Tuesday, December 24, 2013

MAPEPO YAGUNDULIKA KUWA VYANZO VYA MATATIZO MENGI YA WATU

 
Akifundisha katika Mkutano wa maelfu ya watu Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima alieleza kuwa mapepo(mashetani au majini) ndio vyanzo vya matatizo yanayowakumba watu wengi leo hii. Baada ya kufundisha kwa dakika chache Mchungaji alianza kufundisha kwa vitendo na alipoanza tu mapepo yaliyokuwa ndani ya watu mbalimbali yalidhirika na baada ya uponyaji watu hao walielezea matatizo yalikuwa yanawasumbua muda mrefu ambayo yalitokana na kupagawa na pepo waliowangia ndani yao.
 
Binti mmoja  aliyefahamika kwa jina la Amina Salum (Chini katika picha) ambaye hapo awali kabla ya kuokoka alikuwa muislamu, alikuja katika mkutano wa Ufufuo na Uzima akisumbuliwa na magonjwa mbalimbali.

Akieelezea tatizo lake, Amina alisema kuwa alikuwa na tatizo la tumbo ambalo alikuwa akisikia kuwa tumbo linachoma choma ndani kiasi cha kushindwa kula. Tatizo ambalo lilimdhoofisha mwili siku hadi siku.

Wakati Mchungaji Gwajima akipita katikati ya makutano alimkuta amekaa na mapepo yaliyokuwa ndani yake walipomuona mchungaji wakadhihirika kutokea ndani yake ambapo na baadaye yalipewa amri yamtoke mtu huyo. Baada ya hapo dada huyo alipona kabisa magonjwa yake papo hapo.


Mchungaji Gwajima akiwa amemshika Amina baada ya kupokea uponyaji wake.

Wednesday, December 18, 2013

MISUKULE WAENDELEA KURUDISHWA KATIKA MKUTANO WA UFUFUO NA UZIMA

Ikiwa ni siku ya tatu ya mkutano wa Ufufuo na Uzima mjini Morogoro  maelfu ya watu waliendelea kuhudhuria huku uweza wa Mungu wa namn aya ajabu ukiendelea kudhihirishwa kupitia mchungaji Josephat Gwajima

Mchungaji Josephat Gwajima alifundisha somo la NYOTA YAKO INATUMIWA NA MTU. Akifundisha alisema kila mtu anayo nyota katika maisha yake au kipawa ambacho Mungu ameweka ndani yake ili kupitia hiyo aweze kufanikiwa

Lakini wachawi na waganga wa kienyeji wanakua na uwezo wa kuichukua nyota ya mtu na kuitumia kwaajili ya kazi zao binafsi, akielezea mtu aliyechukuliwa nyota ana dalili zipi, mchungaji Josephat Gwajima alisema unakuta kwa mfano mtoto alikua ana akili darasani lakini  baada ya kuchukuliwa nyota yake unakuta ule uwezo wote unaondoka na anakua hawezi tena kufanya vile vitu alivyokua anafanya mwanzoni.

Baada ya kufundisha mchungaji Josephat gwajima alianza kuomba maombi ya kuwarudishia watu nyota zao na baada ya hapo aliwarudisha wale waliokua wamechukuliwa msukule.
Jina:Rose Mwakipesile
Anaishi mzumbe alichukuliwa na wachawi na wakampeleka kariakoo ambako alikua akitumiwa na wachawi kufanya biashara kariakoo ya nguo na alisikia sauti ikimuita njoo akajikuta yuko mkutanoni

Jina :Esther Anatory
Anaishi Modeko alichukuliwa shimoni na kazi yake ilikua kunyonyesha watoto baharini alisikia sauti inamuita njoo akajikuta yuko mkutanoni

Jina:Flora Mizambwa
Alichukuliwa msukule akawa anakaa msituni alichukuliwa na mwalimu ambae hamjui jina lakini ni mwanaume anaishi mazimbu alikua hali chochote na alisikia sauti inamuita njoo akajikuta yuko mkutanoni

Latifa Jane
Alichukuliwa akakaa polini na alikua analimishwa na wachawi chakula chake ilikua pumba na damu za watu alisikikia anaitwa njoo akajikuta yuko mkutanoni na ameacha watu wengi huko

Jina:Pendo Bahati
Alikua uvunguni alichukuliwa na mama mkwe wa kaka yake, alimkuta shuleni akamchukua, sababu iliyopelekea kumchukua ni kwasababu alikua na akili darasani, yule mchawi alipomchukua akamgeuza mbwa mweusi kichawi na kumpeleka kwao akawa kama ndie yeye hapo nyumbani kwao

Ashura Mohamed
Alichukuliwa akakaa pangoni na alisikia sauti inamuita njoo akajikuta yuko mkutanoni anaishi kirakala


MCHAWI ANASWA KATIKA MKUTANO WA UFUFUO MOROGORO

MCHAWI ANASWA KATIKA MKUTANO WA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO


Ikiwa ni siku ya tatu ya mkutano wa ufufuo na uzima unaoendelea katika viwanja vya vya shule ya sekondari ya morogoro mchawi mmoja aliyejulikana kwa jina la Fatuma amekamatwa katika mkutano huo akiwa yuko katika shughuli zake za kila siku za kichawi.

Dada huyo aliyekamatwa na Nguvu za Mungu alielezea akasema alikuwa na wenzake ambao walitumwa na bosi wao ambaye ni mchawi na mganga wa kienyeji maarufu kutoka mjini Bagamoyo wilaya ya pwani kuja katika mji wa Morogoro kuchukua miili ya watu waliokufa katika nyumba za kuhifadhia maiti za hospitali(mochuari) kwa ajili ya kitoweo.

Akizungumza alisema yeye na wenzake walipoteana walipofika karibu na hospitali ya rufaa ya mji wa Morogoro ambapo ni eneo la jirani na sehemu mkutano unapofanyika, alipofika maeneo hayo alisikia nguvu inamvuta kwa nguvu na kumpeleka asipotaka yeye ndipo alipojikuta ametua katika viwanja shule ya sekondari ya Morogoro ambapo ndipo mkutano unapofanyika
Dada huyo aliyeonekana kuwa na wasi wasi alisema tulikuja mimi na wenzangu kwa usafiri wa njia ya fisi lakini tulipokaribia hospitali sijui nini kimetokea na mimi nikasikia nguvu zinanivuta nikajikuta niko mahali hapa

ALIANZAJE UCHAWI

Akielezea jinsi alivyoanza uchawi alisema miaka kumi na tano iliyopita alikua anaumwa ndipo alipoamua kuondoka kwao Babati(Manyara) kwenda kutibiwa mkoani Pwani kwa mganga aliyejulikana kwa jina la Idi. Alipofika kwa mganga aliambiwa akachume pilini dawa Fulani na aitafune, alipofanya sawasawa na maelekezo ya yule mganga ndipo alipojiona anaanza kuingiwa na ukatili usiokuwa wa kawaida na akaanza kupata hamu ya kula wanadamu wenzake, kuanzia siku hiyo ndipo alipoanza kuagizwa na Idi kwa ajili ya kufanya shughuli za kichawi pamoja na wenzake.

NAMNA ALIVYOKUWA AKITENDA KAZI

Yeye na wenzake walikuwa wanawashughulikia hasa watu ambao waliokoka na baada ya hapo wakarudi nyuma, akieleza jinsi walivyokua wakiifanya kazi hiyo alisema mtu yeyote aliyewahi kuokoka na baada ya hapo kumuacha Yesu anakuwa na majini mawili wanaotumwa kukaa ndani yake, na wachawi hawa wanapomfuata mtu huyo wanaongea nayale mapepo na wanayaagiza yamnyonge mtu huyo na mtu huyo anakufa mara moja

Katika utendaji kazi wake yeye ndiye aliyekuwa kiongozi wa kikundi chake hicho walichokuwa wanatenda shughuli hizo za kichawi.Alisema mimi niliwekwa kuwa kiongozi wa wenzangu kwasababu mimi nilikua nimefanikiwa kuwaua watu watatu waliokua wameokoka na kurudi nyuma. Kule kwenye uchawi mtu aliyefanikiwa kuwaua watu waliorudi nyuma ndie anakua na cheo kuliko wengine, mimi niliua watu ambao walikua hawajawahi kuokoka zaidi ya thelathini na waliokua wameokoka na kurudi nyuma watatu alisema dada huyo.

Akielezea alisema sisi tulikuwa na uwezo wa kuwaua watu kwa matukio tuliyokua tunayatengeneza, unaweza ukakuta mtu anatembea njiani alafu akawa kama ameumwa na nyoka lakini nyoka mwenyewe hamuoni, mtu huyo baada ya masaa machache atakufa na sababu itakuwa kwamba aliumwa na nyoka lakini sivyo tunakuwa ni sisi tumemtengenezea kifo ili tukamle nyama.

WATU ALIOWAHI KUWAUA

Alisema anakumbuka miaka mitano iliyopita alimuua mdogo wake aaliyekuwa anajulikana kwa jina la Udiyomboli, watu watatu ambao waliwahi kuokoka na kasha kurudi nyuma pamoja na wengine Zaidi ya thelathini aliowaangamiza kwa kutumia uchawi
Baada ya hapo dada huyo akiongea kwa huzuni aliomba msaada akasema, nimechoka kufanya uchawi siyapendi maisha haya na sitaki tena kurudi kule Bagamoyo.

Dada huyo tayari ameshaachana na mambo ya uchawi na amempokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake.

Tuesday, December 17, 2013

MOROGORO YAZIDI KUTIKISWA KWA UWEZA WA MUNGU
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima akifundisha aina nne za misukule siku ya pili ya mkutano Morogoro

John Lisu na waimbaji wenzake wakimtukuza Mungu ndani ya Morogoro

John Lisu akiimba wimbo wa Yu hai Jehova

Mchungaji Gwajima akifundihsa neno la Mungu ndani ya Morogoro

Baada ya kufundisha alianza kuomba maombi kwaajili ya kuwarudisha wote waliochukuliwa katika mazingira ya kutatanisha

Sehemu ya umati uliohudhuria mkutano


Ikiwa ni siku ya pili ya mkutano wa kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na mchungaji Josephat Gwajima mjini Morogoro maelfu ya watu wemehudhuria katika viwanja vya shule ya sekondari ya Morogoro kushuhudia mambo ambayo Yesu Kristo akiyafanya kupitia mtumishi wake.

Mkutano huo unaoanza kila siku ya saa tisa jioni ulionekana kuhudhuriwa na maelfu ya watu walioanza kufika uwanjani hapo mapema  ili kushuhudia yale mambo ambayo Mungu anatenda.

Mchungaji Josephat Gwajima aliongozana na waimbaji maarufu kama vile Flora mbasha, John Lisu na wengine wengi ambao walikua wakimtukuza Mungu wakati wa Mkutano.

Mchungaji Gwajima alifundisha somo la aina nne za misukule na baada ya hapo yalifuata maombi ya nguvu ili kuwarudisha watu hao waliokua wamechukuliwa katika mazingira ya kutatanisha.

Hali akiwa amejaa nguvu za Roho mtakatifu aliamuru watu waliokua wamechukuliwa msukule kurudi mara moja ndipo maajabu yalipoanza kutokea na kushuhudia watu ambao hapo kwanza walikua wamepotea na wengine walikufa zamani walipoanza kutokea mahali hapo. Ambao baadhi yao walishuhudia dakika chache baada ya kurudishwa kutoka msukuleni.

Wakazi wa Morogoro walionekana kushangazwa kwa namna ya ajabu jinsi Mungu alivyowafungua watu hao na kuwaweka huru kabisa kwa jina la mpakwa mafuta wake Yesu Kristo.

Uwanja mzima ulisikika kwa sherehe za shangwe huku watu wakimtukuza Mungu kwa matendo yake makuu aliyotatenda siku hiyo

Sunday, December 15, 2013

MKUTANO WA UFUNGUZI WA MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA WAANZA NA MAAJABU MJINI MOROGORO


Ikiwa ni siku ya ufunguzi wa mkutano wa Ufufuo na Uzima unaondelea katika viwanja vya shule ya sekondari ya Morogoro mkutano huo umeanza kwa maajabu ya namna mbali mbali na ya kushangaza.

Akifungua katika mkutano huo, mchungaji Josephat Gwajima alieleza kuwa Mungu amewaita watu kwa namna tofauti tofauti na anawatumia kadiri apendavyo, akasema yeye ameitwa na Mungu kuwarudisha watu wote waliokufa katika mazingira ya kutatanisha.

Aliendelea kusema kuwa yeye hapingi watu kufa lakini anachokataa ni kusema mtu amekufa wakati amechukuliwa na wachawi na yuko chini ya uvungu wa kitanda cha mtu.

Akasema huu ni wakati wa Bwana kuwarudisha watu wote waliochukuliwa katika mazingira ya kutatanisha na katika mji wa Morogoro ni wakati wa kushuhudia kwa macho yao mambo ambayo Mungu atayatenda kwa kuwarudisha watu waliochukuliwa katika mazingira tata.
Mchungaji aliwahoji baadhi ya watu waliochukuliwa msukule kutoa shuhuda zao, watu hao ni sehemu tu ya watu zaidi ya mia tano waliorudishwa kutoka msukuleni

Wakati mchungaji Gwajima akielezea  jinsi dada Nives alivyofufuka kutoka katika wafu, alimuita mdogo wake Nives ambaye anajulikana kwa jina la Dericdady ambae ndie aliyemuombea dada yake wakati amekufa na akafufuka ili awaonyeshe watu namna alivyoomba wakati dada yake amekufa.

Wakati kijana huyo akionyesha jinsi alivyoomba wakati wa kumfufua dada yake ndipo watu mbali mbali waliokua na mapepo walipagawa mapepo jambo ambalo liliwashangaza wengi waliokua wakitegemea kuona mambo kutotokea mpaka mchungaji aombe


Baada ya kuwahoji watu hao Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima alifundisha kuhusu DAMU INENAYO kwa ufupi, alisema ni vizuri kujua kwamba damu inauwezo wa kunena, akitolea mfano damu ya Habili alisema damu ina mambo makubwa matatu

  • Damu inanena
  • Damu inaponena Mungu anaweza kusikia
  • Damu inaweza kulia
Baada ya hapo yalifuata na maombi ya kuwafungua watu waliokua wamefunga na magonjwa na udhaifu mbali mbali

Mchungaji Josephat Gwajima hali akiwa amejaa Roho mtakatifu aliwaamuru watu wote waliokua na mashetani kukimbia mbele, hapo ndipo maajabu yalipoanza kutokea na Kuuona uweza mkuu wa Yesu ukijidhihirisha kupitia mchungaji Josephat Gwajima


Alphani Kiloko
alikua ana matatizo ya kuanguka mara kwa mara na baada ya hapo alikua hajui nini kinachoendelea , baada ya maombezi alifunguliwa na kuwekwa huru kabisa kwa jina la Yesu.

Sehemu ya umati wa watu waliopita mbele wakati wa maombeziKijana (mwenye fulana nyeusi) Alikuja kwenye mkutano akiwa hawezi kuongea(bubu) na baada ya maombezi akafunguliwa  na kuweza kuongea, neno la Kwanza kusema ilikua asante Yesu na baada ya hapo akaomba kwa kinywa chake chips mayai na soda

Moshi Rajabu (Kulia)
Alikuja kwenye mkutano akiwa na shida ya kupotelewa na mwanae katika mazingira ya kutatanisha lakini kabla hajapata muujiza wa kupokea mt0to wake alifunguliwa kutoka katika vifungo vya pepo wachafu

Neema Ayubu akiombewa na mmoja wa watendakazi wa UfufuonaUzima
Neema alikua na maumivu ya mwili mzima kwa muda wa mwaka mmoja, lakini leo baada ya maombezi akafunguliwa na kuwekwa huru kabisa kwa jina la Yesu

 
Makutano wakiondoka uwanjani mara baada ya mkutano

Thursday, December 12, 2013

MWANAMKE ANAYESAKIKA KUWA NI JINI AIBUKA NA KUTOWEKA MKUTANO WA MCH. GWAJIMA - JIJINI TANGA

Mkutano mkubwa wa Ufufuo na Uzima na mchungaji Josephat Gwajima umehitimishwa kwa tukio la aina yake lililosisimua watu waliohudhuria mkutano huo. Ni tukio la ajabu kutokea ikiwa ni siku moja tu mara baada ya mkutano wa Ufufuo na Uzima kuhamia katika jengo moja maarufu mkoani Tanga.

Pamoja na kufundisha kuhusu misukule, nyota, ndoto na kuhusu wafu; Mchungaji Gwajima alifundisha pia kuhusu majini na jinsi ya kuwashinda ambapo alisema wazi kuwa majini ni viumbe ambavyo ni vya rohoni na vinaweza kuvaa umbele lolote la binadamu au mnyama.

Sehemu ya Umati uliokuwa ukihudhuria mkutano wa Mchungaji Josephat Gwajima jijini Tanga.
Akinukuu hay ya kitabu cha Shehe Falsihi wa zanzibar alisema "majini ni viumbe vya angani ambavyo havina viwiliwili hivyo huwezi kuviona kwa macho, lakini vinaweza kuvaa ima umbo la kifuu cha nazi au umbo lolote" alisoma haya hiyo akieleza kuwa uislamu na ukristo wote unataja viumbe hivi yaani majini.

Wakati somo likiendelea kukatokea jambo la ajabu ambalo kwa tafsiri ya rohoni ilikuwa ni uthibitisho wa kile ambacho Mchungaji Gwajima amekuwa akifundisha katika jiji hilo la Tanga.

Mchungaji Gwajima alipokuwa akizunguka katikati ya makutano ili kuwafungua wenye vifungo, zilisikika kelele za watu zikipiga kelel kuwa kuna mtu amevaa ushungi yupo kwenye kona ya bati. jambo ambalo lilivuta hisia za wengi. Kwani mwanamke huyo alionekana na watu wote akiwa kwenye bati la nyumba moja ya ghorofa pembeni mwa jengo la kuabudia.
Watu waliokuwepo wakiwa wanamshangaa muda mfupi kabla hajatoweka..  (Ghorofani amezungushiwa rangi)


Ni kweli kuwa kwa ghorofa lile hakuna ambaye angeweza kupanda, wala kukaa kule juu na ukizingatia ni mwanamke. Watu wakiwa wametaharuki na wengine kuliitia jina la Bwana ghafla mwanamke huyo akatoweka mbele ya macho ya watu wote na kuweka hofu miongoni mwa watu wote.

NI NINI TAFSIRI YAKE?
Akiongea jumapili hii kanisani, Mchungaji Gwajima amesema jambo hili ni udhihirisho wa kile alichokuwa anakisema; na ya kwamba yeye alimwona mwanamke huyo kabla watu hawajamuona na kwa kuwa Mungu amekuwa amekuwa akimwonyesha viumbe vingi vya rohoni akahisi kuwa watu hawajamuona. Alisema, "Mungu amekuwa akinionyesha viumbe vingi vya rohoni wakati nahubiri na mara nyingi huwa sitaki kuwatia hofu watu hivyo hukaa kimnya bila kuwambia "
Muda mfupi kabla ya Mwanamke huyu kutoweka Camera yetu ilimnasa

Kumbe ilikuwa ni uthibitisho wa Mungu kuwa viumbe hawa wapo na pia wanaweza kuvaa miili ya binadamu kama vile walaika walivyovaa mwili na kumwendea Ibrahimu na hawa wanavaa miili ili kutekeleza haja zao duniani. Majini ni halisi lakini kwa jina la Yesu wameshindwa kabisa na Tanga imekuja kwa Yesu.

Wakati huohuo eneo jipya la kuabudia la nyumba ya Ufufuo na Uzima - Tanga lipo katika hatua za mwisho za ukarabati ili lianze kutumika shuhudia pichani.


Monday, December 9, 2013

KUWAFYEKA WATUNZA KUMBUKUMBU

                                                                                                       
Utangulizi

Kwenye biblia shetani anaitwa mshitaki wa ndugu. Ufunuo 12:10. "Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.".1Petro 1:8

Mahakama nyingi hazifanyi kazi usiku, lakini mahakama ya mshitaki huyu inafanya kazi saa ishirini na nne, .
Mtu hawezi kufungwa mpaka kuwepo na mashitaka, kwa kawaida mtu anapokamatwa na polisi huwekwa mahabusu, halafu polisi huandaa hati ya mashitaka na mtu hupelekwa mahakamani, kwenye mahakama za juu hati ya mashitaka huandaliwa na mkurugenzi wa mashtaka (DPP).  Na hati zinaandaliwa ili mtu afungwe.
Sasa shetani ndiye mkurugenzi(wa rohoni) wa mashtaka.  Zaburi 109:6, Uweke mtu mkorofi juu yake, Mshitaki asimame mkono wake wa kuume’.  kuna washitaki wakorofi. 

Mashitaka dhidi ya Yesu, pilato alikuwa mgumu kushughulikia  swala hilo sababu hakukuwa na hati ya mashtaka. Matendo 25:27 "Kwa maana naona ni neno lisilo maana kumpeleka mfungwa, bila kuonyesha mashitaka yale aliyoshitakiwa".  

Mtu hawezi kufungwa isipokuwa ameshtakiwa. 
Hakuna gereza analoweza kuingia mtu bila mashitaka.  Polisi ni watekelezaji wa sheria, ukifanya kosa unakamatwa, na ofisi wa DPP inaandaa mashtaka, hivyo hata katika ulimwengu wa roho kuna idara kabisa ya kuandaa mashtaka na mtu hawezi kufungwa na magonjwa,umasikini au shida ya namna yoyote mpaka yawepo mashitaka.

Kisa cha kweli

Mwaka juzi shetani alinitokea na kuniambia kwa kuwa tumeshampiga sana, basi sasa kila mtu achukue nyaraka zake twende mahakamani, mim nikawaza mahakama gani anayozungumzia..? kama ni ya Mungu, Mungu ni baba yangu na anakaa ndani yangu.. pia nikagundua unapoenda na shetani mahakamani lazima uwe makini la sivyo utaweza kuishia jela.
  
Kolosai 2:3-14 "akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;  akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;"

Yesu alipokuwa msalabani pia alifuta hati za mashtaka kulingana na hukumu zake Yesu!
 Iko hivi mfano Mungu amesema mshahara wa dhambi ni mauti, sasa wewe unapotenda dhambi mashetani wanaandika na wanaangalia kwenye sheria za Mungu wako wanaangalia mfano umezini, wanaenda mbele za Mungu na kushitaki kuwa huyu amezini na wewe umesema mshahara wa dhambi ni mauti tunaomba tukaitimize hiyo sheria.

Mungu akikaa kimya wanajua ndo imekubalika, mashambulizi yanaanza.  Mungu aliwahi kunionyesha jinsi mashetani yanavyoshtaki…
Shetani ni mkurugenzi wa mashtaka, mapepo ni watekelezaji wa hayo mashtaka.  Biblia inasema Mungu si mwepesi wa hasira, ila pia hawezi kumwacha mtenda dhambi bila adhabu.  

Yesu alipokuwa duniani aliletewa mwanamke aliyekuwa akizini, na wakamwambia kwa taratibu za kiyahudi huyu mtu anatakiwa apondwe mawe hadi kifo.  Yesu hakuwakatalia ila akawaambia ambaye hana dhambi awe wa kwanza kumponda mawe, wale mafarisayo wakaondoka mmoja mmoja ndipo Yesu akamwambia Yule mwanamke washtaki wako wako wapi? Kama wameondoka basi na mimi siwezi kukushitaki enenda kwa amani.

Kwa hiyo kilichomponya yule mwanamke ni wale washitaki wake kuondoka.  Washitaki ndio chanzo cha tatizo.  Hivyo hata wewe kwa jinsi unavyokuwa na washitaki wengi ndivyo kwa jinsi hiyo hiyo matatizo makubwa yatakavyokupata, kwasababu wana tabia ya kuweka kumbukumbu

Kuna idara maalum ya kumbukumbu, ambayo wanapotaka kukushughulikia wanayachukua na kuyapeleka kwa Mungu!  Yaani hiyo ni idara ambayo inasimamiwa na mapepo maalum wanatunza toka makosa ya mababu zako.  Hakuna gereza bila mashitaka.

‘Kwa jina la Yesu leo napiga watunza kumbukumbu wote, kwa jina la Yesu’

Kuna wengine wamefungwa toka tumboni kutokana na madhambi ya mababu na mabibi zao!  Mfano bibi  alikuwa mchawi, wanachofanya mapepo wanakwenda mbele za Bwana na kutoa mashtaka kuhusu familia yako.  Wanamwambia kwa kuwa bibi yake alikuwa mchawi na aliwazuia wengi kuolewa na huyu haturuhusu kumzuia kuolewa, Mungu akinyamaza tayari ndo tiketi ya wao kukuvuruga.  Mungu hawezi kukuadhibu ila mashetani ndo hutunza kumbukumbu na kwenda kukushtaki mbele za Bwana kwa kutumia sheria za Mungu.  Ndio mana inatokea mtu yanampata mabaya wakati hakutenda kosa lolote
"Kwa jina la Yesu, nashambulia watunza kumbukumbu wote wanaotunza kumbukumbu za familia yangu na ukoo wangu"

Saturday, December 7, 2013

MOROGORO KUTIKISWA NA UFUFUO NA UZIMA

Baada ya mikutano iliyovunja rekodi kwa idadi ya watu yaani Arusha, Moshi na Tanga; sasa kanisa la Ufufuo na Uzima linahamishia mikutano yake mkoani Morogoro ambapo Mchungaji Gwajima ambaye pia ni mchungaji kiongozi wa kanisa hilo anatarajiwa kuhubiri kwa siku nane mfululizo. 

Pamoja Mchungaji Gwajima atafuatana na timu ya watendakazi zaidi ya mia tatu na waimbaji maarufu wa injili kama Flora Mbasha, John Lisu, Jackson Benty na Mwanamapinduzi Band. 

Mkutano huo wa kwanza kufanyika Morogoro kwa kanisa la Ufufuo na Uzima unatarajiwa kushuhudia misukule wakirudi, wagonjwa wakipona, viwete wakitembea na mambo mengine mengi ya ajabu. 

Usikose kuhudhuria na wewe ili kupokea muujiza wako.


Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima

Thursday, December 5, 2013

ALIYEIANGUSHA MELI YA MV SPICE HIGHLANDER AOKOLEWA KUTOKA KWENYE UTUMWA WA SHETANI KWA NGUVU ZA MUNGU KATIKA MKUTANO WA MCH.KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA, JIJINI TANGA.

BINTI AITWAYE THERESIA AMBAYE ALIKUWA ANATUMIKISHWA NA SHETANI AELEZEA JINSI ALIVYOSHIRIKI KATIKA KUIZAMISHA MELI YA MV SPICE HIGHLANDER KWA NJIA ZA KISHETANI.
Theresia akiombewa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima ili kumuweka huru kutoka katika kifungo cha kumtumikia shetani, pia alikuwa anamatatizo ya miguu na hapa anaombewa kwa jina la Yesu.

Theresia ni binti aishiye Jijini Tanga na Mama yake mzazi, na siku hii ambayo alifunguliwa kutoka kuzimu kwa shetani alikuwa amekuja kwenye Mkutano wa Injili uliokuwa umeandaliwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima Jijini Tanga na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima.
Theresia akiwa analia kwa uchungu punde tu..baada ya kutoka kufunguliwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akiwa anamuhakikishia kuwa kwa sasa tayari yuko salama na hatochukuliwa tena...kwa maana kwa Yesu ni salam Daima..

Na baada ya Mchungaji Josephat Gwajima kuanza kuwaombea maelfu ya watu ambao walikuwa mkutanoni wengi walifunguliwa, na waliokuwa katika vifungo vya shetani, na  msukuleni walifunguliwa na kurejeshwa katika hali zao za kawaida.


Mchungaji Kiongzoi Josephat Gwajima akiwa na Binti Theresia pamoja na Mama mzazi wa binti Theresia

Theresia akiwa tayari kuanza kuelezea habari nzima..ALIFIKAJE KUZIMU 
Siku moja nilikuwa nimetumwa dukani na mama yangu mkubwa, wakati navuka barabara ghafula nikakutana na mtu ana kila kiungo katika mwili wale kikiwa kimoja kimoja , akajitambulisha kwa jina la Lucifer akanipa mkono ila nikakataa, akauchukua mkono wangu kwa nguvu akanikumbatia, nikajikuta chini ya bahari. Akaja mwenyewe  nikaogopa sana akaniambia nimekuchagua kwa sababu nimekuchagua hata kabla hujazaliwa. Kwa sababu una akili sana. 
Theresia akiwa anaelezea ushuhuda wa yale aliyaona katika ulimwengu wa kishetani.
Akaniambia nilipozaliwa aliniwinda sana ila alishindwa kunichukua kwa sababu bibi yangu alikuwa ananiombea sana . Lucifer akaniambia anataka niwe mke wa mtoto wake. Tukafunga ndoa  na baada ya miezi 6 baba yake akaniambia anaweza  kunipa nguvu nyingi sana lakini anataka nimtumikie yeye. Baada ya miaka 6 akanipeleka shemu Fulani ndani ya bahari ya pacific lakini ni chini sana, sehemu hiyo ni mji kama ilivyo miji ya huku.
Tukaingia sehemu Fulani tukamkuta dragon ambae alianza kuongea na Lucifer, nikafunga macho na nikajisikia kujawa na  nguvu sana, akaniambia amenipa nguvu na mamlaka ya kumiliki na kutawala fahamu za wanadamu.

Mama mzazi wa Theresia alianza kulia kwa uchungu sana baada ya kunza kusikia habari hizi za kutisha ambazo mwanae wa kuzaa ameyapitia.


Siku moja niliamka asubuhi nikiwa na njaa sana kwa sababu usiku wake sikula chakula, Lucifer akaniambia kuna meli inaitwa Mv spice nikaenda na baadhi ya watu tukatega nyaya za kopa, ile meli ikawa inakuja tukatega pale maji yanapogawanyikia  ili watu waseme ni mkondo wa maji, kuna maneno nikayasema halafu nikasimama pembeni, ile meli ikaanza kuzama mpaka kwenye kina cha chini kabisa cha bahari ambacho nilitaka mimi, kisha  tukaunganisha mabomba mpaka kule pacific na tukapata damu nyingi sana. Mimi nilikuwa nahitaji kunywa damu kiasi cha tani 5000 kwa siku ili niwze kutena kazi kwa nguvu nyingi.

Theresia akiendelea kuelezea huku mama mzazi akiwa anaendela kusikiliza kwa umakini wakiwa na Mchungai Josephat Gwajima

Pia kazi yetu nyingine ilikuwa kuwafanya watu wanaompenda Mungu waache kabisa na kuanza kuwaza vitu vilivyo tofauti kabisa na mapenzi ya Mungu, na waliuwa wakiifanya kazi hii kwa ku-control akili na fikra za wanadamu, yani utawala mkubwa  wa shetani ni kuzishika na kuzikamata fikra za wanadamu ili watende mambo ya kumchukiza Mungu na kujiondolea neema ya Mungu, na walikuwa na uwezo wa kumfanya binadamu atende jambo lolote baya iwe kuuwa,kulewa kutokwenda kanisani.

ULITOKAJE HUKO?
Nakumbuka ilikuwa muda wa kulala huko kuzimu kama kawaida huwa tunalala ila siku hii ikawa tofauti kwa maana nilianza kusikia sauti za watu wanaita njooo njoooo kwa jina la Yesu, mara nikasikia nguvu zinaniishia na nikawa sijielewi kabisa mara nikashanga nimetokea katika viwanja vya tangamano.
Mama yake Theresia anasema kabla ya mtoto wake kurudi alikuwa na matatizo ya kuumwa magojwa yasiyoisha ya kila wakati. Pia alikuwa na tabia ya uvivu na kulala sana , pia hakupenda kusali kabisa, pia kipindi cha mitihani aliugua sana, mama yake Theresia aliongea haya huku akibubujikwa na machozi maana alikuwa hajui kama alikuwa anaishi akiwa na picha picha tu ya mtoto wake na kumbe mtoto halisi alikuwa yuko kuzimu tena ameolewa na shetani na anaifanyia Dunia mambo ya ajabu ya kuiteketeza.
Theresia akimshukuru sana Bwana Yesu kwa kumuokoa na kumrejesha tena katika ulimwengu huu...maana alikiri amekuwa akitafuta ukombozi kwa muda mrefu...

Theresia akiombewa na Mchugaji Kiongozi Josephat Gwajima na Mchungaji Mwandamizi Eng.Yekonia Bihagaze ili kujazwa roho mtakatifu baada ya kuongozwa sala ya toba na kummpokea Yesu kwa Bwana na Mwokozi binafsi wa Maisha yake.

Theresia akiwa amejazwa roho mtakatifu na akinena kwa lugha.
Mchungaji Josephat Gwajima akitoa ufafanuzi.
Shetani anauwezo wa kumuona mtu na maisha yake,vipawa na karama ambazo Mungu amempatia mtu tangu akiwa tumboni mwa mama yake, na ndio maana Theresia alivyofika kuzimu akaambiwa amekuwa akitafutwa siku nyingi sana toka akiwa tumboni ila maombi ya bibi yake yalimkwamisha kuchukuliwa mapema.
Mchungaji Josephat Gwajima akifafanua.
Pia mchungaji Josephat Gwajima aliendelea kuelezea kuhusu kazi hasa aliyoielezea Theresia, Theresia alisema kuwa alikuwa anauwezo wa kuwashikilia fikra, akili na fahamu mwanadamu yeyote..ni hio ndio nguvu hasa ya utawala wa kishetani, kwa lugha nyingine ni typical LUCIFERIC KINGDOM agenda kucheza na mawazo ya wanadamu na kuwapandia mapando ya mawazo ya ajabu ya kutenda dhambi,na ndio roho ya Mpinga Kristo inavyotenda kazi (THE ANTICHRIST)
Mchungaji Josephat Gwajima akiwa anasisitiza kuwa ni lazima kila mtu awe na uwezo wa kuomba na kuishinda roho ya mpinga Kristo na kuushinda ule uwezo wa Shetani wa kumvuvia mtu kufanya maovu, kwa maana shetani ndio anayesababisha mambo yote maovu kufanyika na mwanadamu..

Hapa Mchungaji alikuwa anamaanisha,kwa mfano shetani akiwa anataka kumtumbukiza mtu kwenye ulevu,hawezi akawa anamshushia pombe kutoka mawinguni zimjie alipokaa...bali atamuingizia wazo la kunywa pombe na kumshawishi kuwa anakibali cha kunywa na ndipo mtu mwisho wa siku unamkuta kalala kwenye mitaro kapoteza fahamu kwa ulevi au kafa kabisa...lakini chanzo ni uvuvio wa kishetani kwenye akili ya mwanadamu.

USHAURI ANAOTOA THERESIA KWA WATU WENGINE
Watu inabidi wamtafute Yesu kwa kiwango cha juu sana, kwa sababu yeye ndiye atakayeweza kuwapa kila kitu wanachokihitaji, pia anasema vijana wengi wapo kwenye hatari ya kuangamia hivyo kama hawatamtafuta Mungu hakika wataangamia .

Theresia akiwa anamsifu Mungu kwa Nyimbo kwa maana kuwa kumbe alikuwa anakipaji cha kuimba pia lakini kumbe shetani alikuwa amekifunika.

Pia anamshukuru Mungu kwa kumrudisha kutoka katika vifungo vya shetani maana yeye mwenyewe ilikuwa ni ngumu sana kutoka huko, anachoweza kufanya ni kumtumikia Mungu na kumpenda daima na akaahidi kumuimbia Mungu siku zote kwa kuwa Mungu ndiye mkombozi wake.AMEN