Thursday, October 31, 2013

SEMINA NA MCHUNGAJI MWANGASA NDANI YA UFUFUO NA UZIMA MOSHISEMINA NDANI YA NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA,MOSHI.       TAREHE:  30/10/2013.                                                By:  Mchungaji Mwandamizi Mwangasa


SOMO: KUVUNJA MADHABAHU

Madhabahu ni nini?

Madhabahu ni daraja toka duniani kwenda mbinguni.


Kuna aina mbili za madhabahu

1.       Madhabahu ya Mungu wa Mbinguni

2.       Madhabahu ya shetani(sehemu inayowaunganisha wachawi na shetani)

Amu 6;25-28.

25 “Ikawa usiku uo huo Bwana akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo;

 26 ukamjengee Bwana, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata.

 27 Ndipo Gideoni akatwaa watu kumi miongoni mwa watumishi wake, akafanya kama Bwana alivyomwambia; lakini ikawa kwa sababu aliwaogopa watu wa nyumba ya baba yake, na watu wa mji, hakuweza kuyatenda hayo wakati wa mchana, basi aliyatenda usiku.

 28 Hata watu wa mji walipoondoka asubuhi na mapema, tazama, madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ng'ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu iliyojengwa”.


Gideoni aliagizwa na Mungu akaibomoe madhabahu ya mungu Baali maana kwa wakati ule walikuwa wanamwabudu mungu Baali na kumtolea kafara kama vile ya damu.Kwa kufanya hivyo walikuwa wanapata nguvu kinyume na nguvu za Mungu wa  Mbinguni.


Roho inayomtawala mchawi na kumfanya aende kwenye madhabahu ya shetani ni wivu.Kazi yao katika ulimwengu wa roho ni kujadili jinsi ya kutenda ili kufikia kusudi la kumfunga mtu.Mfano mtoto anapelekwa kwenye makaburi na kufanyiwa zindiko kwa mizimu ya mikoo,na kwa kufanya hivyo matokeo yake ni kuandaa matatizo kama magonjwa yatakayoutesa ukoo mzima mfano ukoo Fulani mabinti wote huwa hawaolewi,tambua ya kuwa kuna madhabahu ilyojengwa kulinda ukoo na laana hiyo lakini tambua leo iko madhabahu ya Yesu kristo inayovunja madhabahu ya kishetani.


Wachawi huwa wanapeleka mashitaka yao kwa shetani lakini leo wewe na mimi tupeleke mashitaka yetu kwa Yesu Kristo ili aivunje madhabahu ya kishetani inayotesa maisha yetu.


Tambua ya kuwa kila kinachotokea mwilini kimeanzia rohoni.Tambua ya kuwa chanzo cha tatizo ni madhabahu iliyowekwa kwa kila tatizo hivyo anza kubomoa chanzo cha tatizo ambacho ni madhabahu mana Bila kubomoa madhabahu wafu hawawezi kufufuka,magonjwa hayawezi kupona na leo tumezikamata nguzo mbili ambazo ni mauti na kuzimu na ni lazima zibomolewe.


Tambua ya kuwa wewe ni jeshi la Bwana linakwenda kubatilisha kila mpango wa giza maana yeye ni Bwana wa mbwana na ni mfalme wa wafalme.Ukiamua kusimama kwa uaminifu mbele za Bwana hata mashetani na wachawi wafanyeje hawataweza maana imeandikwa katika     Zaburi 34:7 “Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa”.
Usisubiri mapepo na mapepo na mashetani wakuvamie,anza kuwavamia leo kwa Jina la Yesu,simama kama mwanajeshi wa Bwana anza kukataa aibu,kupuuzwa,magonjwa kwa Jina la Yesu maana vita ya rohoni lazima uamue kuokoka maana wachawi hawamwogopi mtu yeyote ambaye hajaokoka na nuwa Mwanajeshi wa Bwana.  

Tuesday, October 29, 2013

IBADA KUTOKA NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA MOSHIIBADA KUTOKA NYUMBA YA UFUFUO NAUZIMA  MOSHI.                                            
SOMO: DALILI ZA MTU ALIYECHUKULIWA MSUKULE
TAREHE:  29/10/2013.
MCHUNGAJI KIONGOZI: JOSEPHAT GWAJIMA
MCHUNGAJI MWANDAMIZI:MWANGASA

Shetani yupo na anafanya kazi lakini watu wengine hawaamini kama shetani yupo.Mtu anaweza kuingiwa au kutupiwa mashetani asiweze kula wala kunywa.Pia mashetani yanaweza kumfanya mtu akonde na kuwa mwembamba.
Mark 9:18 na kila ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze”.
Pepo anaweza kumwekea mtu kifafa,kutaliwa na laana.Mark 9:20 “Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu”.

Dalili za mtu aliyechukuliwa msukule.

1.Anaanza kuwatokea jamaa zake baada ya kufariki.Kuwa anaonekana mtu aliyekufa ni dalili ya watu wa familia kuwa na mashetani.

2.Baada ya kufariki anatokea mtu ndani ya familia anang’ang’ania  au kulazimisha mazishi yafanyike siku hiyo hiyo.

3.Baada ya mazishi,siku ya pili au ya tatu kaburi la marehemu huyo linaanza kutitia,hii ni kwa sababu mtu aliyechukuliwa msukule anakuwa bado ndani ya mwili.  

4. Marehemu anaonekana ama mrefu au mfupi sana zaidi ya kipimo cha mwanzo kipindi cha uhai wake.Hapa yawezekana wamepima gogo refu au fupi Ukiona vile Anza kuomba na kuita “Njoo kwa Jina la Yesu” 

5.Kifo cha ghafla.Binadamu ni kama gari jipya hivyo haiwezekani likawa jipya halafu likaharibika bila sababu,hivyo ni lazima augue.Hospitari wanaweza kusema amepata mshtuko wa moyo.Na roho ya kifo huwa inatumwa kwa muda inakaa ndani mwako wala siyo siku moja hivyo jifunze kufuta tarehe ya ya kifo kilichopangwa kwa Jina la Yesu.

6.Mgogoro kwenye familia baada ya msiba.Watu wengine wana macho ya rohoni,moyo unachoongea jua kipo.

7.Maneno ya marehemu wakati anakata roho.Mfano “hao manakuja,hao wananichukua”.Haya maneno yana maana sana,maneno haya yazingatie hivyo ita mtu huyo aliyechukuliwa.

8.Maiti inabadilika sura.Wachawi wanaweza kumchukua mtu na kukuachia kitu.Mara baada ya kugundua kachukuliwa anza kuomba kwa Yesu na tumia maandiko.

9.Watu wanalazimisha kulia.Watu hao waweza kuwa ndugu au watu wengine kama vile majirani.Mfano mfiwa aweza kuambiwa “wewe umefiwa na mama halafu hulii?”.Nia yao ni wewe(mfiwa) ukiri kuwa ndugu yako kafariki.Ukiona hivyo kataa kukiri haraka kuwa mtu waka amekufa.Mfano Yesu alisema Lazaro hajafa bali amelala.Lengo la kulazimisha watu kulia ni kurahisisha mtu kuchukuliwa.mana wasipolia hawawezi kumchukua na kwenda naye.

10.Wanajitokeza watu wanazuia wachungaji(walokole) wasimwombee.Wanaweza kusema hiyo “siyo imani yetu” au “kaombee huko lakini siyo hapa”.

11.Wanandugu wanakataa watu wsiombe wakisema hata akirudi sisi kwetu ni uchuro. 

12.Ndugu wa marehemu wanawaita na kuwapa dawa ili marehemu asije kukutokea tena.

Kwa hiyo ni muhimu inapotokea kuna kifo au tukio limetokea na kuna dalili zilizotajwa, ni vema kuliita Jina la Yesu.

Friday, October 25, 2013

MKUTANO MKUBWA WA INJILI UNAOENDELEA KATIKA VIWANJA VYA MASUJAA MJINI MOSHI, NA MCH.KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA WA KANISA UFUFUO NA UZIMA


MKUTANO MKUBWA WA INJILI UNAOENDELEA MJINI MOSHI.                           
TAREHE:  25/10/2013.                           
SOMO: LAANA ZA FAMILIA 
Na Mchungaji Kiongozi: Josephat Gwajima
Mch.Kiongozi Josephat Gwajima.

Kuna familia zinaandamwa na matatizo mbalimbali, mfano. matatizo ya kutokuolewa,umasikini au matatizo mengine yanayotokana na laana za familia. Mchungaji Kiongozi alihaidi kuvunja matatizo yote ya kifamilia yanayoletwa na familia,na kusema kuwa leo kuna mambo ambayo anataka kuusemea ukweli.
kuna familia ambazo zinakuwa  zipo chini ya laana fulani na hata mtu akipenya anapenya kwa taabu sana.
Sasa tutaangalia siri iliyopo nyuma yake halafu utafunguliwa katika Jina la yesu.

Tukiangalia maandiko 

Mwanzo 9:18-25..
18 Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani.
 19 Hawa watatu walikuwa wana wa Nuhu na kwa hao nchi yote ikaenea watu.
 20 Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;     
 21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.
 22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
 23 Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.
 24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.
 25 Akasema,Na alaaniwe Kaanani;Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.

Tukiangalia kitu hiki cha ajabu, Hamu ndiye aliyeona uchi wa babaye lakini anayelaniwa ni mwanaye Kanaani.Hapa tunaanza kujifunza jambo ya kuwa jambo linapotokea kwa wazazi linakwenda kwa watoto,wajukuu na watoto na watoto.

Lakini Kanaani alikuja kuwa na watoto baadae,hebu tuwaone watoto waliozaliwa na Kanaani aliyelaaniwa walikuwa kina nani na maisha yao walikuwaje;

Mwanzo 10:15-19. 
 15 Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi,
 16 na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi,
 17 na Mhivi, na Mwarki, na Msini,
 18 na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Baadaye jamaa za Wakanaani walitawanyikana.
 19 Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha.

Ndio haohao watoto ambao wana wa Israeli wakati wanatoka katika nchi ya utumwa, Mungu alimwambia Musa waangamizwe njiani wauawe wote,hii inatupa picha ya ajabu ya kwamba wote waliozaliwa na Kanaani walikuwa na laana na ndio Mungu akamwambia Musa ili wauawe.

Tukiangalia tena maandiko matakaifu

Kitabu cha Kutoka 3:7-8. 
 7 Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;
 8 nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.

Hapa tunaanza kuona kumbe laana zinaweza kutokea katika familia,hivyo inawezekana leo hii una matatizo siyo kwa sababu umetenda dhambi ila ni kwa sababu kuna mambo yalitendwa kwenye familia yenu yankuandama mchana na usiku, hivyo naomba leo unifatilie kwa makini ili tuvunje hizo laana na Baraka yako itakwenda kutokea katika jina la Yesu.

Kitabu cha Kutoka 3:17
“Nami nimesema, Nitawapandisha kutoka katika mateso ya Misri na kuwaingiza katika nchi ya Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, nchi ijaayo maziwa na asali”
Hapa Mungu alikuwa akiongea na wana wa Israeli.Kwa hiyo utaona mojawapo ya alama ya laana ni kunyang’anywa kile kitu ulichokimiliki kwa nguvu zote.

Kitabu cha Mithali 26:2 
“Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.”

Kwa hiyo kumbe maana yake ni  laana yenye sababu inampiga mtu.
Lakini utaona pia kuwa mambo ya imani nayo yanaweza kwenda familia hata familia.2Timoteo 1:3-5. 
 3 Namshukuru Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana.
 4 Nami natamani sana kukuona, nikiyakumbuka machozi yako, ili nijae furaha;
 5 nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.

Maelfu ya wakazi wa mjini Moshi waliofika kwenye mkutano wa Mchungaji Kiongozi Jospehat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima., wakiwa wamenyoosha mikono yao kumkabidhi Yesu maisha yao.