google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HATARI YA NDOTO| Jumapili 11 August 2013.


Na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima|Kawe Tanganyika Packers|Dar es Salaam

1.0 Utangulizi

Leo nitafundisha kwa habari ya ndoto. Neno ndoto limeandikwa ndani ya Biblia zaidi ya mara 86. Katika kitabu cha mwanzo pekee neno ndoto limeandikwa zaidi ya mara 30. Katika kitabu cha Daniel neno ndoto limejitokeza zaidi ya mara 22.Kwa kawaida kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho.

Nitafundisha hatari ya ndoto leo kwa mifano ya ndoto za wafalme wawili. Mfalme wa kwanza Nebukadreza aliyekuwa mfalme katika mashariki ya kati. (Danieli 2:1-6) Nebukadreza alitawala kipindi ambacho ufalme wake ulikuwa mkubwa mashariki ya kati yote na dunia yote. Mfano wa pili ni mfalme wa Misri Farao, huyu alikuwa mfalme katika Afrika (Mwanzo 41:1-8).

Daniel 2: 1-6, tunajifunza habari ya ndoto iliyootwa na Mfalme Nebudkadreza. “ Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi ukamwacha….”

1.1 Ndoto ni nini?

Ndoto ni jambo linalotakiwa kumpata mtu siku chache zijazo. Ndoto ni kipimo cha hali ya rohoni ya mwotaji. Mfano mtu akiota anakimbizwa na ng’ombe inaamanisha kuwa kiwango cha nguvu zako za rohoni kimeshuka. Endapo utaota wewe ndio unamkimbiza adui inamaana nguvu zako za rohoni zipo juu. Ndoto ni bayana.


2.0 Msisitizo wa Hatari ya ndoto

Ikiwa ndoto inamfadhaisha mfalme ambaye ni mkuu wan chi, je nini mimi na wewe? Hii inatuonesha kuwa kitendo cha mfalme kutaka kufahamu tafasiri ya ndoto inamaanisha kuwa ndoto ni bayana.

2.1 Mambo ya kufanya ukiota ndoto

(i) Jambo la kwanza la kufanya baada ya kuota ndoto ni kuindika hiyo ndoto
Habakuki 2:2-3; BWANA akanijibu akasema, iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili kila aisomaye apate kuisoma kama maji.

(ii) Baini je ndoto uliyoota ni ya mema au ya mabaya

(iii) Ukiota ndoto ukabaini ni ya mabaya anza kuomba mara baada ya kustuka toka ndotoni. Usisubirie kukuche. Omba kinyume cha hiyo ndoto. Batilisha hiyo ndoto.

2.2 Maandiko yanayofanya baadhi ya watu wapuuzie ndoto

Mhubiri 5:3; “kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi…”
Zekaria 10:2; “kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo…”

Yeremia 23:25; “Nimesikia waliyosema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema nimeota ndoto nimeota ndoto.”

Watu hupuunza ndoto kwa kuwa ndoto huja kwa shughuli nyingi na pia hupuuza ndoto kwa kuwa zipo ndoto za uongo. Kimsingi kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho. Uwepo wa maandiko mawili yanayofanya baadhi ya watu wapuuzie ndoto hauwezi kupuuza ndoto zaidi ya 80 ambao zilikuwa bayana, na Mungu alisema na watu katika ndoto.

3.0 Baadhi ya maandiko yanayotufanya tuzishughulikie ndoto tunazoota

Mwanzo 20:3-5; “Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku…”

Mwanzo 28:12 Ndoto ya Yakobo “…akaota ndoto na tazama ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena tazama malaika wa Mungu wanapanda na kushuka juu yake….”

Mwanzo 31:11”Na malaika wa Mungu akiniambia katika ndoto…”

Mwanzo 31:23-24 “…Mungu akamjia Labani Mshami katika ndoto ya usiku…”

Mwanzo 37:46; ndoto ya Yusuph

1 Falme 3:5-10; Ndoto ya Suleiman

Ayubu 7:14; Ndoto ya Ayubu