Tuesday, October 8, 2013

MCHAWI AUMBUKA HUKU MWANAMKE ALIYEKUFA AKIRUDI MKUTANONI ARUSHA

Tukio hili la aina yake lilitokea siku ya nne ya mkutano wa Mchungaji Josephat Gwajima jijini Arusha; kufufuka kwa mwanamke huyo aliyezikwa miezi mitatu iliyopita ilifuatana na tukio lingine la aina yake lililovuta hisia za wengi ambapo mwanamke mwingine anayesadikiwa kuwa mchawi kuanguka wakati mkutano ukiendelea.

Mchawi akiwa ameshikiliwa na watendakazi wa Ufufuo na Uzima kuepusha watu wenye hasira wasimuumize


 Mwanamke huyu alianguka ghafla muda mfupi baada ya Mchungaji Josephat Gwajima kuomba maombi ya mwisho na kuamuru kazi zote za wachawi ziharibike katika jiji la Arusha. Maelfu ya wakazi wa Arusha waliohudhuria mkutano huu, walioshuhudia tukio hilo wanasema walipokuwa katika harakati za kurudi majumbani kwao ndio ghafla akaanguka huyu bibi kutoka angani nakumdondokea mtu mmoja ambaye alipooza mkono mmoja hapo hapo.

Waumini hao wakiwa na ghadhabu kubwa kutokana na kukereka sana na matendo ya kishirikina wanayotendewa, walimkamata bibi huyo na kumpeleka madhabahuni ambapo Mchungaji Gwajima alikuwa akihubiria.

Bibi huyo alifikishwa salama akiwa anahema sana huku akiwa hajielewi vizuri baada ya hapo mahojiano yalifuata.

Mchawi aliyeanguka (mwenye nguo nyeusi) na kulia ni mwanamke aliyefufuka mara baada ya mchawi huyo kuanguka


Tukio hilo liliambatana na atukio lingine la kusisimua la mwanamke mmoja ambaye kwa mujibu wa watoto wake, alikufa miezi mitatu iliyopita. Mama huyo alionekana muda mfupi baada ya yule mchawi kuanguka; watoto wake walipomuona wote watatu walizimia hapo hapo kwa kile kilichoelezwa kuwa hawakuamini macho yao.

Watoto wake wakilia muda mfupi kabla ya kuzimia na kupoteza fahamu.
Walipozinduka ndipo waliposema kuwa mama yao alikufa na kuzikwa kabisa; lakini wanashangaa kumuona tena, wanamshukuru Yesu Kristo kwa matendo makuu.
Watoto wake wakiwa hawaamini macho yao

MUNGU KWETU SISI NI MUNGU WA KUOKOA NA NJIA ZA KUTOKA MAUTINI ZINA YEYE!!!
Wakazi wa Arusha walioshuhudia tukio hilo kubwa na la aina yake.

No comments:

Post a Comment