Sunday, September 7, 2014

KIFUNGO CHA AKILINA MAISHA YA WATU - Pastor Josephat GwajimaIBADA YA JUMAPILI TAREHE 7-09-2014

NA MCHUNGAJI KIONGOZI: JOSEPHAT GWAJIMA

SOMO: KIFUNGO CHA AKILI.
Mchungaji kiongozi J. Gwajima.

Watu wengi wanadhani Mungu ana nguvu na ana uwezo na ni muumbaji lakini wamesahau ana akili ameumba kwa akili na wale wanaomuabudu wana akili

 ZABURI 147: 5.

 5 Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu, Akili zake hazina mpaka. 
Mama Mchungaji Grace Gwajima

Tunaanza kuona Mungu ana akili na akili zake hazina mipaka wala hazichunguziki.

Sasa kuna kifungo ambacho unaweza kumwona mtu yuko vizuri lakini akili yake imefungwa. Sasa kwanini Mungu ametupa akili ni kwasababu kuna mambo mengine tunaweza kuyafanya kwa akili. Unaweza kumshuhudia mtu anakwambia jambo mpaka uka mshangaa jambo hilo hawezi kulifanya kwa akili ndio maana Mungu alivyowaumba watu akaweka mambo mengine tusimsumbue ila tutumie akili zetu. Shetani

naye anawafunga watu akili ndio maana ya kifungo cha akili. Ndio maana akili ya mahesabu ni tofauti na akili ya maisha na akili ya kufanyia bihashara nitofauti na akili ya kufanyia akaunti shuleni. Unaweza ukamkuta mtu anajua mahesabu lakini hana akili ya kuendesha kampuni.

Unamkuta mtu anaakili ya darasani na amekosa akili ya kutunza familia yake na ndio maana imeandikwa “enyi waume ishini na wake zenu kwa akili” unakuta mtu anaakili ya bihashara lakini hana akili ya kutunza familia yake na leo watu wa namna hiyo wanatakiwa wawe na akili kwa jina la Yesu. Mungu yupo kila mahali, kila sehemu kila mahali ulimwenguni kote na AKILI ZAKE HAZICHUNGUZIKI. Kama Mungu ana akili na akili zake hazichunguziki na amekuzaa wewe maana yake ulipompokea Yesu ukazaliwa mara ya pili baada ya kuzaliwa na wazazi wa mwili ukazaliwa kwa Damu ya mwanakondoo kwanini aliyekuzaa awe na akili alafu wewe usiwe na akili? lazima uwe na akili kama Mungu alivyo na akili. Imeandikwa “kila kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu” maana yake tunaamua kama Baba yetu, tuna rudisha kama Baba yetu, tu kama Baba yetu Mungu wa Mbinguni na sisi aliyetuzaa tuna asili yake.

Kuna baadhi ya majibu yako ndani ya akili yako. Ndio maana wazungu wanakuja Afrika kutuchezea kama toy wanatuletea miradi isiyo na maana ni kwasababu wana akili  ndio maana imeandikwa kwenye Biblia enyi wagalatia msio na akili ni nani aliye waloga?!

Mithali 3:19
19 Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara; 

Kuna watu wakianza kufikiria mambo ya maana wanaumwa akili na wengine wanahela mkonononi lakini hawajui jinsi ya kizitumia na kuna watu wanatumia akili za watu kufikiria na kufanya maamuzi na wengine wameibiwa akili zao hawawezi kufanya mambo ya kimaendeleo. Wengine wanasema eneo la thamani kubwa ni kaburini ambapo zimelala nyimbo ambazo hazikuimbwa,  kuna mahubiri yamelala ambayo haya kuhubiriwa, kuna ndege zimelala ambazo hazikutengenezwa.

Isaya 40:28

28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki. 
Wachawi wanaweza kumloga mtu akili yake na uchawi ni akili ya kishetani ambayo unafanya kazi ya kuzuia akili za watu.

Wagalatia 3:1-

1 Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? 

Kadiri unapozidi kupata maarifa unazidi kujijazia uoga maarifa kama ya kadiri unavyozidi kusoma unapatwa na uoga Fulani mfano ulipokuwa kijijini ulikuwa unakunywa maji ya kisima lakini sasa hivi unajua kuna backteria.  Magonjwa duniani yamegawanyika katika makundi mawili; magonjwa ya bacteria na virusi na yote yanaweza kusikia sauti ya Bwana Yesu kristo yakaambiwa ondoka nayaka ondoka na backteria yanaweza kutibika na virusi ndio hayawezi kutibika. Kuna backteria wazuri kama wale wanaogandisha maziwa yanganda lakini hawana madhara ni viumbe na tumepewa akili ya kuvitambua na kuviondoa kwenye miili yetu kwa jina la Yesu. Ndiomaana mfalme wa misri alipokuwa akipatwa na matatizo alikuwa anaita watu wa aina tatu wenye akili, wachawi, na waganga.

Kutoka 7:11

11 Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao. 

Wenye akili wanauwezo kuliko wachawi na waganga, akili ya kumwambia mtu jambo akalifahamu na kukubaliana nalo hiyo ni akili ya mtu. Unakuta mtu anatakiwa kuolewa na unamwona mtu hajawahi kunena na haonekani mkesha na hata kwenye ministry hayupo lakini ana gari zuri na kazi nzuri hapo hauhitaji maombi wala kumuuliza Bwana hapo unatakiwa utumie akili. Biblia inasema mtu akizaliwa akaishi miaka mia asipate chakula kizuri na asiishi vizuri ni afadhali mimba iliyoharibika. Mfano kipepeo anarangi nzuri lakini alianza yai akaja buu ambalo ni funza linaelekea kuwa kipepeo sasa watu wanaogopa buu, wanashindwa kupigana ili wafanikiwe. Maisha ni vita ya kupigana ili tupate kushinda.  Naamuru kwa jina la Yesu akili yangu iachiwe.

Kutoka 35:35
35 Amewajaza watu hao akili za moyoni, ili watumike katika kazi kila aina, ya mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu, na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yo yote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.
Mungu alikuwa anamwambia Musa katikati yako nimewaweka watu wenye akili wanaoweza kufanya mambo makubwa.

 

Kumbukumbu ya torati 1:15
15 Basi nikatwaa vichwa vya kabila zenu wenye akili, waliojulikana, nikawafanya wawe vichwa juu yenu, maakida ya elfu elfu, na maakida ya mia mia, na maakida ya hamsini hamsini, na maakida ya kumi kumi, na wenye amri, kwa kadiri ya kabila zenu. 
Kila mtu ni baunsa wa kitu fulani kwenye maisha, na pale ambapo mwanadamu amekufa na akili yake imelaza vitu ambavyo havijatokea. Biblia inasema Watu wanaomjua Mungu wao watakuwa hodari watatenda mambo makuu.

1 MAMBO YA NYAKATI12:32
32 Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao. 

 

Mungu alipokuumba wewe aliweka akili ndani uitumie wewe na kutatua matatizo yako. Adui mkubwa wa mafanikio yako ni mafanikio yako ya leo, unapofanikiwa leo usiridhike mwambie Mungu nimefanikiwa kwanza nataka  nitende tena zaidi. Kama rohoni mtu yupo vizuri ukimsikiliza mtu unajua mtu huyu atafika mbali. Wachawi wanakuja kwenye kichwa chako  wakati umelala wanaona kuna kiongozi mkubwa wa taifa yupo hapa na wanachukua hiyo akili ya uongozi wanaenda kuweka kwa mwanasiasa Fulani ndio maana mtu unamrudisha anakwambia nilikuwa Bungeni nyuma ya kiti  cha spika anasema alikuwa anamsaidia spika asiumbuke maana yake alipewa akili ya kuendesha Bunge, lakini sasa watu wa dunia hii wanakuja kuichuka akili ya mtu anayetakiwa kuwa spika anaendesha bodaboda kwanini? Ni kwasababu wameichukua akili yake wanaitumia mahali, alafu wewe utajuaje sasa kama akili yako inatumiwa sehemu

1.       Akili yako inapanga mipango ambayo wewe hutaki na hujawahi kuwaza kuifanya, Mipango inayopangwa kule kwenye akili yako inakujia na wewe umekaa na hujawahi kufanya hiyo unayoiwaza na huwezi jua kwamba akili yako inatumika mahali wamekunyanganya kile kinachokusaidia kutembea kwenye mafanikio yako. Shetani anatumia akili za watu walizopewa na Mungu kuendesha dunia hii atakavyo

2.       Kuna mtu amefunga akili yako hii ni pale unapoanza kupanga mipango ya maendeleo kichwa kinauma na unashindwa kuendelea kufikiria na hakuna nchi kavu ila kuna akili kavu na kama hujafanikiwa usimtafute mtu wa kumlaumu bali unatakiwa umwambie Bwana aifungue akili yako uitumie kuendelea. Unachotakiwa kuwa nacho kiko ndani ya kichwa chako hakiko mbinguni unatakiwa uombe naondoa giza lililotanda kwenye akili yangu.

Shule inaongoza akili ya mtu ili aweze kufanya jambo Fulani na sio inayoweza kumpa mtu uwezo wa kufanya jambo mfano magari haya yanayoonekana leo ni kwa kutumia akili ya mtu. Kataa kukaa pale ulipo na kuridhika uanze kwa kile kidogo ulicho nacho kwa kutumia akili. Mfano mwanzilishi wa kampuni ya Samsung kule korea ya kusini kama angekufa kabla hajatoa simu ungeenda kule kaburini kwake ungeona simu zote zimelala kaburini kama una macho ya rohoni. Sio kiwango cha elimu ndio kinakutambulisha wewe ninani bali ni akili ile uliyo nayo ndio inayokutabulisha, lakini kuna mashetani maalum ambayo yanakuja kushikilia akili ya mtu na lazima yatoke kwa jina la Yesu.
Kwa mamlaka ya Jina la Yesu ninaamuru akili yangu ilinayotumiwa na waganga achia kwa jina la Yesu akili yangu irudi, akili inayotumika mahali Fulani ninaamuru akili yangu irudi kwa jina la Yesu, akili yenye mipango ya kujenga kiwanda achilia kwa jina la Yesu, akili ya kusimamia kampuni ninaamuru irudi kwa jina la Yesu, wale wanaoilinda akili yangu isisimame ninaamuru waachie kwa jina la Yesu. Sehemu yeyote ambapo akili yangu inatumika ninaamuru waachie kwa jina la Yesu, ninrudisha akili yangu kwa jina la Yesu na wale wanaochukua akili yangu ninawafyeka kwa jia la Yesu. Akili iliyozuiwa na wachawi na mashetani niniachilia kwa jina la Yesu. Ninaamuru kwa jina la Yesu  wale wanaotumia akili yangu mahala popote ninawafyeka kwa jina la Yesu ninasimama kinyume na mjenzi yeyote anayetumia akili ya mtu kujenga utawala wake kujenga ninawateketeza kwa jina la Yesu, ile akili iliyojenga miji ya kishetani ninapindua kwa jina la Yesu. Akili inayowaza mambo ya mafanikio naamuru iamke kwa jina la Yesu. Imeandikwa watu hawa ni ‘watu walioibiwa na kutekwa’ ninaamuru akili iliyoibiwa irudi kwa jina la Yesu kristo kwa damu ya Yesu. Katika jina la Yesu nabomoa ngome inayozuia akili kwa damu ya Yesu. Naondoa wigo uliowekwa kwenye akili yangu kwa jina la Yesu, naondoa wigo wa hofu, naondoa wingi wa mashaka kwa damu ya Yesu. Ninabomoa madhabahu zao zinazoshikilia akili kwa damu ya Yesu. Akili ya kujua kitu cha kufanya, akili ya kufanya maamuzi, akili ya kuanzisha bihashara akili ya kujenga kiwanda, akili ya mipango, akili ya kufanya biashara ifunguke kwa jina la Yesu, akili ya ubunifu iamke kwa jina la Yesu, kifungo cha akili, kufa mipango naivunja mipango ya kishetani kwa jina la Yesu, akili za kishetani nazivunja kwa jina la Yesu.

Asante Mungu Baba, asante Bwana Yesu asante Yesu kwa kunipa akili asante Yesu kwa kunipa akili kwa jina la Yesu.

AMEN.

No comments:

Post a Comment