Saturday, September 21, 2013

MAANDALIZI MKUTANO WA ARUSHA

Na Mwandishi wetu,

Asubuhi majira ya saa tatu asubuhi majeshi ya Bwana walikutana katika viwanja vya relini,hii ni pamoja na wale waliokua waliofikia sehemu mbali mbali tofauti na kambini.

Baada ya kufika uwanjani watu wote waligawanywa katika makundi kumi yaliyokua chini ya ma MP’s , na makundi yote hayo kumi yalikua chini ya AP.

Baada ya kugawanywa katika makundi imbali mbali majeshi ya Bwana yalipanda mabasi ya ufufuo na uzima kuelekea mahali ambapo walitakiwakwenda kubandika matangazo kwa siku hiyo.

Wakati wakielekea huko walipofika njiani eneo la Mrefu walisimama kwa muda kulisubiri gari la matangazo ambalo lilifika panapo majira ya saa nane mchana.

Wakati gari la matangazo likisubiriwa maeneo ya Mrefu baadhi ya watenda kazi walitumia nafasi hiyo kukaribisha watu wa maeneo hayo katika mkutano unaoanza tarehe 27 /9 /2013.
Baadhi ya mambo yaliyojitokeza wakati huo ni pale baadhi ya watu walionyesha kiu ya kutaka kumpokea Yesu ,ndipo baadhi ya mashepherd wa Ufufuo na uzima walipotumia fulsa hiyo kuongoza watu hao sala ya toba na kuwaombea baadhi yao.
Kati ya mambo yaliyotendeka mahali hapo ni tukio la mamammoja aliyekua miongoni mwa waliompokea Yesu kushuhudia na kusema alikua akisumbuliwa na maumivu ya tumbo muda mrefu na alipokwenda hospitali walisema ana vidonda vya tumbo, lakini baaada ya kuombewa maumivu yaliisha pale pale,

Haikuishia hapo mama mmoja nae aliyekua akisumbuliwa muda mrefu na matatizo ya miguu alipokea ponyaji wake pale pale na kushuhudia kua maumivu yaliyokua yakimsumbua yametoweka mara moja.

Tuliondoka mahali pale majira ya saa nane na nusu mchana na kuwaacha watu wa eneo la mrefu wenye furaha huku wakiahidi kutokukosa katika mkutano baada yakuona Mungu akiwagusa hao wachache waliokua hapo.

Baada ya hapo tuliondoka na kwenda moja kwa moja katika eneo la Tengeru, Eneo hili lilikua na watu wengi kidogo kulingana na shughuli mbali mbali zilizokua zikiendelea mahali hapo.

Majeshi ya ufufuo na uzima yalipofika mahali hapo watu walionekana kuguswa na matangazo hayo na ndipo waliposogea kwenye gari la matangazo kwa wingi ili kusikiliza kilichokua kikiendelea hapo.

Tulipoongea na baadhi ya watu kuwakaribisha kwenye mkutano walionekana kuwa na shauku kubwa yakuhudhuria, huku wengine wakiuliza kanisa lenu liko sehemu gain hapa Arusha ili tuje?

Maeneo ya Tengeru lilibandikwa tangazo kubwa la mkutano lenye picha ya baba (SNP JOSEPHAT GWAJIMA)

Na panapo majira saa 11:45 jioni majeshi ya Bwana yalianza kurudi uwanjani. Wakati tuko njiani kurudi tulifika eneo moja ambapo jina lake halikuweza kupatikana kwa haraka hapo napo liliwekwa tangazo jingine kubwa barabarani.

Majeshi ya Bwana yakarudi uwanjani panapo majira ya saa moja usiku wakafika wote uwanjani,.

Mnamo saa mbili usiku majeshi ya Bwana yaliongozwa na Rp Bryson kufanya maombi na kuzunguka uwanja huku wakipiga majeshi .

Baada ya maombi majeshi ya Bwana walielekea kambini kwaajili ya kupata chakula cha usiku pamoja na kupumzika


IKAWA JIONI IKAWA ASUBUHI, SIKU YA JUMAPILI

Imetayarishwa na Shepherd Frank John Minja.
Na kuhaririwa na Mp Davie M Abson

No comments:

Post a Comment