google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUWAFYEKA WATUNZA KUMBUKUMBU

                                                                                                       
Utangulizi

Kwenye biblia shetani anaitwa mshitaki wa ndugu. Ufunuo 12:10. "Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.".1Petro 1:8

Mahakama nyingi hazifanyi kazi usiku, lakini mahakama ya mshitaki huyu inafanya kazi saa ishirini na nne, .
Mtu hawezi kufungwa mpaka kuwepo na mashitaka, kwa kawaida mtu anapokamatwa na polisi huwekwa mahabusu, halafu polisi huandaa hati ya mashitaka na mtu hupelekwa mahakamani, kwenye mahakama za juu hati ya mashitaka huandaliwa na mkurugenzi wa mashtaka (DPP).  Na hati zinaandaliwa ili mtu afungwe.
Sasa shetani ndiye mkurugenzi(wa rohoni) wa mashtaka.  Zaburi 109:6, Uweke mtu mkorofi juu yake, Mshitaki asimame mkono wake wa kuume’.  kuna washitaki wakorofi. 

Mashitaka dhidi ya Yesu, pilato alikuwa mgumu kushughulikia  swala hilo sababu hakukuwa na hati ya mashtaka. Matendo 25:27 "Kwa maana naona ni neno lisilo maana kumpeleka mfungwa, bila kuonyesha mashitaka yale aliyoshitakiwa".  

Mtu hawezi kufungwa isipokuwa ameshtakiwa. 
Hakuna gereza analoweza kuingia mtu bila mashitaka.  Polisi ni watekelezaji wa sheria, ukifanya kosa unakamatwa, na ofisi wa DPP inaandaa mashtaka, hivyo hata katika ulimwengu wa roho kuna idara kabisa ya kuandaa mashtaka na mtu hawezi kufungwa na magonjwa,umasikini au shida ya namna yoyote mpaka yawepo mashitaka.

Kisa cha kweli

Mwaka juzi shetani alinitokea na kuniambia kwa kuwa tumeshampiga sana, basi sasa kila mtu achukue nyaraka zake twende mahakamani, mim nikawaza mahakama gani anayozungumzia..? kama ni ya Mungu, Mungu ni baba yangu na anakaa ndani yangu.. pia nikagundua unapoenda na shetani mahakamani lazima uwe makini la sivyo utaweza kuishia jela.
  
Kolosai 2:3-14 "akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;  akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;"

Yesu alipokuwa msalabani pia alifuta hati za mashtaka kulingana na hukumu zake Yesu!
 Iko hivi mfano Mungu amesema mshahara wa dhambi ni mauti, sasa wewe unapotenda dhambi mashetani wanaandika na wanaangalia kwenye sheria za Mungu wako wanaangalia mfano umezini, wanaenda mbele za Mungu na kushitaki kuwa huyu amezini na wewe umesema mshahara wa dhambi ni mauti tunaomba tukaitimize hiyo sheria.

Mungu akikaa kimya wanajua ndo imekubalika, mashambulizi yanaanza.  Mungu aliwahi kunionyesha jinsi mashetani yanavyoshtaki…
Shetani ni mkurugenzi wa mashtaka, mapepo ni watekelezaji wa hayo mashtaka.  Biblia inasema Mungu si mwepesi wa hasira, ila pia hawezi kumwacha mtenda dhambi bila adhabu.  

Yesu alipokuwa duniani aliletewa mwanamke aliyekuwa akizini, na wakamwambia kwa taratibu za kiyahudi huyu mtu anatakiwa apondwe mawe hadi kifo.  Yesu hakuwakatalia ila akawaambia ambaye hana dhambi awe wa kwanza kumponda mawe, wale mafarisayo wakaondoka mmoja mmoja ndipo Yesu akamwambia Yule mwanamke washtaki wako wako wapi? Kama wameondoka basi na mimi siwezi kukushitaki enenda kwa amani.

Kwa hiyo kilichomponya yule mwanamke ni wale washitaki wake kuondoka.  Washitaki ndio chanzo cha tatizo.  Hivyo hata wewe kwa jinsi unavyokuwa na washitaki wengi ndivyo kwa jinsi hiyo hiyo matatizo makubwa yatakavyokupata, kwasababu wana tabia ya kuweka kumbukumbu

Kuna idara maalum ya kumbukumbu, ambayo wanapotaka kukushughulikia wanayachukua na kuyapeleka kwa Mungu!  Yaani hiyo ni idara ambayo inasimamiwa na mapepo maalum wanatunza toka makosa ya mababu zako.  Hakuna gereza bila mashitaka.

‘Kwa jina la Yesu leo napiga watunza kumbukumbu wote, kwa jina la Yesu’

Kuna wengine wamefungwa toka tumboni kutokana na madhambi ya mababu na mabibi zao!  Mfano bibi  alikuwa mchawi, wanachofanya mapepo wanakwenda mbele za Bwana na kutoa mashtaka kuhusu familia yako.  Wanamwambia kwa kuwa bibi yake alikuwa mchawi na aliwazuia wengi kuolewa na huyu haturuhusu kumzuia kuolewa, Mungu akinyamaza tayari ndo tiketi ya wao kukuvuruga.  Mungu hawezi kukuadhibu ila mashetani ndo hutunza kumbukumbu na kwenda kukushtaki mbele za Bwana kwa kutumia sheria za Mungu.  Ndio mana inatokea mtu yanampata mabaya wakati hakutenda kosa lolote
"Kwa jina la Yesu, nashambulia watunza kumbukumbu wote wanaotunza kumbukumbu za familia yangu na ukoo wangu"

Post a Comment

0 Comments