Sunday, May 18, 2014

SOMO: MADHABAHU YA UHARIBIFU

Na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima, 18 Mei 2014.

1. 0 Utangulizi

Maandiko ya Msingi: Zaburi 18: 1-50, Waamuzi 6:1-40, 

Kipindi ambacho Taifa la Israel walipokuwa watumwa wa wamidian, watu walikuwa wanaonewa sana na kunyang’anywa mali zao hata mazao yao yalikuwa yakiharibiwa. Hivyo Gidion alikuwa amejificha kwenye mwamba akipepeta ngano ndipo malaika akamwita ewe shujaa Gidion,,lakini Gidion alikataa kuitwa shujaa kwa maaana alikuwa hajiamini. Lakini malaika akamhakikishia kuwa yeye ni shujaa ila ile madhabahu ya Baali aliyokuwa nayo baba yake ndiyo iliyokuwa inamshikilia hata asijitambue kuwa ni shujaa. Hii inatufundisha kuwa kuna madhabahu mahali ambayo inakuzuia wewe usifanikiwe kama Mungu alivyokusudia kwako.

Kwenye madhabahu ile ya nyumbani kwao Gidion kulikuwapo na ashera pia, ashera ni mti uliopandwa kwa ajili ya kusimamia kitu fulani , kwa mfano mti unaweza kupandwa kwa jina la mtu na ule mti ukistawi ndipo mtu Yule anapata matatizo mfano ugonjwa ndiyo maana kuna mtu anakuwa mgonjwa wakati wa masika hii ni kwa sababu ya ule mti unakuwa umenawili kwa mvua. Kuna mtu yuko mahali hapa na watu wasiompenda wamempandia mti eidha wa balaa, magonjwa, umasikini, kukataliwa, kuachwa na kadhalika, lakini leo tunatuma radi na kulipua maashera yote kwa jina la Yesu.

Kwa hiyo Gidion akaambiwa na bwana wewe ni shujaa unatakiwa kwenda kupigana vita ila kwanza bomoa madhabahu iliyo kwenye mji huu inayofanya watu kuwa waoga. Na sisi leo watu wa Ufufuo na Uzima tunaenda kila mahali ilipo madhabahu inayolishikilia Taifa letu na tunaibomoa kwa jina la Yesu. Leo lazima watu wote waliolazwa kwenye madhabahu ya nchi hii watatoka na kuelekea  katika hatima zao na mafanikio yao kwa jina la Yesu.  Gidion baada ya kuibomoa madhabahu ya Baali  watu wa mji walimtafuta ili wamwuue lakini baba yake Gidion (Yoashi) akasema mwacheni baali ajitetee mwenyewe kwa kubomolewa madhabahu yake, kwa hiyo nakutangazia hata wewe leo hakuna dhara hata moja litakalokupata kwa kuzibomoa madhabahu za wachawi .

2.0 MADHABAHU NDANI YA BIBLIA

Mwanzo 8:20, Nuhu alipotoka kwenye safina akamjengea Mungu madhabahu, Hii inaonyesha kuwa kila madhabahu lazima iwe na tukio inaloliwakilisha, kwa mfano kuna madhabahu za utawala, kwa hiyo huwezi kumwondoa mtawala aliye na madhabahu imara mpaka uibomoe ile madhabahu ndipo uguse utawala wake.  Mwanzo 12:7, Ibrahim alipoongea na bwana kwamba nchi ile amepewa ndipo alipojenga madhabahu mahali pale ili isimamie umiliki wake aliopewa kwenye  ile nchi, ndiyo maana hata sasa hakuna mtu anayeweza kuwanyang’anya wa Israel nchi yao ingawa mataifa mengi wamejaribu kuwaondoa lakini wameshindwa. Mwanzo 12:8, 13:14, Utaona watu kwenye biblia walikuwa wakijenga madhabahu mahali ili  isimamie jambo fulani.

Madhabahu ni mahali ambapo wachawi na waganga wa kienyeji  wanakusanyikia , wanapokuwa mahali pale wanatoa kafara za damu na wanakuja na mashitaka ya kuwashitaki watu na wananza kujadili. Kwa hiyo mchawi mmoja anapeleka shitaka la kumshitaki mtu kwa mfano atasema simpendi fulani kwa sababu analinga eti anahela ,au ana watoto wasomi au anapendwa sana na watu hivyo  nataka tumkomeshe. Kwa hiyo wachawi wanasema sawa tutamkomesha na ndipo wanapoanza kumtumia mtu mashetani ya kumharibia maisha yake.  Lakini leo nakutangazia kuwa madhabahu zote zilizotesa maisha yako lazima zibomolewe kwa jina la Yesu.  Ninayo ndoto  na ndoto yangu ni kuwa Falme za dunia zimekuwa Falme za mwanakondoo na hii imeishakuwa kwa maana madhabahu za kichawi zilizozuia injili ya Yesu zitabomolewa zote kwa jina la Yesu.

Mchawi anapenda kumshambulia na kumwuua mtu wa karibu yake kwa mfano kaka, dada, mama, baba nakadhalika. Kwa mfano mtu anataka dada fulani asiolewe kabisa, anapeleka jina lake kwenye madhabahu na kumwaga kafara, kwa hiyo kuanzia pale yule dada hawezi kuolewa kabisa kwa maana madhabahu inakuwa inaongea fulani asiolewe, asiolewe. Mwingine anaweza kuwekwa kwenye madhabahu ya uoga, kwa hiyo hawezi kufanya lolote kwa kuogopa eidha hasara kama ni biashara, ajali kama ni safari, kuachwa kama ni ndoa nakadhalika.

Madhabahu inaweza kuwa kakiwanja fulani ambapo wachawi wanakutanikia na kutoa kafara za damu kwa miungu wao. Mtu anaposhitakiwa na jina lake kutajwa mahali pale ndipo mashetani yanaanza kumwandama na kumharibia mambo yake, kwa hiyo mtu yule hawezi kufanikiwa hata afanyeje mpaka atakapoibomoa ile madhabahu. Madhabahu zinapobomolewa watu wanaachiliwa kwa hiyo wachawi na waganga wa kienyeji wanapata hasara, ndiyo maana Gidion alitafutwa auawe kwa kuibomoa madhabahu ya baali iliyokuwa nyumbani kwa baba yake Yoashi. Leo tutabomoa madhabahu iliyokutesa na kuwalaza  kwenye hiyo madhabahu wale waliokuwa wamekulaza kwa jina la Yesu.

Madhabahu /kiwanja cha wachawi huwezi kukiona kwa macho lakini kipo na wachawi wanakutana pale kila usiku na kuwashitaki watu. Ndiyo maana utaona watu wengi wana matatizo yasiyoisha, kwa mfano kuna mtu amelazwa kwenye madhabahu ya kuachwa kwenye ndoa kwa hiyo utamwona mama ameshaolewa na wanaume watatu nakuachwa na wote bila sababu ya msingi.

Mungu anapotaka kumwinua mtu anaruhusu apitie mambo magumu sana kila upande na asione msaada. Ndipo sasa mtu anapoona hana msaada anakumbuka kumlilia Mungu. Kwa mfano Israel walipokuwa na njaa kali sana mpaka watu wamefikia hatua ya  kula watoto wao, ndipo Mfalme akasema mwambie nabii Elisha kesho saa saba atakatwa kichwa asipotabiri kwa habari ya njaa kwenye taifa la Israel. Baada ya kutishwa ndipo nabii Elisha alitoa unabii kwamba kesho chakula kitapatikana tena kwa bei nafuu sana kuliko hata kabla ya njaa kutokeaa na  kesho yake yakatokea kama vile Elisha alivyosema. Hii inafundisha kuwa mtu unapopata matatizo usianze kulia wala kuwalaumu watu bali wakati huo ni wakatiwa kuutafuta uso wa Mungu ili upate jibu la kukutoa mahali pale.  Usifikiri magumu yanayokupata Mungu amekuacha siyo ni kwamba Mungu anataka uanze kumlilia na kumtafuta yeye kwa moyo wako wote kwa maana aliona umeanza kwenda mbali naye.
Kwa hiyo kuna madhabahu ambayo inaweza kuwa imemshikilia mtu mfano mtu anaweza kuwa amelazwa kwenye madhabahu ya umasikini hata akisoma na kusafiri nchi zote duniani hawezi kufanikiwa. Kwa hiyo ili mtu huyo afanikiwa lazima aibomoea ile madhabahu. Leo kila mtu ataomba kulingana na udhaifu alio nao kwenye maisha yake kwa mfano mtu mwenye hofu ataomba akisema kwa jina la Yesu naibomoa  madhabahu ya hofu iliyonishikilia na kuiharibu kafara waliyoitoa kwenye hiyo madhabahu.   Kwa jina la Yesu leo naamuka na kuondoka kwenye madhabhu walioyonilaza kwa jina la Yesu. Na mtu yeyote aliyepeleka jina langu kwenye madhabahu  hiyo namponda kwa jina la Yesu.

Wakati mwingine madhabahu inaweza kuwa siyo kiwanja bali inakuwa kwenye kitu chochote kile, kwa mfano dada mmoja alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya tajiri, siku moja yule dada akaingia kwenye ofisi ya boss wake na kuona chupa ndogo lakini ndani ya ile chupa yumo yule dada akiwa hai. Hii inatufundisha kuwa yule dada alikuwa amelazwa kwenye madhabahu ya yule tajiri , kwa hiyo mafanikio aliyonayo yule tajiri ni kupitia nyota ya yule dada. 

3.0 MAMLAKA TULIYOPEWA NA BWANA WETU YESU KRISTO
Mathayo 10:1, kwa hiyo watu wa Mungu tumepewa mamlaka ya kutamka na ikawa na leo tunaenda kuzibomoa madhabahu zote kwa jina la Yesu. Mambo hapa dunia hayatokei yenyewe ila kuna kitu  kinafanywa ili yatokee. Na nguvu ya kufanya mambo yatokee ni uwezo wa mtu wa Rohoni  alionao ndiyo unaleta matokeo mazuri ya mwilini. Kwenye ulimwengu wa Roho unapotamka kwamba navunja madhabahu iliyonishikilia mahali popote itakuwa kama utakanyotamka.

4.0 HITIMISHO
4.1 MAOMBI
Kwa damu ya mwanakondoo naibomoa madhabahu ya wachawi kwa jina la Yesu, mahali popote walipotaja jina langu napaharibu kwa jina la Yesu, Naibomoa hali ya  kuwa kichaa, naibomoa madhabahu ya wendawazimu,naibomoa madhabahu ya mikosi kwa jina la Yesu. Mtu yeyote aliyenilaza kwenye madhabahu yake ya utawala leo naondoka na nakataa kubaki pale kwa jina la Yesu na nyota yangu naimuru ianze kung’aa.

Nakataa watoto wangu , kazi yangu, ukoo wangu kuwekwa kwenye madhabahu ya wachawi kwa jina la Yesu. Naibomoa madhabahu ya kifo, umasikini,uoga na mikosi kwa jina la Yesu. Imeandikwa Gidion aliwapeleka watumishi wake kumi wakaibomoa madhabahu ya baali, na sisi watumishi wa Mungu leo tunazibomoa madhabahu zote zilizoshikilia taifa letu na watu  kwa jina la Yesu.  Imeandikwa bomoeni bomoeni hadi msingini, leo nabomoa madhabahu zote, madhabahu ya dhiki, magonjwa, umasikini kwa jina la Yesu. Nabomoa madhabahu ya shaba, udongo, chuma ,mti kwa jina la Yesu. Nakataa kushikiliwa kwa jina la Yesu, mtu yeyote anayenicontrol kupitia madhabahu yoyote leo nakaataa kwa jina la Yesu. Madhabahu ya mabaya iliyoimarishwa naivunja kwa jina la Yesu, mabaya hayatanipata mimi. Naamuru mizimu, majini, majoka anza kuondoka kwa maana madhabahu zenu zimebomolewa kwa jina la Yesu.  Imeandikwa bwana amenifunga mshipi wa vita,  leo nafanya vita na kuziteketeza madhabahu zote na nawachinja makuhani wote wa hizo madhabahu.

Naivunja madhabahu inayoninyima promosheni,inayonizuia nisisafari, inayonizuia nizipate pesa kwa jina la Yesu,.  Na kuhani yeyote aliyenipeleka kwenye hizo madhabahu leo namchinja . Imeandikwa bomoeni bomoeni hadi msingi leo naenda kubomoa madhabahu za njia panda, porini, bahari . Nainyamazisha damu iliyomwagwa kwenye madhabahu za wachawi kwa damu ya Yesu. Ninaamuru kuanzia sasa kila madhabahu inayonena nainyamazisha kwa jina la Yesu. Kila madhabahu iliyojengwa kwenye nchi ya Tanzania ili kukamata akili na nia za watanzania leo nakupasua vipanda vipande kwa jina la Yesu. Naamru na roho zote zilizolazwa kwenye madhabahu zianzae kuamka kwa jina la Yesu. Nakata kamba zote zinazounganisha watu na madhabahu za wachawi kwa jina la Yesu.

Nakata ashera zote zilizopandwa kwa majina ya watu kwa jina la Yesu. Nazilaani ashera zote na kuanzia sasa zianze kukauka kwa jinala Yesu. Nawateka nyara wasimamizi na makuhani wa madhabahu  nawachinja kwa jina la Yesu. Ewe Mungu wa madhabahu nakukamata na kukuteketeza kabisa na enzi yako yote kwa jina la Yesu. Leo naamuru mioyo, nafsi, akili na vyote vilivyoshikiliwa kuachiliwa kwa jina la Yesu. Nauzima moto uliwashwa kwenye madhabahu ya wachawi ili watu wapate magonjwa, kichaa, umasikini , balaa na mikosi kwa jina la Yesu. Naibomoa madhabahu iliyojengwa kwenye kichwa, tumbo, kifua  kwa jina la Yesu. Naibomoa madhabahu iliyohai na inayotembea kwa jina la Yesu.

Ufunuo 6:9, kuna roho za watu zinaweza kuwa zimewekwa chini ya madhabahu.  Hata wewe leo unaweza kuwa hapa lakini roho yako imelazwa kwenye madhabahu, sema leo naivunja madhabahu iliyonilaza na toka kwa jina la Yesu. Wachawi wa familia wanaweza kumwuuza mtu na kumpeleka alazwe kwenye madhabahu.  Leo naiteketeza hati ya makubaliano yao ambayo imewekwa kwa jina la Yesu, hati iliyonifanya niuzwe na nibaki madhabahuni leo naichana na kuiteketeza kabisa kwa kwa jina la Yesu.