Mch.Kiongozi Josephat Gwajima |
Jumapili Tarehe 17.11.2013
Na Mch. Josephat Gwajima
Nimeamua
kuliita hili somo vita sababu tunakwenda kupigana vita moja kwa moja na majeshi ya wafu waliokufa katika dhambini
1 Samwel 28:6-20
“…Ukanipandishie yeye nitakaye mtaja
kwako…” tunaoana hapa mfalme anakwenda kwa mganga wa kienyeji anaomba
apandishiwe mtu aliekufa miaka mingi, Hapa tunaona kumbe mtu aliekufa anaweza
kupandishwa na waganga wa kienyeji kutoka kuzimu na akapanda/akazuka.
1
Samwel 28:11 “…Nipandishie Samwel...” hapa tunaona Samwel alikuwa
amekufa lakini mfalme sauli anamwambia mganga wa kienyeji nipandishie Samweli.
1
Samwel 28:15 “…Ndipo Samwel akapanda na akamwambia mbona umenitaabisha
mimi hata kunipandisha juu...” Kumbe mtu
aliekufa anaweza akapandishwa na akazuka kikweli kweli (Samweli akazuka juu),
1
Samwel 28:19 “….Tena pamoja na wewe Bwana atawatia Israel mikononi mwa
Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwepo pamoja nami…” Haya ni maelezo
anayoyatoa Samweli baada ya kuzuka juu. Akatoa maelezo kwamba baada ya siku
tatu utakufa wewe na wanao na mtakuwa mahali hapa name, yaani na nyie
mtapandishwa kama mlivonipandisha mimi.
Ukisoma theolojia kuna ubishani mwingi
unaendelea, wanatheolojia wengi wanasema sababu Samwel alikuwa mtu wa Mungu,
sasa ilikuaje mpaka mganga wa kienyeji akaweza kumpandisha, hivyo husema huyu hakuwa
Samweli bali ni pepo (Samweli feki). Lakini mimi nataka nikuambie kuwa huyo
alikuwa ni Samweli mwenyewe ndio maana aliweza kumpa maelezo mengi sana,
ikiwemo kwamba wewe umemuacha Bwana, na umeamua kunitaabisha kunipandisha juu, hivyo
baada ya siku tatu wewe na familia yako mtakufa.
Mfalme Sauli alipoona hajibiwi kwa
maono wala kwa ndoto, ndio maana akaamua aende kwa mganga wa kienyeji, ndio
maana mimi huwa na kwambia kila kiongozi ambaye hajaokoka anamganga wake wa
kienyeji, Mwanadamu kwa asili huwezi ukawa mtupu, ni lazima uwe umeungamanika
na madhabahu ya mwanakondoo ama madhabahu ya lusifa. Mimi mwenyewe unavyoniona
hapa kuna mamlaka nyuma yangu nimeungamanishwa nayo. Usifikiri leo Ufufuo na
Uzima tupo hivi, ukadhania tumeibuka buka tu, hapana kuna vita huko nyuma
tumepigana.
Sauli amekwenda kwa mganga wa
kienyeji akaomba apandishiwe Samweli ili amuulize limpasalo kutenda. Sauli
alijificha ili asijulikana na mganga wa kienyeji kama ni mfalme, maana wafalme
walikuwa hawaruhusiwi kwenda kwa waganga wa kienyeji. Baada ya mganga wa
kienyeji kuanza kumpandisha Samweli alipiga kelele, akamwambia mbona
umenidanganya, (mganga wa kienyeji viliumana na samweli alivokuwa anazuka),
Sauli akauliza kwanai anayezuka ni nani akamwambia akasema ni mzee anamavazi
meupe anazuka katika nchi. Hapo usifikiri kiliwekwa kikopo cha maji, Sauli
akamuona Samweli kwenye maji hapana, Samweli alipanda akaanza kuongea ndani ya
mganga wa kienyeji. Inanifurahisha hiimaana mganga wa kienyeji badala ya
kupandisha vibwengo akapandisha Samweli, na Samweli akatoa maelekezo.
Mchungaji Kiongozi,Josephat Gwajima, akihubiri ndani ya nyumba ya ufufuo na uzima, Kawe, Dar es Salaam |
Watu wakifa wanakwenda wapi?
Kabla Yesu hajafa msalabani kuna
sehemu ilikuwa inaitwa shiol hili neno ndio hilo limetafsiriwa na biblia
linaitwa kuzimu, yaani ulimwengu wa wafu, ama eneo wanalokaa wafu. Waliokufa
katika dhambi ama waliokufa katika haki. Shiol ilikuwa imegawanyika sehemu
mbili shiol ya watu waliokufa katika haki
na shiol ya watu waliokufa katika dhambi,
na hii ilikuwa kabla Yesu hajafa msalabani.
Mwanzo 37:35 “…Nitamshukia mwanangu hata kuzimu nikiwa
nasikitika…” Yaani hapa Yakobo anamaanisha akifa atamshukia mwanae Yusufu huko
kuzimu, hii ilikuwa ni kuzimu ya waliokufa katika haki.
Torati 32:22 “…Moto
umewashwa kwa hasira yangu unateketea hata chini ya kuzimu…” Hii ni kuzimbu ya
waliokufa katika dhambi.
“Kusimu
upande wa wenye haki, na kuzimu upande wa waliokufa dhambini Kabla ya Yesu
Kristohajafa msalabani”
1 Samweli 2:6 “…Hushusha hata kuzimu,
tena huleta juu…” Zaburi 6:5 “…Maana mautini hapana kumbukumbu lako; katika
kuzimu ni nani atakayekushukuru?...” Zaburi 16:10 “…Maana hutakuachia
kuzimu nafsi yangu…” Yuda 1:6 “...Amewaweka vifungo vya
milele chini ya giza…” kuzimu kwa lugha ingine ni chini ya giza kwenye vifungo
vya milele.
Yesu alipokufa akashuka kuzimu ya
waliokufa katika dhambi akamnyang’anya yule joka ufunguo wa kuzimu na mauti,
halafu akaeleke upande wakuzimu ya Ibrahimu (kuzimu ya walikufa katika haki)
akawaambia yule uzao wa mwanamke ndio mimi, akawahubiria manabii wote huko
kuzimu, na kuwaambia nimekuja kuwahamisha twende juu mbinguni, huku sio mahala
penu. Yale makaburi kufunguka ilikuwa ni ishara ya uhamisho wa watu wote
waliokufa katika haki kutoka kuzimu ya chini na kwenda mbinguni (paradiso) kule
Yesu anakaa. Yesu akawaambia sasa tunahama huku tunaenda paradiso. Kwa hiyo
baada ya hapo kuzimu ikawa ni mahali pa wafu waliokufa kwatika dhambi na paradiso
(mbinguni) ikawa ni makao ya waliokufa katika haki huko wakimuimbia Mungu,na
kufurahi.
Sasa kama vile Samweli
alivyopandishwa kutoka kuzimu, kaganga kamama kakampandisha Samweli juu, hivyo
ndivyo ambavyo leo mtu aliekufa katika dhambi inawezekana akaitwa na waganga wa
kienyeji na akaja, wakamtumia kuharibu ukoo kama wawezavyo, Samweli alipanda
lakini mganga alishindwa kumpa maelekezo sababu alikuwa mtakatifu akiwa
duniani, lakini mababu na mabibi waliokufa katika dhambi wakipandishwa
wanaamrishwa wafanye kile mganga anataka.
Kama tulivyoona aliekufa katika haki akaenda
mbinguni, humuimbia Mungu na kufurahi huko mbinguni, na wale waliokufa katika
dhambi hushuka kuzimu (kifungoni) na kutumika kwa kazi za kuzimu. Na ndio maana
leo nasema lazima tupigane nao vita.
Unapokata roho huwa kuna malaika
maalumu wanaochukua roho yako, kama ulikuwa unatenda dhambi malaika wa giza
wanabeba roho yako wanashusha mpaka kuzimu(gereza la milele), na kama ulikuwa
unatenda haki, malaika kutoka mbinguni wanabeba roho yako na kuipeleka mbinguni
(pradiso), Ufunuo 20:13. “…Kuzimu ikawatoa watu waliokuwa ndani yake…” Kuzimu
ni makao makuu ya shetani, na ziwa la moto ni sehemu ya hukumu ya wale
waliokufa katika dhambi, ukishafika hapo unakuwa mfungwa, na unaanza kumtumikia
shetani. Babu yako yule aliekufa katika dhambi yupo kuzimu hajakaa tu kule,
yupo anapiga mzigo huko, ndio maana utasikia watu tunaowarudisha msukule hapa,
ama watu waliokuwa wamekufa wakifufuka hapa kwetu utasikia kazi yangu ilikuwa
ni kwenda kwenda kuua watoto wadogo mahosipitali wengine utasikia nilikuwa
nasababisha ajali barabarani, hizo ndizo kazi za wafu huko kuzimu.
Mtu anajiuliza hivi watu wanawezaje
kumtupia mtu mapepo hata 1000, unauliza huyu ana akiba ya mapepo kiasi gani,
kumbe mengine sio mapepo bali ni watu waliokufa wanatumikishwa na shetani, wapo
kuzimu lakini wanatumwa kuja duniani, na huwa wanatumwa kwenye koo zao kufanya
uharibifu sababu wao wanazijua hizo koo zao vizuri, ni rahisi kushambulia kwa
mafanikio makubwa. Kwanza wanafahamu lugha ya ukoo wenu, wanamfahamu baba wa
ukoo, wanafahamu madhaifu yenu yote, ndio maana vita yako huwa inakuwa kali
kweli. Shetani huwa anawatuma anawaambiakama vile wewe ulivyokuja huku
katuletee shangazi yako, ndio maana utasikia watu wanalalamika bibi yangu
alikufa kwa kansa na mama yangu nae kwa kansa na mimi nina kansa sasa hivi, huu
ni ugonjwa wa ukoo! Hakuna ugonjwa wa ukoo ni wafu wanatenda kazi katika ukoo.
Makundi
yanayoshambuliwa sana na majeshi ya wafu
1. Wale wanaochukua majina ya
ndugu wa ukoo ambao hawajaokoka (majina ya mabibi, mababu, shangazi).
Tuangalie sana majina tunayowapa
watoto, utasikia mtu anamwita mtoto dragon, astrorogy, au momony angalia utalia,
usimpe majina ya ndugu wa ukoo waliokufa watoto wako kama hujui maana yake,
chagua majina yanayompa utukufu Mungu, Glory, Ruth, Grace….
Kwanini agano jipya linaanza na
kutaja ukoo wa Yesu?
Hii walitaka kutuonesha kwamba ukoo
wa Yesu hauna mganga wa kienyeji, wala msoma nyota, wala darweshi, wate
walikuwa watu wa haki.
2. Wale
wanaopenda/wanaoendekeza mila za familia
Utasikia desturi ya ukoo wetu ndugu
yeyote anaekufa wote tutanyolewa vipara, mtoto akizaliwa lazima kitovu apewe
shangazi, lazima tukajengee makaburi ya babu. Ukiwa unashiriki hizi taratibu
lazima majeshi ya wafu yatakupata tu.
3. Wale wanaopenda makabila
kuliko kumpenda Mungu
Namna ya
kuomba
Kwa jina la Yesu ninajitenga kabisa,
na watu waliokufa kwenye dhambi. Mimi ni wa ukoo wa Yesu, ninajitenga na nyie
kwa jina la Yesu. Jina lolote la mtu alielala katika dhambi, ninajitenga nalo
kwa jina la Yesu
Jitenge na umasikini wa ukoo,
umasikini wa bibi, umasikini wa babu, umasikini wa shangazi, jitenge na ukoo wako
kwa damu ya Yesu, najitenga kutoka babu nababu na babu, nawaamuru muachie mali
zangu, achia afya yangu, kata kamba zote za ukoo, kamba za familia kwa jina la
Yesu.
0 Comments