SEMINA NDANI YA NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA,MOSHI. TAREHE: 30/10/2013. By: Mchungaji Mwandamizi Mwangasa
SOMO: KUVUNJA MADHABAHU
Madhabahu ni
daraja toka duniani kwenda mbinguni.
Kuna aina mbili za madhabahu
1.
Madhabahu ya Mungu wa Mbinguni
2.
Madhabahu ya shetani(sehemu
inayowaunganisha wachawi na shetani)
Amu 6;25-28.
25 “Ikawa usiku uo huo Bwana
akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba,
ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo
karibu nayo;
26 ukamjengee Bwana, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu
zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa
kuni za ile Ashera uliyoikata.
27 Ndipo Gideoni akatwaa watu kumi miongoni mwa watumishi wake, akafanya
kama Bwana alivyomwambia; lakini ikawa kwa sababu aliwaogopa watu wa nyumba ya
baba yake, na watu wa mji, hakuweza kuyatenda hayo wakati wa mchana, basi aliyatenda
usiku.
28 Hata watu wa mji walipoondoka asubuhi na mapema, tazama, madhabahu ya
Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule
ng'ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu iliyojengwa”.
Gideoni
aliagizwa na Mungu akaibomoe madhabahu ya mungu Baali maana kwa wakati ule
walikuwa wanamwabudu mungu Baali na kumtolea kafara kama vile ya damu.Kwa kufanya
hivyo walikuwa wanapata nguvu kinyume na nguvu za Mungu wa Mbinguni.
Roho
inayomtawala mchawi na kumfanya aende kwenye madhabahu ya shetani ni wivu.Kazi
yao katika ulimwengu wa roho ni kujadili jinsi ya kutenda ili kufikia kusudi la
kumfunga mtu.Mfano mtoto anapelekwa kwenye makaburi na kufanyiwa zindiko kwa
mizimu ya mikoo,na kwa kufanya hivyo matokeo yake ni kuandaa matatizo kama
magonjwa yatakayoutesa ukoo mzima mfano ukoo Fulani mabinti wote huwa
hawaolewi,tambua ya kuwa kuna madhabahu ilyojengwa kulinda ukoo na laana hiyo
lakini tambua leo iko madhabahu ya Yesu kristo inayovunja madhabahu ya
kishetani.
Wachawi
huwa wanapeleka mashitaka yao kwa shetani lakini leo wewe na mimi tupeleke
mashitaka yetu kwa Yesu Kristo ili aivunje madhabahu ya kishetani inayotesa
maisha yetu.
Tambua
ya kuwa kila kinachotokea mwilini kimeanzia rohoni.Tambua ya kuwa chanzo cha
tatizo ni madhabahu iliyowekwa kwa kila tatizo hivyo anza kubomoa chanzo cha
tatizo ambacho ni madhabahu mana Bila kubomoa madhabahu wafu hawawezi
kufufuka,magonjwa hayawezi kupona na leo tumezikamata nguzo mbili ambazo ni
mauti na kuzimu na ni lazima zibomolewe.
Tambua
ya kuwa wewe ni jeshi la Bwana linakwenda kubatilisha kila mpango wa giza maana
yeye ni Bwana wa mbwana na ni mfalme wa wafalme.Ukiamua kusimama kwa uaminifu
mbele za Bwana hata mashetani na wachawi wafanyeje hawataweza maana imeandikwa
katika Zaburi 34:7 “Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa”.
Usisubiri mapepo na mapepo na mashetani wakuvamie,anza kuwavamia
leo kwa Jina la Yesu,simama kama mwanajeshi wa Bwana anza kukataa
aibu,kupuuzwa,magonjwa kwa Jina la Yesu maana vita ya rohoni lazima uamue
kuokoka maana wachawi hawamwogopi mtu yeyote ambaye hajaokoka na nuwa
Mwanajeshi wa Bwana.
0 Comments