilo hadi uone amani moyoni kuwa BWANA ameshatenda na hili jambo ndilo ambalo Eliya alilifanya alipokuwa anaomba mvua kunyesha tena. Eliya alikuwa mwanadamu wa namna moja na sisi alikuwa na Bidii katika maombi.

JAMBO LA KUFANYA:
Baada ya kujua mambo haya ni muhimu kubadili mtazamo wako na jinsi unavyoomba. Mungu anajibu maombi kama ukiomba sawasawa na neon lake. Kwanza uwe na picha ya kile ambacho unataka BWANA akutendee, uombe na imani na bidii. Hapo lazima Mungu akutendee kwasababu hakuna baba ambaye mwanaye atamwomba mkate akampa jiwe au samaki akampa nyoka. Badili mtazamo wako katika maombi yako ili uwe mpokeaji wa maombi yako ni si mwombaji asiyepokea chochote!!!

-FRANK ANDREW-
Resident Pastor G.C.T.C

Sunday, February 3, 2013

UJUMBE: MATUKIO YA KICHAWI (sehemu ya pili)

Na Mchungaji Kiongozi: Josephat Gwajima                                      03 Februari, 2013Josephat Gwajima
SENIOR PASTOR G.C.T.C
UTANGULIZI:

Watu wengi wanajiuliza kwanini tunazungumzia uchawi mara nyingi, hii ni kwasababu shetani hutumia wachawi katika kutenda kazi duniani; na ndio maana katika Biblia kuna maandiko mengi yanayotaja uchawi na wachawi kama ifuatavyo:- Hesabu 23:23 24:1; 1Wafalme 9:22; 2Wafalme 17:17; Isaya 47:9,12; Mika 1:12; Nahumu 3:4; Matendo ya Mitume 8:9; 18:11; Wagalatia 5:20; 3:1; Ufu 9:21. Ni kweli tumepewa mambo yote na Mungu kama vile afya na mafanikio lakini shetani kupitia wachawi amekuwa akizuia, hivyo tunatakiwa kushughulika nao katika ulimwengu wa roho.. Katika sehemu ya kwanza ya somo hili tuliona kwa habari ya Ayubu ambapo shetani alipata ruhusa ya kugusa maisha yake. Shetani hakumtokea Ayubu kwa namna ambayo angemfahamu kuwa ni shetani, lakini alimjia kwa njia ya matukio, kumbe waweza kuwa unapitia kwenye hali mbaya kumbe ni matukio yanayosababishwa na wachawi.Wakristo walio wengi wanapambana na shetani bila kujua nguvu za adui wanae pamaba nae. Nchi ya Japani ilipokuwa haijui kuwa Marekani wana bomu la nyuklia; waliwachokoza wakidhania kuwa watashinda, Lakini matokeo yake walishindwa kwasababu walikuwa hawajui nguvu ya wanayeshindana naye. Mara nyingi watu wengi hupambana na shetani bila kujua nguvu zake na matokeo yake wengi huishia kushindwa. Huwezi kupambana na adui usiyemjua,  vivyohivyo ili uweze kumshinda shetani ni lazima uanze kwa kutafuta maarifa kuhusu yeye.MAFURIKO YA KICHAWI:

Ufunuo 12:13-16 Yule Joka alikuwa shetani, Biblia inasema Yule joka akatoa maji kama mto; kwa kawaida ingeonekana kama mafuriko ya maji dhidi ya yule mwanamke. Kumbe kuna matukio yanaweza kutokea kwenye maisha yako au kwenye nchi, na kumbe yamesababishwa na wachawi. Si kila moto au mafuriko ni ya kiasili, mengi huwa yanasababishwa na shetani ili kuua watu ili awashushe kuzimu. Kuna matukio yanatokea unadhania kuwa ni ya kawaida kumbe yameletwa na wachawi ili kuangamiza watu. Ni muhimu kujifunza kuyaangalia matukio kwa jicho la rohoni.BIASHARA ZA KICHAWI:

Ezekieli 28:16, 18. “kwa wingi wa uchuuzi wako; watu walikujaza udhalimu” shetani mfanya biashara naye hutenda kazi pamoja na wachawi na waganga wa kienyeji. Kwa njia hii shetani anafunga maisha ya watu, na ndio maana  kuna watu wanafanya biashara za kichawi, Yaani wanamwendea shetani halafu wanamuomba aiwezeshe biashara yao kwa kumpa shetani ama damu au kafara. Wachawi wanapokuwa wanatoa kafara, huwa wanakuwa wanafanya biashara na shetani. Ufunuo 18:1- mstari 5” “wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwasababu ya kiburi chake” mstari 11” “nao wafanya biashara wa  nchi walia na kuomboleza maana hapana mtu anunuaye bidhaa zao tena” mstari 13  biashara ya roho na miili ya wanadamu. Kumbe biashara nyingi unazoona watu wanafanya duniani, ni biashara za kichawi. Yaani mtu anafanya biashara lakini ndani yake kuna uvuvio wa kishetani, Nahumu 3:4. Ndio maana biashara za watu wengi hazifanikiwi wakati huohuo watu wanaomtegemea shetani wanafanikiwa kwa haraka ni kwasababu wameuza roho zao kwa shetani.Matendo ya Mitume 16:16-17; 19:24 “aliyewapatia bwana zake faida nyingi” biashara hizi zipo kabisa, na ndio maana unaweza kufanya biashara lakini wenzako wanauza zaidi kuliko wewe hata kama wote mnauza bidhaa ileile, kumbe wenzako wamenuiza ili wao wauze na wewe usiuze. Ni vizuri kuanza kufanyabiashara na BWANA, yaani kabla ya kuanza biashara ni muhimu kufanya maombi kwanza ili kuiweka biashara yako katika ulinzi wa Mungu. Unapotaka kuanza biashara fanya na BWANA.MAGONJWA YA KISHETANI:

Kuna watu ni wagonjwa sasa kwasababu ya wachawi. Magonjwa mengi sana husababishwa na wachawi. Unaweza kuwa unasumbuliwa na magonjwa yasiyopona kwasababu ya chanzo chake ni cha rohoni. Na ndio maana unapooumwa hata kama utaenda hospitali unatakiwa usiache maombi kwasababu shetani anaweza kusababisha magonjwa, hata Ayubu aliumwa majipu mabaya ambayo kimsingi yalisababishwa na shetani.BIBLIA NA MATUKIO YA KICHAWI:

Mathayo 9:32 “tazama walimletea mtu bubu mwenye pepo, na yule pepo alipotolewa alinena” huyu ni mtu ambaye watu walipomuangalia walimuona ni bubu. Cha ajabu Yesu alipomuona hakushughulika na ububu bali alishughilika na pepo kuonyesha kwamba ule ububu ulisababishwa na pepo. Kuna mambo mengi ambayo yanasababishwa na shetani, hivyo unatakiwa kuyashughulikia.

Mathayo 13:10-15 “alikuwa na pepo wa udhaifu kwa muda wa miaka kumi na nane…” 15” “na huyu mwanamke aliye uzao wa Ibrahimu ambaye shetani shetani amemfunga” watu walishamzoea kumwona kuwa ni mama mwenye kibiyongo yaani hawezi kujinyoosha kabisa lakini Yesu alipomtoa pepo Yule mama alipona.Wachawi wapo na watu wengi wanalogwa, Kumbukumbu la Torati 18:11; watu wanalogwa na wanalogeka, matatizo ya watu wengi yanasababishwa na shetani kupitia matukio ya kichawi. Marko 9:17; kuna magonjwa ambayo yanakuja kwenye maisha ya mtu kwasababu ya kulogwa. Katika utendaji kazi wa shetani anaweza akaingia ndani ya mtu na kumfunga, lakini pia shetani anaweza kumkandamiza mtu akiwa nje ya mwili na ndio maana kwa watu waliokoka lakini hawapigani vita ya rohoni wanaweza kujikuta wanakandamizwa na shetani akiwa nje yao. 1Wathesalonike 2:18, Paulo hakuwa amepagawa na pepo lakini shetani alimzuia. Zekaria 3:1. Shetani anaweza kukuzuia kutokea nje, yaani unahitaji kwenda nje ya nchi lakini shetani anakuzuia kupitia mtoa pasi ya kusafiria. Matendo ya Mitume 13:6 hata wachawi hupambana pia ili kukuzuia, ni muhimu kuishi maisha huku ukijua kunakushindana rohoni. JINSI YA KUSHINDA DHIDI YA MATUKIO YA KICHAWI

Mpokee Yesu kwanza; huwezi kushindana na shetani kama hujaokoka, ni muhimu umpokee Yesu kwanza ili akuwezeshe kupigana katika vita dhidi ya shetani. Jifunze kuomba mwenyewe; baada ya kuokoka kuna amani ya mwanzo unayoipata ile isikufanye ukasahau kuwa tupo vitani, kama tulivyoona hapo juu wanaoshindana nawe wanaweza kuwa ndani yako au nje yako. Katika hali hiyo unachotakiwa kufanya ni kujifunza kuomba mwenyewe kwasababu hata ukitegemea kuombewa kila siku, kuna muda utakuwa mwenyewe, na hapo unatakiwa usimame mwenyewe. Mtu uliyeokoka unatakiwa uhame kwenye ule wokovu wa kuombewa uhamie kwenye wokovu wa maarifa na kupambana kwa kutumia Jina la Yesu Kristo.


-Josephat Gwajima-

Senior Pastor G.C.T.C