Sunday, May 11, 2014

SOMO: VITA VYA HALI


Na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima 11th May 2014 , Sunday
  
 Zaburi 27:1-14, Vita vya hali ni somo linaloendana na somo la matukio ya kichawi 

Ayubu1:19-24, Kuna vita vya hali kwa mfano mtu anaweza kusikia uchungu, au hali ya hewa na mazingira kwa mfano watoto wa Ayubu waliuawa na hali ya hewa ya upepo mkali . Ibilisi aliporuhusiwa na Mungu kugusa maisha ya Ayubu na tukio mojawapo alilolitenda ni kuanza kuleta hali mbalimbali ili kusudi watu wajue kuwa ni matukio ya hali ya hewa, shetani alileta upepo tokea pande nne ukaipiga nyumba na watoto wa Ayubu wakafa. Rusifa anasababisha hali ikiwa ni mojawapo ya silaha za kuwashambulia watu. Leo tunataka tushindane na vita ya hali kwa jina la Yesu, Wanadamu wengi hawajui kuwa shetani anatumia hali ya kushambulia maisha yao, kwa mfano hali ya moto, mvua kali, upepo , hali ya mtu kujisikia Uchungu, hali ya kukosa amani nguvu nakadhalika.

Leo tunatangaza kila silaha ya kukosa amani , kila silaha ya woga na kila silaha ya hali itakayofanyika juu yako wewe haitafanikiwa kwa jina la Yesu.  Kwa mfano tulipokuwa Ubungo kila siku nikitaka kuhubiri wingu linatanda na mvua inanyesha na mimi mhubiri nalowana  na baada ya kugundua kuwa ni hali ya vita  kwa hiyo nikaanza kufunga anga kabla ya kuanza ibada.
Kuna matukio yanatangazwa kwenye vyombo vya habari kama maafa ama majanga ambayo yametukia kutokana na hali mbalimbali lakini watu wanapokea taarifa hizo bila kujua kuwa ni matukio ya kichawi yanayoletwa na hali.

Kuna hali ya kuharibika biashara yako iliyotengenezwa, hali ya kuachwa, hali ya kuumwa na hali mbalimbali zinazotengenezwa kinyume na maisha ya mtu. Leo tunaenda kushindana kwa maana imeandikwa kwa maana kushindana kwetu siyo juu ya damu na nyama bali juu ya falme mamlaka wakuu wa giza na majeshi ya pepo wachafu. Je hayo mafuriko ni kawaida, siyo  hiyo ni vita vya hali ya hewa ya mvua, maana imeandikwa katika ufunuo  “joka akafunua mdomo na mto ukatoka ili kumgarikisha mtu, unaona joka alitoa mto , kumbe shetani anaweza kutoa mto na kugharikisha watu.  Kwa hiyo mtu anaweza kutengenezewa hali ya hewa ya joto na akawasha AC mpaka akachoka lakini joto liko palepale.

Kumbe shetani anaweza kunyoosha mkono wake na hali fulani ikampata mtu, kwa mfano mtu anaweza kutengenezewa hali ya kutokutulia mpaka ukimwuliza hawezi hata kuelezea hali yake.  Utaona shetani alitengeneza moto ukatoka mbinguni na kuteketeza kundi la wanyama wa Ayubu.


Freemasons ni wakala wa shetani na wamepewa uwezo wa kutengeneza hali mbalimbali  juu ya mtu kwa mfano  wanakuwa na makongamano ya kuzibadilisha fikra za watu hii ina maana wanatengeneza hali fulani ndani  mtu  ili aamini kuwa mafanikio yanaweza kuja  bila uwezo wa Mungu. Watu wanaingizwa kwenye freemonson society kwa kuvutwa na wenzao ,kwa kukaribishwa na kuambiwa maneno ya kutiwa moyo, kupewa zawadi na kusaidiana kumbe huo ni mtego. Utasikia mtu anaambiwa kuwa kuna Society inayoitwa Global Brotherhood inayosaidia watu kubadilisha mtazamo na fikra za mtu kuelekea mafanikio makubwa. Hakuna kitu hapa duniani kinachoweza kutokea chenyewe. Na duniani kuna makundi ya watu watatu:
      I.            kundi la kwanza wasiojua kinachoendelea na  watu hawa ni kundi kubwa na wanaweza kuitwa wapumbavu/ wajinga .
         II.            kundi la pili ni wale wanaojua kinachoendelea  lakini hawajui  jinsi ya kutenda kwenye hilo wanalojua.
     III.            Kundi la tatu ni wale wanaojua kinachoendelea na wanajua la kutenda kwenye hilo ninaloendelea hawa ni wachache sana na wanaitwa wenye hekima/akili.

Uchawi una makundi matatu
·         Black magic – hawa ni wachawi wanaoruka na kula nyama za watu na uchawi huu ufanyika kwa siri.
·         White magic -- uchawi uliokubalika na jamii na ukitendwa watu wanaona hauna madhara mfano wanamazingaombwe
·         Black Science - wanaweza kutengeneza virusi  vya magonjwa na wakatupa kwa watu, wanaweza kutengeneza hali ya hewa fulani mfano matetemeko, mvua kubwa nk.
Vifaa hizi vya hali ya hewa vinatengenezwa sehemu mbalimbali hata wajapani wengi wanatengeneza vifaa hivyo. Hata kwenye biblia utaona Musa alipoyapiga maji kwa fimbo yake ukatokea upepo mkali na bahari ikagawanyika , hiyo ulikuwa silaha ya hali.  Leo nakutangazia kwa jina la Yesu kuwa hakuna silaha ya hali ambayo itafanyika juu yako na kufanikiwa kwa jina la Yesu.

Black science ni watu waliochukuliwa msukuleni na huko wanakutana na mashetani na wanaanza kuwafundisha technologia ya kuonekana kwa macho na  hali ya hewa ni mojawapo ya hizo technologia.kwa mfao Japani wametengeneza Train inayokwenda underground kwa kasi sana 500km kwa saa na haina dereva inaendeshwa electronically , lakini ukiwauliza mmetoa wapi hii technologia hawajui ilikotokea , lakini hii inaonyesha kuwa mpinga Kristo analeta technologia hizi kuuleta ulimwengu pamoja ili aweze kutawala vizuri wakati wake ukifika.

Hali mbalimbali zinaweza kutengenezwa kwa mfano ndege kubwa yenye watu mia nne ikapotea kabisa , utajiuliza imekwenda wapi? Hii ni hali imetengenezwa na ndege  ikachukuliwa  na kuyeyushwa kabisa, hii inadhibitisha kuwa ufalme wa giza unatenda kazi nyuma ya matukio. Nyakati hizi ni za kuwa makini sana kwa maana shetani anatembea katikati ya watu na anajiungamanisha na wanadamu. Kila mtu mchana wa leo aliyetengenezewa hali fulani kwa mfano hali ya ugonjwa, hali ya umasikini, hali ya kukataliwa nk na mtu ametulia na kuridhika leo nakutangazia kuwa Mungu anataka utoke kwenye hali hiyo kwa jina la Yesu. Kuna watu wengine wametengenezewa hali ya kutojikubali , mtu anajisikia unyonge kila wakati mpaka anaogopa kuwa kati kati ya watu wengine.
 
MAOMBI
Kwa jina la Yesu hali niliyowekewa ya kukataa ndoa, hali ya kuogopa, hali ya kujikataa, hali ya kuwashwa naikataa kwa jina la Yesu, nami leo navaa hali ya ujasiri na kuzishambulia hali za kishetani zinazonisumbua  kwa jina la Yesu. Nawasha moto na kuteketeza hali ya maumivu inayonisumbua, hali ya kukosa usingizi na hofu wakati wa usiku , hali ya kujiona mnyonge na kujiona sifai, nayaamuru mapepo yanayohusika na hali hizo yang’oke na kuniachia  kwa jina la Yesu.

Katika jina la Yesu kuanzia sasa nasimama kinyume na hali  yoyote ya kishetani  iliyonipata, nasimama kinyume na silaha ya hali iliyonipata kwa jina la Yesu. Nasambaratisha hali ya aibu iliyonipata, hali ya kupata hasara kwenye biashara, hali ya ugonjwa na udhaifu kwa jina la Yesu. Nakataa hali ya umasikini, hali ya unyonge, hali ya kuonewa, hali ya magonjwa, hali ya aibu, hali ya kushindwa kwa jina la Yesu. Nawasambaratisha mashetani wote wanaonifuatilia na kuniletea hali mbaya kwenye maisha yangu kwa jina la Yesu. Imeandikwa kila silaha itakayofanyika juu yangu haitofanikiwa, naamuru silaha zote za kuniletea hali mbaya zivunjike kwa jina la YESU. Imeandikwa kila pando asilopanda baba yangu wa mbinguni litang’olewa, nang’oa hali ya huzuni mliyonipandia, nang’oa hali ya uchungu mlionipandia kwa jina la Yesu. Enyi mashetani mnaovaa sura za watu na sura za hali mbalimbali  na kuja kunitesa leo nawaamuru kudhihirika  na kutoweka kabisa kwenye maisha yangu kwa jina la Yesu.
 **********************************AMEN************************************
                .
.

No comments:

Post a Comment