Na Mch. Josephat
Gwajima
Utangulizi:
Biblia imetaja sana kwa habari ya ndoto, ukisoma katika
kitabu cha Mwanzo pekee, neno “ndoto ” limeandikwa zaidi ya mara 36. Pia,
katika kitabu cha Daniel neno ndoto limeandikwa zaidi ya mara 29. Na ndio maana
Mungu alipotaka watu wake wajenge ama madhabahu au hekelu aliwaonyesha kwanza
katika ndoto; kumbe ujenzi wowote huanzia katika kuona. Vivyo hivyo hata watu
wanaomtegemea shetani huingia ulimwengu wa roho na kujenga kile walichokiona
kutoka kwa shetani.
TABIA YA MUNGU
KATIKA NDOTO:
Kutoka 25:8-9; Mungu akitaka ujenge anaanza kukuonyesha;
ndio maana alimwonyesha pia na Musa na kumtaka ajenge sawa sawa na
alichomwonyesha “exactly like the pattern I will show you” Kutoka 25:37-40; Hii
ni tabia ya Mungu kuwaonyesha watu kupitia ndoto na watu wengi pasipo kujua
wamejikuta wakidharau ndoto.
Ukisoma katika kitabu cha Habakuki 2:2-3; Mungu alimwamuru Habakuki aiandike ile ndoto;
kwasababu asingeweza kufanya kuona kwanza katika ulimwengu wa roho. Na ndio
maana neno ndoto limeandikwa mara nyingi katika kitabu cha Mwanzo kwasababu
hicho ndicho kitabu cha asili (origin). Hiyo inatufundisha kuwa mwanzo wa vitu
huanzia katika ndoto.
Mambo ambayo Mungu anaweza kuyafanya kupitia ndoto:
i)
Mungu
anaweza kufumbua mafumbo kupitia ndoto:-
Mwanzo 40: 2-19; Hapa tunaona kwa
habari ya mwokaji na mwoshaji wa Farao ambao walipata kujua hatari iliyokuwa
imejificha kwa njia ya ndoto. Kwa njia hiyo wote wawili wakajua maisha yao siku
tatu mbele. Kumbe ndoto yaweza kukufunulia mitego au hatari iliyojificha au
kupangwa na watu wabaya.
Farao
alikwisha kupanga kuwa siku ya tatu itakuwa hukumu yao lakini bila kuwambia;
lakini waliweza kufunuliwa katika ndoto. Ni maombi yangu kuwa Mungu na
akuonyeshe hatari zote ulizopangiwa sirini.
ii)
Mungu
anaweza kukurudisha au kukurudishia ulichokipoteza:-
Katika
kitabu cha Danieli pekee, neno “ndoto” limeandikwa zaidi ya mara 29; Danieli
alikuwa uhamishoni Babeli; akiwa huko Mungu akamwonyesha kwa habari ya
kumrudisha mahali pake. Vivyo hivyo katika maisha yako inawezekana ulikuwa na
mafanikio lakini sasa hayapo; au ulikuwa na afya nzuri lakini sasa haipo; katika
ndoto Mungu aweza kukurudisha sehemu unayotakiwa kuwapo.
Na
ndio maana kila siku huwa nasema Tanzania mpya niliyoiona katika ndoto inakuja;
Tanzania yenye maendeleo; yenye hospitali nzuri, yenye gesi, Tanzania yenye
madini inakuja na sifi leo ama kesho mpaka ndoto itimie.
Ni
maombi yangu Mungu akurudishie ile hatma njema ya maisha yako ambayo shetani
aliichukua katika maisha yako.
iii)
Ndoto
zinaweza kukuonya:-
Ndoto
zaweza kukuonya usichukue maamuzi ambayo sio sahihi, uache tabia mbaya ambayo
ina mwisho mbaya. Mathayo 2: 13-16; Baada ya Herode kugundua kuwa
amedhihakiwa na mamajusi akaamua kuua watoto ili amwangamize Yesu; lakini
Yusufu akapewa onyo na Mungu kuwa ampeleke mtoto Misri. Ni kweli Herode
aliangamiza lakini walioangamizwa ni wale ambao baba na mama zao hawakuota
ndoto.
Hapa
tunaona athari moja ya kutoota ndoto, maana madhara yake yaliwahi kugharimu maisha
ya watoto wao. Kupitia ndoto Yesu aliokolewa, Mungu huongea pia kupitia ndoto.
Ndio maana ni muhimu kumwomba Mungu akupe ndoto ya kuokoa familia au ukoo wako.
iv)
Mungu
anaweza kutufariji katika ndoto:-
Katika
maisha unaweza kupitia wakati mgumu, umezungukwa na madeni au kukata tamaa lakini
Kupitia ndoto Mungu aweza kukuonyesha utakuwa nani baadaye. Kwa njia hii Yusufu
alifarijiwa kupitia ndoto; kwa njia hiyo Yusufu alipokea faraja na
kuhakikishiwa ushindi.
Yusufu
alipoota ndoto zilisababisha achukiwe na ndugu zake, na wakamtupa shimoni na
baadaye kumuuza Misri lakini ndoto yake ilibaki palepale. Haikutosha hapo, bali
alisingiziwa ametaka kumbaka mke wa waziri mkuu wa Misri na akaja kufungwa.
Lakini katika mateso yake Mungu alikuja kumfariji kupitia ndoto na kumrudisha
katika nafasi yake.
Vivyo
hivyo katika maisha yako inawezekana ulisingiziwa na kupoteza nafasi ambayo
Mungu alikupa; leo kila aliyekunyang’anya nafasi naamuru uchukue nafasi yake;
nafasi ya ndoa, nafasi ya umeneja, nafasi ya uongozi ninaiamuru irudi kwako
katika jina la Yesu Kristo. Yule Yule aliyekupiga
vita mwaka jana mwaka huu utachukua nafasi yake katika jina la Yesu.
Kutoka katika
ufungwa gerezeni hadi kuwa mkuu katika nchi ya Misri, yote hii ilianza katika
ndoto. Kumbuka ndoto za Yusufu zilianza alipokuwa na miaka 16 lakini alikuja
kuimiliki akiwa na miaka 40. Tatizo la watu wengi wanakata tamaa mapema;
hutakiwi kufa moyo, hapo katikati wakati unaisubiria ndoto unaweza ukapitia
mateso na mabonde lakini ndoto itakuja na itatimia usipozimia moyo.
v)
Mungu
aweza kukuonyesha utakuwa nani baadaye katika ndoto:-
Mungu
hutenda kazi tofauti na sisi tunavyowaza; Yule mtu unayemuona mdhaifu ndiye
ambaye Mungu anamuona shujaa; vivyo hivyo kwa habari ya Yesu, yeye alizaliwa
katika hema ya ng’ombe; Samweli alizaliwa na Hana ambaye alikuwa hazai hapo
mwanzo; Musa naye alitupwa kwenye mto akakulia kwa baba wa kambo; Samson
alizaliwa na mama ambaye alikuwa tasa hapo mwanzo; na ndio maana hata siku moja
usidharau mambo madogo kwasababu ndiyo ambayo Mungu huyatumia.
vi)
Mungu
anaweza kutuonyesha ushindi juu ya adui zetu katika ndoto:-
Kila
mtu ana adui wa maisha wake; awe rais, waziri, mchungaji, au askofu lazima
utakuwa na adui wa maisha yako. Yaani kwa kila hatua unayopiga unatengeneza
marafiki na adui wengi kwasababu hiyo kila mtu ana adui zake. Lakini Mungu
anaweza kukuonyesha ushindi wako katika ndoto. Ukisoma katika kitabu cha
Waamuzi utaona kwa habari za Gideoni ambaye alitakiwa kupigana na Wamidiani;
lakini kabla ya kwenda vitani Mungu akatumia ndoto kumwonyesha ushindi unaokuja
mbele.
Ni
maombi yangu Mungu akuonyeshe ushindi juu ya adui zako katika jina la Yesu
Kristo. Kumbe kupitia ndoto unaweza kuonyeshwa adui ambaye hapendi mafanikio
yako yaani Mungu akupe ushindi dhidi ya hila zake mbaya katika Jina la Yesu.
NDOTO:
Sikumoja
nilikuwa nasafari kutoka nchi moja kwenda nyingine, nikakata tiketi ya kusafiri
kesho yake; usiku wake nikiwa nimelala nikaota ndoto nipo ndani ya lile basi ghafla
nikajiona nipo ndani ya basi na likawa linakwenda; gari likiwa linaendelea
kwenda kulikuwa na mzigo juu ya siti niliyokuwa nimekaa ghafla mzigo ule
ukaniangukia na kila nilipojaribu kuinuka nikashindwa ghafla gari likaanguka
alafu nikashtuka kutoka ndoto.
Nilipoamka
nikaanza kuomba kwa bidii na kwa muda mrefu kufika kituoni nikakuta gari
limeshaniacha; basi nikaomba kusafiri na gari linalofuata la kampuni hiyo. Cha ajabu
tukawa tunafuatana na hilo gari ambalo nilitakiwa nipande mimi; mbele ya macho
yangu nikaona gari lile limepata ajali mbaya na moyoni nikasikia niende
kuangalia katika ile siti niliyotakiwa kukakaa; ndipo nikakuta Yule mtu
amepondwa na jeki iliyokuwa ndani ya begi.
vii)
Mungu
anawezakukuonyesha jinsi ya kumtendea mtu katika ndoto:-
Kupitia
ndoto Mungu anaweza kukuonya juu ya uamuzi mbaya unaotaka kuuchukua juu ya mtu fulani
katika ndoto; hii tunaiona kwa habari ya Yesu ambapo mkewe pilato alionywa
katika ndoto juu ya hatua alizotaka kuchukua Pilato juu ya hukumu ya Yesu.
Kumbe Mungu aweza kumuonya mtu juu ya uamuzi mbaya ambao waweza kumgharimu mtu
huyo kupitia ndoto.
Mungu
anaweza kukuonya juu ya uamuzi unaotaka kuchukua juu ya mtu wakati wa hasira,
wakati wa uoga au wakati mgumu. Mungu huonya kupitia ndoto na ndio maana ni
muhimu kutokufanya maamuzi yoyote wakati wa hasira; hofu; wakati mgumu
kwasababu unaweza kujikuta unafanya maamuzi ambayo sio sahihi. Watu wengi
wamevunja mahusiano mazuri na watu kwasababu ya maamuzi mabaya lakini kupitia
ndoto Mungu aweza kukuonya na kukuonyesha njia ya kufanya.
NINI CHA KUFANYA UNAPOOTA NDOTO:
-
Baada ya kuota ndoto ambayo si nzuri unatakiwa
usimame kinyume katika maombi. Sambaratisha ndoto zote na wasimamizi wake wote
katika ulimwengu wa roho.
-
Na ikitokea umeota ndoto nzuri unatakiwa uiteke
na kuimiliki ndoto hiyo; kushindwa kuchukua hatua kutakufanya usiimiliki hiyo
ndoto. Ukiota umefanikiwa katika biashara fulani, unatakiwa uanze kwa kuomba halafu
chukua hatua ya kuimiliki ndoto hiyo.
-
Ukiota ndoto halafu huilewi ni nzuri au mbaya
unatakiwa uamuru katika maombi kuwa kama ndoto hii ni mbaya ninaisambaratisha
katika jina la Yesu na kama ndoto hii ni nzuri imiliki katika jina la Yesu.
0 Comments