Sunday, July 13, 2014

MASHIMO YA KICHAWI YAFUKIWA NA KUSAWAZISHWA KATIKA BONDE LA KUKATA MANENO KAWE.JUMAPILI YA TAREHE 13/07/2014MCHUNGAJI KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA
SOMO: MASHIMO YA KIROHO/KICHAWI
I.                    Utangulizi
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima
Kuna ulimwengu wa aina mbili ; ulimwengu unaoonekana kwa macho na ulimwengu usio onekana kwa macho. Kwanini unaitwa ulimwengu wa roho kwasababu unakaa rohoni na pia kila kinachokaa kule ni roho mfano gari, mtu, mti, nyumba ni roho zinazogeuka kuwa vitu na watu wengi wanaupata kupitia ndoto na ukitaka kwenda kule ni mpaka uwe rohoni na vitu vingi vinaanzia rohoni na uwezo wako wa kushindana kwenye ulimwengu waroho ndio uwezekano wako wa kupokea Baraka za mwili. Wakristo wengi hawatambui taifa linaweza kushikiliwa rohoni, uso wa mtu unaweza kushikiliwa rohoni hata nyumba inaweza kushikiliwa rohoni.
II.                  SOMO.
Waefeso1:33 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; 20 aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 
Waefeso2: 2 ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; 6 Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;   
Waefeso3: 10 ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho;     
Waefeso6: 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 
Akitolewa shimoni
Zamani kwenye agano la kale kulikuwa na  mashimo walikuwa hawana magereza kama ya leo bali yalikuwa ni mashimo marefu sana na ulipokuwa unafanya kosa unatupwa shimoni na kuna aina nyingine ya mashimo ambayo yalikuwa yanawekwa wanyama kama danieli alivyotupiwa kwenye tundu la Simba, na mashimo mengine yalikuwa yana maji na ndio maana ya lile andiko watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa wamefichwa mashimoni wala hapana aokoaye wamekuwa mateka wala hapana  asemaye rudisha. Lakini kwenye agano jipya hakuna mashimo kama hayo bali kuna mashimo ya kiroho ya kichawi ambayo yamejengwa kwenye ulimwengu wa kiroho na wachawi ili kuwaweka watu na ndio maana yesu alipokuja duniani alisema roho wa Bwana yu juu yangu amenitia mafuta niwatangazie wafungwa kufunguliwa kwao.
Ufunuo9: 1 Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu. 
2 Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni. 
Shimo la kuzimu ndio makao makuu ya shetani ni shimo mama lipo kwenye ulimwengu wa rohoni ni refu lisilo onekana linaitwa kuzimu linaitwa shimo la uharibifu, shimo la kifo na hata mashetani walipoasi walitupwa kwenye shimo hilo 2petro2: 2 Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. 
 na hilo shimo ndilo shimo wenye hekima za utawala wanakwenda kuchukua kule au umaarufu wa utawala au nuru ya utawala na sisi tuliookolewa tunapahali petu tunapata ambapo ni Mbinguni juu.  Ndio maana Yesu alisema amelijenga kanisa juu ya mwamba na milango ya kuzimu haita lishinda.
Luka 8: 26 Wakafika pwani ya nchi ya Wagerasi, inayoelekea Galilaya. 
27 Naye aliposhuka pwani, alikutana na mtu mmoja wa mji ule, mwenye pepo, hakuvaa nguo siku nyingi, wala hakukaa nyumbani, ila makaburini. 
28 Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese. 
29 Kwa kuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke mtu yule. Maana amepagawa naye mara nyingi, hata alilindwa kifungoni na kufungwa minyororo na pingu; akavikata vile vifungo, akakimbizwa jangwani kwa nguvu za yule pepo. 
30 Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia. 
31 Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni. 
Miji inaweza kuwa na mashimo ya rohoni na utakaposhughulika na shimo hilo unauteka mji. Mashetani yanamwambia Yesu tunaomba usitupeleke shimoni kwahiyo kila mji kuna mashimo ya kichawi na kuna makao makuu ya utawala wa kishetani matatu nayo ni 1. Shimo la kwanza kubwa la mashetani ni katika nchi “Ufunuo12: 7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 
8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 
9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. ” 2. Katika maji mnyama anapeenme mbili anatokea baharini [pembe ya kwanza ni utawala wa kidini na utawala wa kishetani mwana kondoo maana yake anaonekana mwema] 3. Angani Belzebuli mama wa makahaba anayerutubisha uovu kwa uasherati.
Kuna vishimo vidogovidogo kwenye nchi na unapoona mtu amefariki unasema ameitwa na Bwana kumbe amewekwa mule ndani. Mashimo haya ya kichawi ni kitu gani hasa?. Tulishawahi kujifunza shetani anaweza kuvaa umbo la mtu, malaika walienda kwa Abrahamu wakala wakaongea.  
 Mashetani ni malaika waovu ndio maana kwenye biblia imeaandikwa kuzimu na mauti itawatoa watu wake na ni shimo lisilo na kina na wasiookolewa wote huenda huko.
Mtu ni roho inayokaa ndani ya nyumba inayoitwa mwili  na wanapouzika mwili wanakuwa wameuzika mwili pekee lakini mwenyewe hayupo pale tena.
Luka16: 19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. 
20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, 
21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. 
22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. 
Mtu anapo kufa anachukuliwa na malaika na anatoka ndani ya mwili anapelekwa kwenye shimo la umilele anasubiri siku ya mwisho atupwe kwenye moto ”na walio kuzimu wanatoka” ila jehanum ndio hawatoki. Sasa unapokuwa umelala unakuwa umechukuliwa na wachawi na kupelekwa shimoni na hata mikono inaweza ikachukuliwa, na ndio maana mtu anapokuwa rohoni analishwa chakula cha kiroho mfano Elia alilishwa mkate na malaika akala akaenda.
Kuna chakula cha rohoni na Neno la Mungu nalo ni chakula cha roho na wachawi nao wanachakula chao Danieli1:7- chakula kimenuiziwa mpaka kimejaa nguvu za rohoni upande wa shetani ndio maana watu wanaota wanakula chakula usiku kimenuiziwa magonjwa, balaa, mikosi, utasa nk. Pia kuna namna ya rohoni uso wako unaondolewa, akili inaondolewa inafichwa kwenye mashimo lakini ukiwa duniani unaanza kuona mara magonjwa ya moyo mara kukataliwa “katika jina la Yesu leo nina amuru ikiwa mimi mwenyewe nimewekwa kwenye shimo ninaamuru leo ninahama kwa jina la Yesu.”
Kwanini wachawi wanamchukua mtu na kumweka kwenye mashimo ni kwasababu unakuta mtu mafanikio yake yamewekwa kwenye uso wake na wachawi wanaweza wakauchukua uso wakaenda kuutumia na mwingine.  wanaweza wakaichukua akili nayo na kuitumia.
Mhubiri9: 11 Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote. 
Kila mtu ana eneo lake la baraka mwingine amewekewa kwenye kinywa wengine kwenye matumbo yao wengine kwenye muonekano na ndio maana wale wenye Baraka zao kwenye uzazi unakuta wanapatwa na shida kwenye kuolewa na hiyo ni kazi ya wachawi wanachukua nyota za biashara na shetani ni mwizi na kazi yake ndio hiyo ya kuiba “sema kwa damu ya Yesu mahala popote walipoweka tumbo la uzazi, macho yangu, kinywa changu, akili yangu au chochoto kwenye mashimo kwa damu ya Yesu mashimo yote yaliyowekwa na familia yangu mashimo yaliyowekwa akili yangu napiga mashimo kwa jina la Yesu naamuru kuanzia sasa akili yangu njoo kwa jina la Yesu.
Ukimwona mtu anamatatizo sana na umekaa naye unazungumza nae kumbe ameshachukuliwa ama amechukuliwa kitu ndani yake uso, mikono, miguu Isaya42:22
Luka4:1-
Hakika Mungu ni mwema
Shetani anamwambia Yesu atampa mali ila masharti yake amsujudu lakini zaburi24 vitu vyote viijazavyo nchi ni mali ya Bwana. Sasa shetani na wachawi wanauwezo wa kuona Baraka na kusudi watu walilowekewa na Mungu ili watumie kufanikiwa na wachawi wanachukua akili za watu na kwenda kumpa mtu mwingine. Mungu anawapa watu vitu mbali mbali na tangu ukiwa mtoto mdogo wanakuja wanakuibia na kuviweka shimoni na kumpa mtu mwingine, unakuta mtu anatabia mbaya lakini anaolewa lakini wewe unatabia nzuri hauolewi kumbe umeibiwa uso wako Mungu ni Mungu wa kurudisha aliwarudisha waisraeli toka utumwani misri na ndiomaana anasema nitakurudishia afya yako, na anaweza kukurudishia afya yako tena, familia yako, bihashara yako. Mungu ni muumbaji na shetan ni mwizi.
Watu wanaofanikiwa wanasiasa, wenye magari hawana Mungu wana mganga wake wa kienyeji. Na kuna watu wanaenda kwa mganga na kumwambia wanataka uongozi na mganga anamwambia njoo kesho na mganga huyu anatoka usiku anakwenda anazunguka anamkuta mtu haombi ana nyota ya uongozi anaichukua nyota hiyo, anatoka anaenda kwa mwingine kuchukua nyota ya kupendwa, anatoka anakwenda kwa mwingine anachukua nyota ya kuongea. Sasa wale waliochukuliwa nyota zao wanaamka hawajui chochote. Unakuta mtu anamatatizo anatamani kufanya biashara lakini hawezi kuisimamia akafanikiwa kumbe wamechukua akili ya bihashara wameficha kwenye mashimo na unamwona mwingine anafanikiwa na hamtumikii Mungu kumbe amepata toka shimoni. sema kwa jina la Yesu kuanzia sasa shimo lolote lenye nyota yangu rudisha kwa jina la yesu.
Makaburini zimelala hazina nyingi ambazo hazijafanyika hapa duniani na hatari kubwa kuliko yote katika maisha ni kufa kabla hujatumia kipaji ulichopewa na Mungu na elimu ni nzuri na ni ya lazima lakini haikuhakikishii mafanikio bali ni taa inayo kusaidia upate kutumia kipaji ulichopewa na Mungu. Kanisani ni center ya walioteswa ni sehemu ya kuwa huru kwa walioonewa. Kuna namna ambayo Mungu anataka uwe na wachawi nao wanaona vile unavyotakiwa kuwa na wanavichukua na unatakiwa uwe mtu wa kupigana kwamaana kushindana kwetu si juu ya damu na nyama maana yake kuna mamlaka za kichawi falme za kichawi tunazotakiwa tupigane nazo ndizo zinazotusumbua. Kuna jambo ambalo wewe umezaliwa ili ulitimize na unapolitimiza jambo hilo na ukafa wewe ni mtu uliyefanikiwa kwa hiyo kuna mtu mwingine amefanikiwa nusu na unaweza usifanikiwe kumbe kuna wanaozuia. Katika jina la yesu hakuna atakaye zuia kila nilichokusudiwa nikifanye kabla sijafa kwa jina la Yesu.
Kwenye kitabu cha yeremia Yeremia anaambiwa na Mungu tangu tumboni nalikujua na kuna watu Mungu amewachagua wawe viongozi na unakuta mama tangu mimba ile imeanza inamatatizo tangu tumboni na unakuta umezaliwa na uunamatatizo lakini kuna jambo lilikuja katikati pale ndilo likaleta maisha uliyo nayo na usishukuru kile ulicho nacho ni mapenzi ya wakala wa kishetani ndio wamekufanya uwe hivyo. Ile akili ya bihashara yako inatumiwa na watu mahali fulani ndio maana shetani anamwambia Yesu nikupe mali lakini hana lolote anataka kuwaibia watu ili aje ampe yesu.
Pengine familia yako imeibiwa au kitu chochote utajuaje umeibiwa? Ndoto unazoziota au unakimbizwa maana yake mashetani yanakufuatilia au uko kwenye kichaka maana yake uko kwenye kichaka cha kishetani unapoota unafanya mapenzi na mtu maana yake unaushirika na mashetani unapoota umevunjika miguu maana yake kuna jambo litatokea upatwe na upofu na kila ndoto unayoota ni jinsi ulivyo rohoni unatakiwa uziharibu ndoto zote mbaya.
Mungu anaongea na watu kupitia ndoto na hakuna ndoto ambayo haina maana na kwenye kitabu cha hatari ya ndoto utakuta unatakiwa ufanye nini unapoota.
Na unatakiwa uchukue hatua na biblia inasema adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake na unakuta mtu ameibiwa nyota yake na mjomba lakini hajui unatakiwa uamue kwa jina la Yesu na utashangaa baada ya wiki moja au mbili utajiri wake unaporomoka wote na anabaki mtupu. Pia mwingine ameibiwa akili na inatokea anashindwa kusoma kwasababu wanajua atafanikiwa kupitia masomo. Pia ndoa nyingine zina baraka wale wanaowaonea wivu wanatengeneza jambo na ndoa yake inavurugika.
Maelfu ya watu wakipiga mashimo ya kichawi

III.                 MAOMBI.
Kwa jina la Yesu nayapiga mashimo ambayo yameweka uso wangu, nayateketeza kwa damu ya yesu mashimo ya kuzimu mashimo ya ukoo mashimo ya familia mashimo ya mashetani mashimo ya wachawi nayapiga kwa jina la yesu nayashambulia mashimo ya ukoo kila shimo lililochimbwa kwa ajili ya kuweka vutu vya ukoo  kila shimo lililohifadhi familia yangu nayapiga kwa jina la yesu kristo, nafanya vita na walinzi wa mashimo nawateketeza kwa moto wa Mungu. Shimo liloshikilia uso wangu nalipiga kwa jina la Yesu, nayashambulia kila mashimo ya kichawi kwa jina la yesu mashimo yote ya rohoni natetekeza kwa jina la yesu nashambulia shimo la kuzimu lililo meza akili zangu kwa jina la Yesu shimo lililoiba uso wangu naliamuru tapika kwa jina la Yesu shimo lililomeza mvuto wangu naamuru kwa jina la Yesu tapika.
Anza kuita chochote ambacho unaona kimeibiwa ita njooooooooooooo kwa jina la Yesu kila kilichofichwa kwenye mashimo njooooooooooooo kwa jina la Yesu, akili iliyofichwa kwenye mashimo njoooooooooooooo kwa jina la Yesu, elimu iliyofichwa njooooooooooooo kwa jina la Yesu, kinywa kilichoibiwa njooooooooooo kwa jina la Yesu, uso uliofichwa shimoni njooooooooooooooo kwa jina la Yesu, Baraka zilizofichwa kwenye mashimo njooooooooooooo kwa jina la Yesu, nafsi za wanadamu njoooooooooooooooooo kwa jina la Yesu kristo……………………………………………
                                         Amen!

1 comment:

  1. Katika jina la yes ninatoka shimoni elimu Yangu akili Yangu hatima Yang
    na kila hatima Mungu aliyeiachilia naamuru ianze kuonekana
    Nimetoka toka mashimo yote ya kichawi kwa jina la yesu
    Amen

    ReplyDelete