Thursday, August 7, 2014

MAOMBI YA NADHIRI

na PASTOR JOSEPHAT GWAJIMA

Mwanzo 28:16-22

“..Yakobo akaweka nadhiri..”
Yakobo alimuwekea Mungu nadhiri hapa, kwa mtu ambae yuko makini na mambo ya MUngu anaweza kuomba maombi haya, katika maombi yaha unamuomba Mungu na kumuambia Mungu akama utanifanyia hivi na mimi nitakufanyia hivi.
Yakobo alipokua safarini kwenda kwa Labani ndipo alipoiweka nadhiri hii na baada ya kupita miaka mingi akayaona yale ambayo alimuomba Mungu amtendee yameshatendeka karibu yote, ndipo Mungu akamtokea na kumkumbusha kuwa ndie Mungu yule aliyemtokea Betheli

Mwanzo 31:13

Mungu ni Mungu atimizaye nadhiri,  jina jingine la Mungu ni Mungu ashikaye maaagano (A covenant keeping God)
Ukiagana na Mungu hawezi kukuangusha katika maagano yenu kwasababu ni Mungu ashikaye maagano.
Ni kama unakubaliana na Mungu mkutane Mororogoro saa nane mchana, hata kama Mungu anajua kuwa hautafika Morogoro yeye atakuwepo mahali hapo kwasababu ni Mungu ashikaye maagano.
Nadhiri inaweza kukupandisha juu sana kama ukiwa mwaminifu lakini pia nadhiri inaweza ikakuharibu endapo huta itimiza, kwasababu nadhiri ina kawaida ya kupima moyo kwa kutumia dhamira ya Mungu.
Unapomuaambia Mungu ukinipa fedha nitakufanyia kitu fulani, Mungu anakupa na inapotokea ukashindwa kuitimiza unakua umeharibu kila kitu

Walawi 22:18

Hapa Mungu alikua anaonyesha wakati mwingine unaweza ukapitia maisha yenye misukosuko na kufikia hatua maombi yote unayoomba yanakua kana kwamba hayatendi kazi hapo ndipo wakati wa kutumia maombi ya nadhiri, na maombi hayo unapoyaomba ni vizuri ukaandika mahali ili usije ukasahau, usiyaombe kama mtu anayeropoka ili baadae Mungu akishakujibu usije ukawa umeyasahau.

Ndio maana ya yale maandiko ya umetegwa kwa maneno ya kinywa chako.
Nadhiri unapoiweka unatakiwa kuikumbuka na ikiwezekana kuiandika kabisa ili Mungu atakapokutendea haukawii kuitimiza mara moja.

Ndio sababu hata sadaka ya madhiri ilikua huruhusiwi kupeleka kilema, maaana yake ulikua huruhusiwi kupeleka iliyopungua.
Kama ukisema Mungu naomba unibariki milioni tatu na nusu yake nitakupa wewe, baada Mungu kukupa badala ya kupeleka milioni moja na laki tano ukapeleka milioni moja na laki nne unakua umempelekea Mungu kilema.

Wakati tunaanza kanisa kuna mahali tulitakiwa kununua kiwanja kwa shilingi milioni thelathini lakini wakati huo nilikua sina hela na ndio kanisa lilikua linaanza , kwasababu nilimuwekea Mungu nadhri kabla sijaanza kutafuta kiwanja Mungu alikua mwaminifu na tukafanikiwa kununua kile kiwanja.
Unapoweka nadhiri Mungu hakawii kuitimiza ili auone moyo wako ni wa namna gani.

Siku moja nilimuwekea Bwana nadhiri kwamba nikipata gari nitampa mtumishi wako, siku moja akaja mzee mmoja kanisani kutoka Mbeya alikua ameokoka na wakati naongea nae nikaikumbuka nadhiri niliyomuwekea Mungu, nikaingiza mkono mfukoni nikampa funguo ya Marcedez Benz niliyokua nayo, yule mzee hakuamini, nikamtafutia na dereva hapo hapo akamsaidia kuendesha kurudi Mbeya.
Yeye alikua hajui kwanini nimempa lakini kulikua na nadhiri ambayo nilikua nimemuwekea Bwana kwamba lazima niitimize.

Baada ya siku chache rafiki yangu mmoja akanipa Land cruiser VX, nikashanga sana na baada ya kunipa hiyo land cruiser na mimi nikaitoa kwa mtu mwingine na nikawa napanda daladala, lakini ni kwasababu ya nadhiri niliyomuwekea Mungu.

Mtu mwingine anaweza kufikiri nikiwanavyo kumi hapo ndio ninaweza kumtolea Mungu ili nibaki navyo nane, lakini Mungu anapenda kuuona moyo.

Watu wengine wanafikiri kuinuliwa na Mungu mpaka ufunge tu na kuomba peke yake, lakini kuna Zaidi ya hapo, kuna nadhiri na uaminifu  mwingi kwenye maisha ya watu wa Mungu mpaka uwe wa tofauti.
Watu wengine wamewahi kufunga na kuomba sana ili na wao warudishe misukule kama sisi lakini hawajafanikiwa ni kwasababu ya maisha yao ya ubinafsi na kutokuwa waaminifu mbele za Mungu.
Ni bora kutokuweka nadhiri kabisa kuliko kuweka halafu usiiondoe.

NAMNA NADHIRI LIVYO YA THAMANI MBELE ZA MUNGU

Mfano wa Yefta
Wafalme 11:30
Yefta aliweka nadhiri kwa Bwana kuwa kama Mungu akiwatia adui zake mikononi mwake wakati anarudi nyumbani chochote kitakachokuja kumpokea cha kwanza atamtolea Bwana kama sadaka ya kutekektezwa.
Alipoenda vitani Mungu akampa ushindi mkuu, aliporudi nyumbani binti yake wa pekee akaja kumpokea wa kwanza. Ikambidi amtoe binti yake kama sadaka ya kuteketezwa mbele za Bwana
Ingekua leo mtu angetafuta namna ya kutoroka, lakini hapa huyu binti wa ajabu akamuambia baba yke umtimizie Bwana nadhiri yako.

Mfano wa Hanna
Samweli 1:1
Hanna alikua hazai na alikua akichekwa na Penina mke mdogo wa mumewe, Hanna ameolewa kama mke mkubwa lakini alichelewa kupata motto ila mke mdogo alipoolewa akazaa bila matatizo nae akaanza kumdhihaki Hanna mke mkubwa.
Hanna alipoenda hekaluni kuomba akaweka nadhiri akasema Bwana kama utanipa motto mmoja tu nitamtoa awe mali yako Bwana, nitamuweka hekaluni akulie huko huko.

Siku moja nilifanya mkutano kule kampala kwenye kanisa moja linaitwa Kasubi kawala, akaja mama mmoja akiwa na shida kubwa na Mungu akamfungua katika shida yake, baadae nikamuuliza mama Mungu amekutendea haya utampa nini? Yule mama akasema mchungaji mimi ni masikini sina cha kumpa Mungulakini namtoa mwanangu awe mali ya Bwana nikamchukua motto nikamuweza kwenye kapu kubwa( nilitaka nione kama anamaanisha au anatania) nikasema mpelekeni ofisini tutamtafutia mahali pa kuishi na kula awe wa kanisani.
Baaada ya mkutano yule mama akabaki mahali pale hakuondoka kwenda nyumbani nikajifanya kama simuoni akawa anapita huku anaongea mwenyewe, baadae akasema namuomba mwanangu nikamlishe, tukamwambia ulishamtoa awe mali ya kanisa tutamlisha sisi yule mama akaanza akulia sana akasema nilimaanisha atamtumikia Mungu akiwa mtu mzima sio sasa hivi, ikabidi tumrudishie motto wake na kumsaidia.
Watu wengi wanasema tunampa Mungu maisha lakini wanakua hawamaanishii.
Unaposhindwa kuitimiza nadhiri inakuletea matatizo makubwa
Kumbukumbu la torati 12:11
Unapotaka kuweka kuitimiza nadhiri ni vzuri kuipeleka mahali pale ambapo bwana ameweka jin alake
Kumbukumbu 23:21

Mtu asiyetimiza nadhiri ni mpumbavu

Muhubiri 5:4

Unaposhindwa kuitimiza ahadi ya Mungu, Mungu anaanza kuiharibu kazi ya mikono yako.
Siku moja tulikua na mkutano Marekani na baada ya mkutano tulikua hatujui tatafikia wapi, lakini mimi nilikua nimemuwekea Mungu nadhiri.

Wakati tunatoka nikakutana na mchungaji ambae nilikutana nae Dar es salaama miaka mingi sana na nilimuozesha binti mmoja ambae nilikaanae nyumbani kwangu,  hapo hapo mchungaji akaniomba nikakae nae kwake na nikamuone binti yule ambae nilimuozesha kwake, tukawa temekwepa gharama za kuishi hotelini na Mungu akaonekana kwetu kwa namna ya ajabu.

Usiweke nadhiri na kushindwa kuiondoa ni bora usiweke.

Mtu mmoja alikua akaniambia anamuomba Mungu apate milioni sita na akasema akipata milioni mbili ataitoa kanisani, nikaomba nae na baada ya siku mbili Mugnu akambariki yule mtu milioni sita,,yule mama akanipigia simu akasema mchungaji nimepata ile hela sasa ile milioni mbili nikupe, nikamwambia hapana uilete kanisani siku ya ibada. Siku hiyo ya ibada nikamwambia mchungaji mmoja leo kuna mtu atatoa milioni mbili akiitoa nenda ukanunue viti, baadae mchungaji akaniambia baba ile hela uliyoniambia haipo. Bbada ya siku chache yule mama akapiga simu akasema alipata matatizo kwenye duka lake akaitumia ile milioni mbili kutengeneza duka lake na ataileta akishapata faida.

Baada ya siku chache yule mama akaachana na mumewake, akapoteza kila alichokuanacho na akaacha mpaka wokovu, hii ni kwasababu ya laana ya kutotimiza nadhiri

Paulo aliweka nadhiri akaitimiza

Matendo 18;18

Ilimimgharimu Paulo kunyoa kichwa chake ili kutimiza nadhiri


MAMBO YANAYOSABABISHA NADHIRI YA MTU ISITIMIE

Ø  Wakati unapomuwekea Mungu nadhiri unatakiwa kuendelea kuwa mwaminifu
u mbele za Mungu, unakuta mtu ameweka nadhiri lakini anaanza maisha ya dhambi, anaendelea na uzinzi na uongo na kutokua mwaminifu, unapifanya hivyo unafunga milango ya Mungu kuitimiza nadhiri hiiyo

Ø  Wakati mwingine Mungu anakua haruhusu jambo litokee kwasababu anakua anataka ukue, mrithi inahesabika kuwa kwama mtumwa ijapokua ni bwana wa yote akiwa bado motto, kuna watu wengine Mungu anajua akiwabariki leo wanamuacha, kwahiyo Mungu anakawia kuitimiza ili amtengeneze mtu vizuri ili awe chombo chema mbele za Bwana. Hivyo ndivyo Mungu anavyotenda kazi

Unapokubali kuwa chombo cha Mungu na kuyatenda mapenzi ya Mungu ziko Baraka zinazifuatana na wewe, ni kama ukiweka maziwa ya mtindi kwenye glasi baada ya kunywa yapo maziwa ambayo lazima yabaki kwenye ukuta wa glasi ndivyo ilivyo kwa mtu anayemtumikia Mungu unapofanyika Baraka kwenye maishaya watu wengine na kuwa mwaminifu kwenye mambo ya Mungu ziko Baraka ambazo ni lazima zifuatane na wewe.


“KATIKA JINA LA YESU BWANA UNISAIDIE KUTOKUWEKA NADHIRI, LAKINI NIKIWEKA NADHIRI NIITIMIZE”

Kwa masomo mengine kwa mfumo wa audio, vitabu na DVD
wasiliana nasi kwa namba
0716671440
0714729805
0718104333
0717727206

No comments:

Post a Comment